Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amesema kuwa serikali haiwezi kusema ni lini mgawo wa umeme utakwisha

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu watanzania ,

Hiyo ni taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu akiwa mkoani Mbeya ,kuwa serikali haiwezi kusema ni lini mgao wa umeme utakwisha bali inachofanya serikali yetu kwa sasa ni kufanya juhudi za kuongeza vyanzo vya umeme kama vile umeme unaotokana na jotoardhi.amesema kwa muda mrefu serikali na Taifa lilikuwa linategemea vyanzo vitatu katika kuzalisha umeme ambavyo vilikuwa ni maji,mafuta pamoja na gas.

Lakini sasa serikali imeamua kuongeza vyanzo vingine vya nishati ya umeme ikiwepo hii ya joto ardhi ambayo ni ya uhakika,endelevu na salama sana kwa matumizi.na kwamba serikali itaongeza kasi katika kukamilisha miradi hii itakayotupatia na kutuwezesha Kuongeza megawati zitakazo unganishwa katika grid ya Taifa.

Amesema ya kuwa kwa sasa matumizi ya umeme yameongezeka sana kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi na kwamba kwa sasa umeme siyo suala la anasa bali ni matumizi na huduma ya lazima kwa mtanzania. Ndio maana serikali yetu inapambana katika kuhakikisha ya kuwa huduma hii ya umeme inapatikana na kuwa ya uhakika.

Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni kuwa tuendelee kuwa watulivu na wavumilivu.natambua maumivu yapatikanayo kutokana na mgao wa umeme.natambua kuna wengine wanapata hasara kwa kuharibikiwa na bidhaa au vitu vinavyotegemea umeme kuendelea kuwa salama .nimeona kuna watu wakitupa nyama ya mbuzi,wengine kuku,wengine samaki wabichi baada ya kuwa wameharibika.

Najuwa kwa sasa umeme ni uchumi,ni mtaji kwa vijana wengi na ni pumzi ya watanzania.ukikata umeme ni kama kuwapatia pumzi ya moto Watanzania,ni kuwatia umaskini,ni kuwapa presha wale wanaotegemea wafanye kazi ili warudishe pesa za marejesho kwenye vicoba na vikundi au taasisi mbalimbali za mikopo,ni kuwakatisha tamaa wajasiriamali.

Ni kuwabubujisha machozi wale ambao vitu vyao na bidhaa zao zinaharibika kwa kuoza. najuwa mamia ya vijana waliojiajiri wanategemea umeme kuendesha shughuli zao, kuanzia wale wa salon,gereji, fundi kuchomelea,mashine za kusaga n.k.

Kwa kutambua hayo ndio maana serikali yetu inafanya juhudi kubwa sana kuhakikisha kuwa umeme unapatikana kwa uhakika na muda wote. ndio maana serikali inaongeza vyanzo vya nishati badala ya kutegemea vilevile vya miaka yote angali idadi ya watu na shughuli za uchumi zinaongezeka na kukua kwa kasi kubwa sana inayoongeza mahitaji ya huduma ya umeme..

Poleni sana watanzania wenzangu , lakini tuendelee kuwa wavumilivu,watulivu,wenye subira na imani na serikali yetu Sikivu chini ya uongozi shupavu, imara,thabiti na madhubuti wa mzalendo wa kweli na mama mwenye upendo na huruma kwa watanzania jemedari wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Screenshot_20240220_210325_Instagram.jpg
 
Mgao wa milele 😂😂😂

Nimegundua kumbe matatizo ya watanzania ni ya KUTENGENEZWA, sio Matatizo HALISI.

Ahsante Lucas Msambwanda.
Mahitaji ya umeme yameongezeka kwa kasi kubwa sana huku vyanzo vya umeme vikibaki kuwa vilevile, ndio maana serikali inafanya juhudi na jitihada kuongeza vyanzo vingine vya umeme kama hiki cha joto ardhi.
 
Mahitaji ya umeme yameongezeka kwa kasi kubwa sana huku vyanzo vya umeme vikibaki kuwa vilevile, ndio maana serikali inafanya juhudi na jitihada kuongeza vyanzo vingine vya umeme kama hiki cha joto ardhi.
Ndio maana halisi ya serikali iliyojaa mazuzu wasio ona mbali.

Wakati nchi nyingi zina short term plans na longterm plans (miaka 5, 10, 50 mpaka 100) sisi tuna vote robbery short and longterm plans, pia concrete false propaganda plans.

Na bila kuwanyoa bila maji hawa ccm hatuchomoki humo.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mahitaji ya umeme yameongezeka kwa kasi kubwa sana huku vyanzo vya umeme vikibaki kuwa vilevile, ndio maana serikali inafanya juhudi na jitihada kuongeza vyanzo vingine vya umeme kama hiki cha joto ardhi.
Huu upuuzi waambie watoto wa chekechea. Hivi ni Tanzania tu hapa duniani ndiyo matumizi ya umeme yameongezeka? Hivi unajua mahitaji ya umeme Tanzania ni kiasi gani na vyanzo tulivyo navyo vinaweza kutengeneza umeme kiasi gani? Lucas unataka kujiweka kwenye nafasi ya msemaji wa serikali tena kila kwenye sekta wakati huna taarifa sahihi juu ya masuala yanayolalamikwa. No research no right to open your stinking mouth,just shut up !!
 
Ndugu zangu watanzania ,

Hiyo ni taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu akiwa mkoani Mbeya ,kuwa serikali haiwezi kusema ni lini mgao wa umeme utakwisha bali inachofanya serikali yetu...
Bwaaaaa bwaaaaa 😂😂, nimecheka kwa nguvu kinoma, majizi ya kura Sasa yameishiwa uongo. Hapa nilipo ni kama nakuona Lucas. Kitu ccm wanaweza kwa usahihi nchi hii ni kupora uchaguzi, na kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Back
Top Bottom