Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

Hio ni uongo mkubwa Sana, unajua ukishatoka unaongea kirahisi rahisi Sana. Kilimo kwa hii nchi ni jipu kubwa Sana, ati laki 5, ukalime upate 2m labda kenya kwenye uhakika WA soko but sio bongo tikiti zaozea pale kariakoo, kweli kabisa laki 5 ikuvushe miezi 4 ukisubiria kuvuna,
Watu tunalima bhana na ukweli twaujua, mfano kuhudumia nusu heka tuu ya nyanya mpaka uvune sio chini ya kilo 8, hapo hujaweka kula yako, kama una watoto hapo hutaacha ona rangi zote. Halafu unashangaa utauza creti buku tano.
Msichukulie vitu kirahisi rahisi hivo.


Word son...

Jamaa ameongea bila research ameongea fantasy......

Nawambiaga watu mara nyingi tuchunge midomo zetu tuangalie maneno ya kuongea wakati mwingine bora kukaa kimya tu mkuu
 
Kama wewe Masanja mungu amekujalia ukalima ukafanikiwa mshukuru mungu sana hiyo bahati kwani kama ni kulima robo tatu ya watanzania ni wakulima lakini mpaka leo hawaja fanikiwa mim ndugu alilima mahindi ekati 200 yalikauka yote mpaka na alikufa kwa presha kwahiyo sio kila alimae anatajirika bahati pia kwani wakulima wote mnaolima huko mbarali wote ni mataji kama wewe ukipata shukuru acha kejeli kwa ambao hawaja fanikiwa



Massanja anaanza kunitia wasi wasi juu ya personality yake...

Now I am thinking aloud,
Donald Trump ni tajiri balaaa lakini hanaga story za kejeli pasipo kuwa na facts kuhusiana na kejeli yake
 
Inanikumbusha Jacky Cliff na nyodo kwenye Nirvana kuwa anavaa designer stuff km Kim Kardashian, kwake ni no fake zone.
Hakuna marefu yasokuwa na ncha
Mtuwachee wenye vipato halali na tunaipa serikali hady kodi


Angesema anaiingizia taifa kiasi gani na ame ajiri watanzania wangapi kwa kilimo ange ni motivate hata mimi lakini kwa hapa ame ni alert about his personality
 
Atakua anazungumzia kilimo cha kwenye Play Station.

Kule kila kitu kinawezekana hata Mwaikimba kuwa mchezaji bora wa dunia kwenye PS inawezekana.
 
Sikuwahi kudhani masanja ni mpuuzi kiasi hiki, kuna wazazi wa watu wanalipwa chini ya hiyo laki tano na wanasomesha watoto na wanategemewa na jamii zao, kupata kwako isiwe dharau kwa wenzako huyo aliyekupa hashindwi kukunyang'anya usidharau wasio nacho bwege wewe
 
Sikuwahi kudhani masanja ni mpuuzi kiasi hiki, kuna wazazi wa watu wanalipwa chini ya hiyo laki tano na wanasomesha watoto na wanategemewa na jamii zao, kupata kwako isiwe dharau kwa wenzako huyo aliyekupa hashindwi kukunyang'anya usidharau wasio nacho bwege wewe
Mpuuzi ni ww jamaa
 
Swala ni ku save money na kufanya kitu tofauti ili kipato kiongezeke hata uki save kidogo kwa siku ktk long run hela utaiona tuu si lazima ukafanya kilimo au ukaanza na laki tano izo ni chenji aisee...
 
Hivi why mtu akishafanikiwa ndio anajifanya kuwapa watu nondo ya kupiga hela!?? Why asitoe wakati anaaanza.
Roman abromavch aliongea ukweli kuwa aliuza vitu vya magendo sana ndio akafika alipofika.je are yu ready to do the same.
The problem watu wakishatoka hawaelezi ukweli kuhusu huo utajiri wao....just bla bla ukiwaambia wengine kuwa mafala.
Wengine wanatumia huo utajiri wao na emotional stories kupiga PESA zaidi. Watu walikuja busy kununua kitabu cha poor dady rich dady wanadhani wanweza kufanikiwa like him but hawakujua dunia nzima kadri mnavyonunua vile vitabu ndio mnamuongezea huyo jamaa utajiri.
Sijawahi sikia testimony ya mtu kuwa kile kitabu kilimsaidia kupata utajiri.
Kila biashara ina mkono wake na kila mtu anasehemu yake ya kutokea usimlaizimishe mtu awe polis,mkulima,mfanyabiashara ili afanikiwe.
Just let pipo be ni sio kuwadhalilisha.
And why Masanja usngle picked BANK teller alone. Mi sio bank teller but umewadhalilisha kabisa.
 
Mimi ni ninafanya kazi inayoendana na hiyo na pia ni mkulima..
Mitaji yote nayoipeleka shamba inatokana na kakazi kangu hako hako..
Faida kiukweli naiona ila si kwa namna ambayo mwandishi anajaribu kutuaminisha apa.. amesema iyo lki 5 unakodi shamba la ekari 13!!!!!? wapi.. then ukikodi initial investment unaifanyaje, au unakodi alafu watu wachezee kigodoro???
ilo tanki la maji la bei hiyo umeliona wapi..
Hayo maji anayapata wapi ya kuanzia...
Full of fantasy..
Mwanzoni kabla sijaanza kilimo miaka kama 6 iliyopita, watu walinipa hamasa sana ya kilimo..
Wakanipa na mahesabu yao ya kwenye madaftari.. nikawa na too much expectations kuliko reality..
Daa kuja kuvuna nikapatwa na homa kabisa..
Nikajipa moyo nikajaribu tena kikanuka..
Nikajaribu kwingine kikanuka..
Hapa kote nilikua napata experience baadae nikaanza kupatia zaid na zaid, mpk sasa si mbaya sana japo si hesabu zile tunazopigiana na kudanganyana tukiwa bar..
BTW aliyetoa hii statement si masanja ni mtu tu ambaye alimtumia masanja kujustify anachoamini..
Masanja ni mjuaye mimi ni very brilliant..
Hawezi kuongea ushuzi huu..
NIMEMALIZA
 
Huyu jamaa ametakatisha pesa yake shamba weeee, now naleta dharau kwanini usimsaidie hii mipango yule jamaa ako wa tbt anayeendesha lori! Yule mtoto wako kashapona uchizi mbona humpeleki hospital....
 
Masanja anaweza akawa hajatoka kimaisha kwa style hii ( kilimo) lakini atleast katoa stairs+ advise jinsi ya mtu kutoka au kujikwamua na umaskini!....naona watu wanamponda tu badala ya watu kuchukua mchele na pumba zake zikaachwa, to me kudos Masanja!
 
Wakuu hayo maneno sio ya masanja! Hiyo msg imetumwa sana kwenye Whatsup siku hizi za karibuni!

Nami nilitakata kuuliza, hayo ni maneno ya Masanja au mtu mwingine aliyemtumia Masanja kama mfano wake?
 
View attachment 328257

SHULE BILA ADA:

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

Je laki 5 yako, unafanyia nini?

#letitshine
tatizo wabongo wakishapiga pesa za kampeni na pesa za kujipendekeza kwa vigogo na watoto wa vigogo wanasingizia kilimo kimewatoa wanasababisha vijana maskin kwenda kula hasara shambani
 
Back
Top Bottom