Shida ya Umeme, Maji, huduma za afya, Elimu na nyingine sio Serikali au Taasisi inayosimamia, shida ni sisi Walaji (Wananchi)

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
221
528
Shirika kama TANESCO na mashirika ya maji kila mkoa (Mfn. DAWASA, MOROWASA, nk) wananchi tunalipa "bills" ili kupata huduma na ikitokea usipolipa kwa wakati watendaji wa haya mashirika hawachelewi kukusitishia huduma na wakati mwingine kukulipisha faini.

Tuchukulie mfano TANESCO na MOROWASA au DUWASA wanakudai deni lao, wangapi wamekumbana na ukali wa maneno kutoka kwa watendaji wa hizi taasisi?

Sasa tuje kwetu wananchi, tunapokosa huduma ambayo kimsingi wao ndio wanatakiwa kuitoa tunawafanya nini??

Ni mkoa gani au wilaya au mtaa wanañchi wake waliwahi kuandamana kwa pamoja kwenda kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji kudai haki yao ya kutopata maji pale wanaponyimwa huduma hiyo??

Kama wananchi hatuchukui hatua yoyote, unadhani ni mkurugenzi yupi atajali?

Ni wananchi wangapi ambao wanashindwa kufanya biashara kwasababu ya umeme kukatika? Wangapi samaki, nyama na bidhaa nyingine zimeharibika kwasababu ya uzembe wa TANESCO?

Lakini kati ya hao ni wangapi wameandamana kwenda makao makuu ya TANESCO au kufungua kesi mahakamani kudai fidia??

Wanafunzi shule nyingi za serikali wanakalia vibao vya madawati mabovu, hakuna madawati ya kutosha, Walimu shule nyingi hawana ofisi wala faniture za ofisi. Wazazi hili wanalijua pamoja na Tanzania kuwa na misitu mingi lakini shule hazina madawati

Ni wazazi wa mkoa upi waliwahi kuandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa halmashauri husika kudai madawati kwa watoto wao??

Ikiwa hakuna malalamiko rasmi mnafikiri nani atajihangaisha kutatua haya matatizo??

Huu upole wa kutodai haki zetu ndio kikwazo cha watendaji wa serikali kuwajibika.

Rais hata awe mkali kiasi gani peke yake hawezi bila back up ya wananchi. Kwanza yeye mwenyewe anatakiwa "awaogope" wananchi

Raia tukijua kusimamia na kudai haki zetu hakuna mtendaji atatoa majibu ya hovyo kwa wananchi. Hakuna mtendaji atakuwa mzembe maana anajua atakachokutana nacho

Hii hali ya kuridhika na kukubali kila tunachoambiwa na hawa watendaji wa serikali ndio msingi wa ukomavu wa matatizo yetu

Ni jambo la kawaida kabisa mwananchi kujibiwa hovyo na muhudumu wa ofisi hata yule wa masijala tu kwasababu anajua hauna cha kumfanya.

Laiti wananchi tungekuwa tunajitambua, tunajua kudai haki zetu, hakuna nesi angemjibu vibaya mgonjwa, hakuna nesi au daktari angeleta uzembe wakati wa kutoa huduma, hakuna meneja wa TANESCO au shirika la maji angeleta uzembe kama huu

Nasema hivi, sisi wananchi ndio tatizo hivyo tutulie tunapokumbana na hizi shida za nchi hii
 
Back
Top Bottom