Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Black mamba 'koboko' mnamtukuza sana ila kiuhalisia ni nyoka wa kawaida na ni chakula maalumu cha mfalme wa majoka King Cobra.

Ukimpata King Cobra na kumtupia humo msituni kwako, ni kitendo cha dakika 30 tu utaona Koboko wako anavyotupiwa mdomoni kama vile mtu anavyotupia tambi za futari mdomoni.
Unataka atatue tatizo kwa kuongeza ukubwa wa tatizo 🤣🤣🤣..

Hizi akili ndo walizifanya wazungu kwenye Scheme za groundnuts Tanzania..
Ili kuondoa Panya kwenye Karanga wakaIntroduce Nyoka wa kila aina..
Baadaye tatizo likawa kubwa
 
Jf salaam🙏

Ni muda Sasa Tangu aanze kuonekana huyu nyoka hatari koboko na inasemekana wapo wawili.

Taarifa zilianza kunifikia kutoka Kwa wazee wangu maana huo msitu ukweli sio wangu ni wa mzee ila kaniruhusu kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.

Mara kadhaa amekuwa akionekana na muda wa usiku kupiga kelele flani Hivi.

Nakumbuka baada ya kupata mapumziko mafupi nilienda kijijni Kwa wazee wetu. Nikafika na nikaenda mlimani(msituni) lengo nikufanya research Kwa kina Ili niwekeze ufugaji wa nyuki (asali).

Nilimchukua dogo mmoja Ambae Huwa anachunga mbuzi wangu tukaenda nae huku akinifotoa picha za Kila aina na Kila Rangi.

Mwisho tukafika kwenye mti mzuri wenye kijani kibichi wenye matawi mazuri akanipigia picha za kutosha pale.

Baada ya hapo tukakaa chini ya mti huo kwenye jiwe huku nikipitia picha nilizopigwa na kufuta zile sikuzipenda

Tukiwa hapo tunapiga story ghafla tukasikia kelele za ndenge flani juu ya mti Mimi kelele zile nazijua Huwa ni Alert ya hatari flani wameiona wale ndege.

Kuinua macho juu sikuamini nilichokiona ni yeye koboko mtesa ametulia tulii Wala hatikisikii kama amekufa.

Dogo(muha) kumuona akapanic akaanza mbio nikamwambia simama hapohapo akasimama huku Nami nikitoka eneo la tukio Hadi Kwa dogo.


Nyoka ni mkubwa na anaogopesha na Kwa mazingira Yale huwezi mshambulia Kwa kutumia njia zetu hizi za asili(fimbo)

Maana ni mstuni vinginevyo anakuua ndani ya muda mfupi tu hakuna sehemu ya ku escape asikudhuru.

KUMBUKUMBU ZANGU

Miaka ya nyuma tukiwa wadogo nilishuhudia maiti za Watoto wenzetu wa2 na ng'ombe 7 zikiwa zimelala Chali (kufa)

Ni baada ya Hawa Watoto kuona huyo nyoka aina ya koboko na kumshambulia ndipo alipowageuka na kuwauma wote wawili na ng'ombe zao zote Saba na zilikufa hapohapo!


Nakumbuka kipindi hicho hicho nikiwa primary mtoto mwingine darasa letu Moja akiwa anaenda kuokota maembe kwenye mti wa mwembe akamuona koboko Kasimama wima naye pasina kujua alianza kumshambulia.

Hapo hapo alimgonga na kufa mama yake alisikia kelele za mwanae akilia Kwa uchungu Kwa sababu ilikuwa mbali na mwembe na mara zote walikuwa wanaenda Watoto kadhaa kuokota maembe pale. ile anatoka akamsaidie alimkuta tiyari kashafariki na nyoka amepanda juu ya mtu flani mfupi.

Ndipo alipo piga yowe kuomba msaada na walifanikiwa kumuua.


Inavyosemekana na Mimi naweza kuwa shahidi wa hili ni kwamba....

Nyoka aina ya black mamba ni wapole kupita kiasi pale anapokuwa katika Hali yake ya kawaida.

Pia anasikia kuliko kawaida anaupeo mkubwa wa kuhisi hatari na hata harufu na hivyo kujiweka tiyari Kwa ajiri ya mapambano.

Akiona mazingira aliyopo sio salama kwakwe kufanya shambulio hujiondokea kabla hujamfikia Wala kumuona.

Lakini pale ukimuona wewe jua kakusubiri na amejiandaa Kwa muda mrefu sana amegojea tu ulianzishe upate unachostahili.


Kwa matukio hayo mawili ambayo siyo ya kusimuliwa na hili langu Mimi mwenyew Tena mwezi 2 tu mwka huu nakubaliana na hili kuwa Hawa nyoka ni wapole na ni hatari.

Tukio la wale watoto wawili na ng'ombe wao. Sisi ndo tulikuwa wa kwanza kumuona yule nyoka na ilikuwa Hivi.....

Siku Moja tunaenda machungani katikati ya njia kulikuwa na mti flan Hivi kama kichaka (ipo miti Ina randa na kutengeneza kichaka kizito)

Tulipitisha mifugo yetu yote salama na sisi wenyewe tukapita salama mtu wa4 ndo akatumbia oneni yule nyoka tukarudi kumtazama asee alikuwa mrefu sana na ametulia kama hajui kinachoendelea...

Tulichokifanya ni kwenda kuwambia wakubwa wetu karibu na eneo lenyewe. Na walipokuja wakamuona na kumtambua walitumbia ondoeni ng'ombe na mifugo yenu hapa tukafanya hivo.

Nao walipoona tumeondoka waliondoka pia bila kumfanya chochote.

Bahati mbaya sana Kwa wenzetu siku chache mbele wao walipo muona tu ujasiri uliwaingia na kuanza kumshambulia huo ndo ulikuwa mwisho wao na ng'ombe wao pia.

Yowe lilipigwa nyoka huyo akauliwa.

Nimekuja kuomba ama kufundishwa njia/mtego Ili nimuue bila kuathiri watu wa maeneo hayo.


Msitu huu nimepanga kufugia nyuki Kwa wingi lakni kinacho niogopesha ni uwepo wa black mamba kwenye eneo hili.

Eneo ni zuri sana Kwa nyuki kwani maji yapo si zaidi ya mita250 na nyuki ni wengi sana hasa kwenye mapango ya miti,mawe na wengine hujitengenezea asali juu ya mti tu.


Najua humu Kuna watu wa maliasili na wataalamu wa maswala haya naombeni namna ya kumuondoa huyu mdudu na nimeambiwa wapo wawili.

Wapo walio waona Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti na usiku hupiga kelele zao Kwa kupokezana wasi wasi wangu zaidi watazaliana na kuongezeka zaidi.

Ahsanteen sana
Peleka paka au nyani ndani ya huo msitu.
Na hayuko peke yake,lazima kuna mwenzie ama wenzie.
 
wewe utakua tabora vijijini uko igombe igombe flani back to the point fuga bundi koboko ndio chakula akipendacho
na ukifuga bundi jiandae kuchomwa moto na wanakijiji kwa tuhuma za uchawi
chagua kuuawa na koboko au wananzengo
😂 😂 😂 eneweyi mkuu bundi ndo chakula chake lakini kwa sasa wamepungua kwa kiasi kikubwa sana enzi hizo tukiwa wadogo bundi walikuwa wengi sana na tuliwachukia sana kwa mlio wao kumbe hatukujua
 
wewe utakua tabora vijijini uko igombe igombe flani back to the point fuga bundi koboko ndio chakula akipendacho
na ukifuga bundi jiandae kuchomwa moto na wanakijiji kwa tuhuma za uchawi
chagua kuuawa na koboko au wananzengo
Ndiyo nimesikia bundi anamkamata na kwenda nae juu sana na kumuachia na kumfuata tena hadi anakufa?.
 
Back
Top Bottom