Kwetu sisi watanzania maji na umeme havina umuhimu wowote ule. Sisi wananchi tumesema

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,017
12,305
Sisi wananchi Watanzania kwa kauli moja tunasema" Tunapenda tuendelee kuishi hivi hivi miaka yote"

Maisha ya sasa tunayoishi bila umeme wa uhakika wala maji ndio maishi bora kwetu.

Huo umeme, maji kwetu hauna umuhimu wowote kazi zetu wala hata hazihitaji kabisa matumizi ya umeme wala maji.

Hakuna faida yoyote ile tunapata umeme ukiwepo zaidi ya hasara tu nashukuru Tanesco kwa kutambua hilo sasa umeme hakuna maisha yetu yamekua bora sana.

Tunapenda kuiomba serikali isilete umeme wa uhakika hali ibaki hivi hivi kwani ndio maisha tunayo penda Watanzania.

Nanyi serikali si mnaona hakuna umeme wa uhakika wala maji ya uhakika lakini mmetuona sisi wananchi wenu wa Kitanzania tukiandamana kupinga hayo ? Natumai jibu ni hapana.

Basi mjue haya maisha sisi ndio tunaya penda hatutaki kabisa umeme wa uhakika utaleta hasara katika kazi na biashara zetu. Tunataka umeme wa hivi hivi ndio tunaupenda sisi wananchi wa Tanzania.

Hatuta andamana kamwe kupinga hali hii bali tunaipongeza serikali kwa kutuletea umeme wa kususua tunao upenda na wenye faida kwetu.

Sisi wananchi kwa pamoja tunasema tunaipenda serikali kwa kutusikilisa kwa aina ya umeme tunao utaka sasa mambo yapo vizuri, Pongezi ziende kwa serikali.

#Hongera serikali kwa kazi nzuri, Kazi iendelee, mitano tena
 
Pongezi kwa Mwenyekiti wa Chama
 
Back
Top Bottom