Kwenye biashara usiogope majina makubwa yaliyokutangulia; Hill water, mabasi ya Tilisho ni somo kubwa la kuingia sokoni ukiwa mpya

Wafalme wa kaskazini kwa mabasi
1. ni Kilimanjaro
2. Bm
Hawa wana ligi yao ya kipekee
Huyo tilisho, ester, Abood, extra luxury,marangu, dar express, kidia, mapenzi ya Mungu, na wao wana ligi yao.
Kwa upande wa maji kwa kaskazini maji kuaminika bado ni Kilimanjaro
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wateja wanapenda kuonja ladha tofauti
sasa kazi kwetu kuwafanya wateja waje kwetu kila siku hapa ndo zinapohitajika kufanyia innivation bidhaa zetu day by day


zile pisi za tilisho acha kabisa
 
Kilicho muumiza mengi alijisahau wenzake wakatumia mwanya huo lakini maji ya Kilimanjaro mpaka sasa bado ni bora zaidi pamoja na maji ya afya maji mengi yana chumvi akijipanga akashusha bei mbona bado jina analo tu mtu akikaa sokoni kwa muda mrefu kumshusha iko kazi labda afanye uzembe
Mengi ni kifo chake hawa madogo ndio chenga ,ila Mengi angekuwa level nyingine.

Maana enzi zake yale ya Kilimanjaro tulikuwa tunaita " Maji ya seminar"🤣
 
Watu wengi tunaogopa kuanzisha biashara fulani kwa kuogopa kwamba ma giant wameshajaa hivyo hatutapata wateja.

Soko la maji ya kunywa lilikuwa limetawaliwa na kilimanjaro, kila sherehe ya harusi utakayoenda maji unakuta Kilimanjaro. Kila hotel kubwa ama bar kubwa maji unakuta kilimanjaro, leo hii kilimanjaro kakimbizwa sokoni.

Mitaani pia maji yalikuwa uhai, baadae akaja afya, ila hill water kaja mpya tu ila kawakimbiza sokoni.

Kwenye biashara ya ma bus. Nani aliwaza njia ya Moshi Arusha kuna bus zitakuja wazidi ma giant wa njia hiyo kwa miaka zaidi ya 20 yaani kilimanjaro express ama Dar express kwa wateja. TILISHO na yeye hakuogopa.. kaja sokoni mpya kwa mbinu ya wahudumu mabinti wapenda social media.. mwisho wa siku kaiteka njia bus zake kila siku zinajaa.

Hilo ndilo somo kubwa la biashara.

Usiogope waliokutangulia.
Bila kusahau halotel
 
Bora umewataja kilimanjaro,kuna sehemu nimeenda kikazi asee hakuna maji zaidi ya kilimanjaro na ndo hivo yana chumvi siku hizi
 
Mimi mwenyewe nilikua namwogopa Simukitaa,zahor matelephone na wengine wengi mjini hapa lakin hii kidogo imenifumbua 🥱
 
Back
Top Bottom