Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

Mikoani ni kuzuri kwa Maisha ya kati kupiga hatua kuliko Dar es salaam.Dar Maisha yana maihitaji mengi sana!!. Mkoani kwa mfano Mimi natembea kwenda kazini. Sina mambo mengi ya anasa au peer group kushindana kimaisha. Ninachopata ni kuongeza elim, kupereka Shamba, na kuwekeza kwenye biashara ndogo. Vijana Mikoani ni kuzur, Mimi nawaambia, nimezariwa dar, nimesoma dar, nimefanya kazi dar, lakini kwa Mshahara wangu wa 521,000/, Dar kumenishinda.Lakini huku Mkoani Miti yangu ipo vizuri, Nakura ninachokitaka, nakunywa ninachokitaka, nauzuria harusi za marafiki ninazozitaka huku. Sio siri vijana Mkoani ndio deal, njooni tufanye kazi na kulima. Baada ya miaka 8 tutakuja Dar tumejaa.
 
Huu uzi ni mawazo ya mtoa mada kwa asilimia Mia moja. Sio masanja aliyeyasema haya.
Hilo bandiko ni bikira wa kisukuma alieandika lakina naona kila mtu anamtupia lawama masanja....mtoa maada naona ana agenda yake na masanja
 
Mimi niliwahi kulima mihogo ya KAEMP ina soko sana huko UGANDA, nililima miche elfu tatu, nlipo vuna, nikapata karo nikaja hapa Dar nikajiunga na chuo cha ualimu STMARYS nimemaliza nasubiri post, kazi ya kilimo hiyo. Big up Massanja
 
Msiwe wakatishaji tamaa wadau,,wengine ndo kwaaanza tunataka tuingie kwenye hyo tasnia ya kilimo.Tatizo lenu mnawaza mnawaza leo tu na kesho,hamuwek plans za muda mrefu
Tunakukatisheni tamaa sio?
Rudi usome vizuri hizo nadharia za masanja then ingia kwenye game na hicho kiji500k after 3-4months uje na mrejesho hapa.
Hakuna mkulima anaewaza mafanikio just overnight. Kwanza kitendo cha kuforsake starehe na maisha ya mjini hasa kwa kijana is more than being focused with goals in fore future. Usikurupuke joh, usije poteza muda wako.
Kama umedhamiria kuja shamba, hata leo hii ukitaka njoo ntakupa shamba bure tena lenye uhakika wa kuvuna mazao yako.
 
masanja nakurushia kifurushi cha mwezi uendelee kutumbua majiou, sijui vijana wamekula maharage ya wapi! wameng'ang'ania mjini bora wadhalilike wadowee lakini kujitoa mhanga kuanza maisha yao hawataki!

Alowambia mjini ndo kila kitu kwa watu ambao hawana chochote nani? kupenda vilivyoko tayari tuu

mwishowe ndo kulalamika daily maisha magumu, serikali mbaya, wewe umejaribu nini haswa serikali ikakukwamishaa? kazi kulalamika mitandaoni, mitaani kila mtu utamuona mbaya kumbe hujielewi maiaha unayalazimisha lazima yawe sehemu ambayo haifaiii
 
wabongo bwana. laki tano ni mfano na benki teller pia ni mfano!!
Mkuu ishu sio mifano aliyoweka huyu mpayukaji!
Cost analysis ya hizo opportunity haiendani kabisa na yield/returns alizotamka.
Huoni kuwa ni porojo za kulewa mafanikio?
Kila mtu alieko mjini anasrumble kupata mtaji wa uhakika na ieleweke wazi kuwa Bongo hii kuna fursa kibao za kumtoa mtu provided una capital in hand.
Masanja aache kuropoka, anajua njia alizopitia hadi kufika hapo na ibaki kuwa siri yake kama jinsi walivyo watu wengine wenye mafanikio.

Nafikiri umenisoma vizuri mkuu!
 
Waalimu na polidi wetu nao waache kazi wakalime? Kwa sababu wanalipwa chini ya hiyo laki 5
Hivi kuna police kwa sasa anakula chini ya laki tano.....hata ambaye elimu yake ni form four anavuta zaidi ya hiyo sasa mwenye degree ndo usiseme wewe jiulize kama anapewa posho tu laki tatu....tu source mchizi wangu askari
 
Kwahiyo atawaambia watu waache kazi za laki tano, au atawaambia waajiri waongeze mishaara?.
 
Masikini akishapata lazima ... ilie mbwata. Hivi Masanja wakati unazunguka na bidhaa jijini ukiwa mmachinga hayo mashamba yalikuwa yamekwisha huko kwenu Ludewa. Leo hii unabeza kazi za wateja wako waliokuweka mjini kitambo.

Kila kazi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na mzunguko wa life kiujumla, ni mpuuzi pekee awezaye kufikiri wote tunaweza kulima nyanya au auze maji na wote tuwe na maisha mazuri. Hao wanaolipwa laki 5 wote wakitoka ofisini wakauze maji au kulima vitunguu atanunua nani?

Kilimo kingekuwa simple kama unavyobwatuka unadhani nani angekuja mjini kufanya kazi ya laki 5 unayoibeza, mbona Masanja ulikuja ukakomaa hapa hadi ukatoka baada ya kuungua sana na jua. Ulishakuwa hadi HOUSEBOY wewe, leo hii teller wamuona kama hana akili au hana malengo na maisha haya.

Mmekaa tu mnaongelea kilimo kana kwamba ni rahisi saaana. Mngejua watu wanaozewa na mazao mashambani huku kwa kukosa masoko. True vipo vinavyolimwa vinalipa haraka lakini havistawi nchi nzima na kwingineko gharama za kuvilima si ndogo.

Masanja hukutoka kwa sababu una akili kuliko vijana wanaosota,huo ni mzunguko wa maisha tu na bahati iliyochagizwa na kipawa. Ulijituma ndio lakini haimaanishi wasiotoka hawajitumi. Chunga kauli zako bro.
atakuja kufilisika tu uyu ngoja mtaona,...pesa ya kampeni na ya original komedi ...ngoja achuje ataona ...madharau sometime si mazuri..yeye alitoka kwa kulima nyanya..anachokiongea kinaongeleka ila hakina reality ...haiwezekani..ingekuwa hivyo tusingeenda skuli... tungelima tu basi...
 
Back
Top Bottom