Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

Masikini akishapata lazima ... ilie mbwata. Hivi Masanja wakati unazunguka na bidhaa jijini ukiwa mmachinga hayo mashamba yalikuwa yamekwisha huko kwenu Ludewa. Leo hii unabeza kazi za wateja wako waliokuweka mjini kitambo.

Kila kazi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na mzunguko wa life kiujumla, ni mpuuzi pekee awezaye kufikiri wote tunaweza kulima nyanya au auze maji na wote tuwe na maisha mazuri. Hao wanaolipwa laki 5 wote wakitoka ofisini wakauze maji au kulima vitunguu atanunua nani?

Kilimo kingekuwa simple kama unavyobwatuka unadhani nani angekuja mjini kufanya kazi ya laki 5 unayoibeza, mbona Masanja ulikuja ukakomaa hapa hadi ukatoka baada ya kuungua sana na jua. Ulishakuwa hadi HOUSEBOY wewe, leo hii teller wamuona kama hana akili au hana malengo na maisha haya.

Mmekaa tu mnaongelea kilimo kana kwamba ni rahisi saaana. Mngejua watu wanaozewa na mazao mashambani huku kwa kukosa masoko. True vipo vinavyolimwa vinalipa haraka lakini havistawi nchi nzima na kwingineko gharama za kuvilima si ndogo.

Masanja hukutoka kwa sababu una akili kuliko vijana wanaosota,huo ni mzunguko wa maisha tu na bahati iliyochagizwa na kipawa. Ulijituma ndio lakini haimaanishi wasiotoka hawajitumi. Chunga kauli zako bro.
Uko sawa mkuu
 
Sawa wewe unayo elimu nenda kalime vitunguu
Simanjiro sijui utaishi shambani.... Sijui utalima kwa mikono... Mbolea utainya... Maji utakojoa.... Baada ya kupinga hoja kwa hoja unaleta dhihaka.... Haya nenda sikonge kalime vitunguu ulale stand.....
Elimu, elimu, elimu, hapo katoa mfano WA laki tano akimaanisha kuwa hata kwa hela kidogo Tu unaweza tajirika na si lazima uanze na kidogo
 
Wanaotaka kulima zao lolote lile wanione..nipo kibaigwa naweza kumpa akili ya kutoka...awe na moyo na apende kilimo...tikiti..kitunguu nyanya hoho...mana ktk ekari mbili watu hupata hadi million 20 na zaid kwa muda wa miez 4 ~6...0759313890... pia nikiwa kama mtaalam wa mifugo ntkupa njia za kufuga baadhi ya wanyama ukatoka...mfano rfk zangu wanamiliki hadi million 100... najua huwez kuamin lkn nitafute uone vile walivyo...yani mimi ni mtumishi naona aibu sana nipo kama zombi sina lolote wakati mkulima anamiliki pesa ndefu nyumba nzuri gari nzuri
 
very good huo ni ushawishi wa hoja ni nguvu ya hoja...unaweza from zero to hero.🙂🙂🙂🙂
 
Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka ROBY ONE FASHION? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda NEW MAISHA na sehemu nyingine zinazofanana na hizo Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

HESHIMA kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

AMKA NAONGEA NA WEWE[emoji117] [emoji117] [emoji117] [emoji117]

Je laki 5 yako, unafanyia
70a9b6fc5d2ec1eb9e69893edf004d76.jpg
nini?
nimemuelew sana mtoa mada amejaribu kutuonyesha kuwa laki tano ni pesa ndogo sana kwenye mawazo ya watu ila kiuchumi ni pesa kubwa kabisa....amajaribu kutoa mifano ya biashara zake ila sio lazima ufuate mawazo yake ya kibiashara wewe tafuta wazo kisha wekeza wazo hilo kwa sh laki tano
 
laki tano kama unalo banda unaanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji au nguruwe jike mwenye mimba
laki tano we ni tajiri mbonaaa
 
Huwa napenda chungu tam kama hizi yaaaniii zinaniipmresss na mm nazidi kupata morale ya NINAWEZA
 
Jamani mi nafikiri mtoto wa kuku amejaribu kuonyesha njia kua hata ukiw na mtaji mdogo uneza fanya mambo yakuingiza pesa nyingi zaid, hana maana kua ni lazima hyo ela uilimie matikiti, tuache mawazo mgando tuamkeni jaman
 
Na kuhusu masanja alisema mwenyeweee mafanikio alionayo ni kwa sababu ya kilimo sasa kwann na ss tusiiige mifano mizuri kama hyo tutengeneze mkwanjaaa
 
Back
Top Bottom