Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Without hesitation or equivocation, I wholeheartedly support your call.
i beg to differ,if JFTanzania is turned off it is us who will suffer and the tyranny will have realised their goals.I suggest appeal to be made to western media to expose this injustice.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
Sishauri hii JF Tz izimwe.mtakuwa mmewapa ushindi hawa tyranny rule na kutunyima sisi members jukwaa huru la kutoa mawazo yetu.zitumike njia zilezile za appealing to western media to pressurise this injustice to our Forum.
 
Kuna haja ya kuelimisha watumiaji wa JF namna ya matumizi sahihi ya mitandao. Uhuru wa kuhabarishana haubarikiwi kwa kuvunja sheria nyingine! Tujifunze kufanya mambo kwa kiasi na kwa utaratibu!

Hata huko kwa walioianzisha hii mitandao, bado kuna sehemu serikali inaingia pale panapotokea uvunjifu wa sheria!

If you tweet jokes about killing Trump, the Secret Service will find you.

Kejeli, uzushi, matusi sidhani kama lilikua lengo la awali forum ilipoanzishwa. Siku za karibuni kumetokea mabadiliko makubwa yanayopelekea umuhimu wa kuwepo kwa regulations Kali! Moderators wajitahidi kudeal na members wanaopelekea mambo kama haya kutokea!
 
Msaada wa Kijitoa jf nimejaribu sijaona options... Waswahili husema Kubali yaishe...
 
Hivi wanaogopa nini kwenye mitazamo ya wengi wa wana JF?

Uwoga uliokithiri usio na sababu ni dalili kubwa ya ugonjwa wa akili
 
i beg to differ,if JFTanzania is turned off it is us who will suffer and the tyranny will have realised their goals.I suggest appeal to be made to western media to expose this injustice.
You are right. We are the one who are going to suffer. Those who does not want freedom of expression will be the winner.
 
That's what I'm talking about! Kuna washauri wanamuingiza shimoni Rais wetu ....
Ha haaaa msiwasingizie washauri, huyu mtu amejipambanua kuwa hapendi kukosolewa na ndio maana alitaka Malaika wazime hii mitandao kwa miaka minne. Pia huyu huyu ameonyesha kukerwa na kukosolewa kiasi cha kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kuwapa vyeo wale wanaomsifu na kumuabudu. Tusilaumu watu ukweli uko wazi
 
mmmh jamani mbona kama sielewi? ina maana max amekamatwa au nn?
 
Watutumia nguvu kubwa kudhibiti watu ila wakishindwa ku-deliver yote haya ni bure kabisa na 2020 watakataliwa kwa nguvu zote.

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati uchumi mbovu ni kazi bure.

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati hakuna ajira ni kazi bure.

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati wanafunzi wanakosa mikopo ni kazi bure.

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati biashara za watu zinakufa ni kazi bure

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati umezuia mikutano ya kisiasa ni kazi bure

Ukiminya uhuru wa watu kujieleza wakati watumishi hujawaongezea mishahara na kuwalipa malimbikizo yao ni kazi bure

Orodha ni ndefu ila mwenye masikio na asikie.
Wakati private companies zinafirisika maana hawalipwi in time na serikali na bajeti ijayo serikali imewatupia virago....
 
Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.
mwanakijiji leo anaisoma namba,bila shaka asingeunga mkono mashudu ya lumumba leo tusingekuwa tunajadili haya na ndugu yetu angelindwa na sauti ya umoja wetu
 
kwanini msifunge tu office mkaziweke pale new York tuchukue kama youtube au instagram na jina libaki lile lile maana ishakuwa kero
 
hii sheria yetu ya cyber crime ata mataifa ya nje waliiona ni tatizo! tukumbuke miongoni mwa sababu za kutopewa pesa za MCC.
 
Sijaelewa ni kwa faida gani nchi ina pata kuwakamata nakuwazuia watu
 
Back
Top Bottom