Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Pole Max!
Hivi kwenye facebook inakuaje iwapo watanzania wamejisajili kwa majina tofauti na kutoa maoni yasiyotakiwa na serekali kama ilivyo kwa jf Nani atakamatwa hapo?
Nadhani ingefaa kuwaenzi wabunifu wetu ili wafike Kimataifa kama ilivyo facebook no.
 
Hakuna haja ya kumkosesha binadamu mwenzako kwa vitu vidogovidogo hasa pale unapojitolea kumsaidia kimawazo na kimkakati.

Kuna wakati rais Magufuli alifika kwenye hatua ya kutamani malaika aje aifunge mitandao ya kijamii (Mlengwa mkubwa akiwa Jamii forum) Ya nini yote hayo? Mitandao ya kijamii ina miiba? Inatembelewa na wangapi? Kisa tunakosoa? (Maana alisema kuwa anatamani ili maendeleo yaje chapchap! Labda huenda tunazuia maendeleo pale tunapokosoa.

Sasa mimi nasema hivi. Aliwahi kusema mwalimu kuwa rais wa nchi anaweza akaamua chochote kwa mujibu wa yeye anavyoona! Naamini kuwa ana uwezo mkubwa tu wa kuamuru Jamii forum-Tanzania ufungwe na ikafungwa! Afanye hivyo.

Sisi wengine kuanzia leo tunajivua rasmi kuikosoa serikali humu jamvini! Tutakuwa tu wasomaji na wachangiaji kwenye majukwaa mengine! Ninaamini kuwa Maxence kukamatwa huku kukiwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ukamatwaji (Kwani bado kesi iko mahakama kuu) hakujatokea hivihivi!

Kumfanya rais mpaka ajiapize kutamani malaika ashuke wala hakuna maana! Bora nikae pembeni...

Kwa masikitiko makubwa naomba kuwaambia wenzangu tuliokuwa tukishirikiana katika mijadala mbalimbali kuwa "Sitaweza kuendelea tena katika hali ya namna hii" Hadi hapo kutakapokuwa na mabadiliko na natamani iwe hivyo ila Sidhani kama itatokea karibuni....

Kwa tunaodhani kuwa wanaotafutwa ni wale wanaotukana basi tujikumbushe kauli hii "Natamani sana malaika washuke waifunge mitandao ya kijamii kisha ije kufunguliwa tukishapata maendeleo" hapo ataelewa kuwa rais wetu hapendi kabisa WAKOSOAJI!

Nasikitika sana sana!!!!
Kumbe mitandao ya kijamii inazuia maendeleo?
Lkn inazuia maendeleo Tz tu au dunia nzima?

Na hayo maendeleo yakishakuja atatumia mitandao hii ya kijamii kuwaelezea watu au itatumika mitandao yao ya kidunia/taifa/kiulimwengu kutangaza angalieni maendeleo tuliyoyapata?

Unaweza ukajificha gizani ukifanya yako ili uibuke baadae uonekane ulikuwa unafanya kitu cha maana lkn badala yake ukaibuka ukakuta watu wanakucheka kwa kituko ulichofanya(outdated)
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
Naungana na Wewe Max aachiwe Mara Moja Jamii Forums sio entity ya .co.tz kwa hiyo sioni ni sawa kwa Serikali ya Tanzania Kuishinikiza kuwapa majina au Taarifa za Members. Je Tanzania wanaweza Kuwashinikiza Facesbook, au Google au youtube au Instagram kuwapa majina au taarifa za members wao? kwanini iwe kwa JF, kwa kuwa Tuu Jamii furums inatumia Kiswahili? Au kuna Usajili wowote wa Jamii Forums katika Taasisi za Tanzania?
 
Mimi sijui ni Amri ya nani Lakini Namjua mwenyekiti wa chama ambacho juzi Kilitoa Tathmini Kuwa Ukawa wamefanikiwa Kutumia Mitandao ya Jamii vilivyo na wakasema hasa Jamii Forums. Pili Namjua Rais wa Nchi Moja aliyesema anatamani Malaika washuke wafungie mitandao ya jamii. Rais huyu sii Mwingine ni Mh. Magufuli, Na nafikiri baada ya kurubiri Malaika akachoka akaamua kuwaagiza "Malaika wake" waende kumkamata Max ili kutisha au pengine Kumhonga! Si walihonga wabunge wote Kwa bilioni 27 ambazo Magufuli aliziiba serikalini? Ili kuwashawishi Kupitisha sheria ya Habari ya Kikoloni! Je nini Kitamzuia kuiba milioni kadhaa serikalini na kuhonga Vijana Wazalendo Kama hawa?
 
hii sheria yetu ya cyber crime ata mataifa ya nje waliiona ni tatizo! tukumbuke miongoni mwa sababu za kutopewa pesa za MCC.
Mtu anajidai kurukaruka tu.

Hawa wazungu wakituamulia kuminya point hatuendi mahali, acha afunge mitandao ya kijamii ili apate maendeleo
 
Mimi Kama wanataka Jina Langu waniulize hapa Live Nitawapa hapa hapa, Hawana haja ya Kumtesa Kijana wa Watu, The Lord is my Shield who shall I fear? Makonda au Magufuli? Hao ni watu au Miungu? Msidanganyike hawa Watawala waheshimuni wakistahili heshima lakini Ukweli ni Kuwa they are Nothing but mortals!
 
MM kwanza nikuunge mkono kwenye maoni yako , lakini pili naomba niweke wazi kua Hali inavoonekana Ni mbaya kuliko tunavyofikiria na hii itaigharimu sana serikali.
 
Tuache unafiki

Humu jamiiforums udikteta kwenda mbele watu wanapigwa ban bila kujulishwa ssababu moderators wamekuwa miungu watu wana moderate kutokana na moods zao

Sasa Leo kibao kimegeuka mnalalamika?

Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Au why hakuna namna ya members kujitoa au kujifuta uanachama?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??



We complain about govt repression huku ndani tunarepress members

PT niaje bro....you good man?
 
MM weweumeshiriki sana kumjenga Sizonje,mlitukejeli tuliokuwa tutunamfamu kabla.Mkuu umekuwa nguvu k kujengahoja.kumtetea Sizonje,ona sasa !Huyu mtu Siye!Mlibugi step.

Mbona unajaribu kunifanya nione nilifanya makosa kumpinga Lowassa. Mbona hilo sijalijutia. Bado naamini mabadiliko yanayoendelea ni muhimu kutetewa. Suala la mitandao ya jamii na hatari iliyokuwepo nilishaonya mimi miaka kadhaa nyuma so katika hili kwangu hakuna kinaschonistua. Serikali zote duniani zinafanana linapokuja suala la kujiimarisha madarakani.
 
Bado naamini mabadiliko yanayoendelea ni muhimu kutetewa.

Mzee...hivi ni mabadiliko gani hayo unayosema ni ya muhimu kutetewa?

Kufuta sherehe za uhuru 2015 na kugeuka na kuja kuwa nazo 2016?

Magu is turning out to be worse than I thought he would be!
 
Do unto others as you would have them do unto you; scrap this appalling media law

By Jenerali Ulimwengu
THE EAST AFRICAN

posted Wednesday, November 30 2016 at 13:28

An object lesson in how to do unto your opponents was delivered many years ago in one Central African country that was ruled over by a particularly obnoxious dictator.

The president had been in power for close to 20 years when an old school friend came to him to ask for a favour.

The friend, a prominent architect, came to complain to the president that all the time the latter had been in office, he had not given a single one of those lucrative government contracts to him. The president listened to his old friend, and an idea formed in his mind.

So the dictator gave orders for his friend to be awarded a contract to build a maximum security jail for political prisoners, but he gave special instructions. The prison was to be built with unshuttered windows and vents that allowed for cold draughts to come into the prisoners’ rooms. The vents were to be so built that they led directly to where the beds would be placed.

The idea was that during the colder months of the year, the draughts would work on the political prisoners, causing them to contract pneumonia, and their deaths would be deemed natural. The architect got a fat cheque from his old friend and built a prison so full of holes the wind that came through it could have sailed a boat.

However, just after the president inaugurated the prison amid much fanfare, with praises for his friend’s innovative architectural innovations, the army staged a coup, overthrew the president and sent him to become one of the first inmates of the brand-new jailhouse. Three months later, he died of… pneumonia.

Elsewhere, in the Mediterranean area, a prime minister went to visit institutions in the capital and to listen to the views of those who lived there. In a high school, the students complained of poor meals, lack of books and dilapidated sporting facilities. He told his assistant to remind him in a month’s time.

But when the PM went to a prison and the inmates complained of the same things as the students, he told the assistant to deal with those issues “tomorrow morning.” As they were leaving, the assistant ran up to the boss to express his surprise at the contradictory instructions, and to ask why the chief was favouring convicts over students. The answer he got was simple: “Stupid; at my age, do you see me going to high school in the future?”

Sure enough, six months later, the prime minister was overthrown and put in jail. He survived to come out and become prime minister again, after two years in a rather comfortable guest house. Now, between the two politicians, who was smarter?

The politician in the first story is the more typical kind in our countries. Those who find themselves in power, by means foul or fair, think they can do anything they like without at some stage suffering the consequences of their acts. From time to time, some of them get a taste of their own medicine, but for some reason, the lessons they learn are seldom passed onto others.
 
Kuinga ccm haina maana kwamba huwez kuikosoa,kuikosoa ni ni tools and firm pilar yakuifanya ijirekebishe,ila kwakuwa ina sikio la kufa mpaka damu maskion,imekaribia kuipata fresh ya unga kama vijana wa mjin wanavyosema
 
Mbona unajaribu kunifanya nione nilifanya makosa kumpinga Lowassa. Mbona hilo sijalijutia. Bado naamini mabadiliko yanayoendelea ni muhimu kutetewa. Suala la mitandao ya jamii na hatari iliyokuwepo nilishaonya mimi miaka kadhaa nyuma so katika hili kwangu hakuna kinaschonistua. Serikali zote duniani zinafanana linapokuja suala la kujiimarisha madarakani.
Umesema mabadiliko yanayo endelea ni muhimu, kwahiyo unaunga mkono kukamatwa kwa max manake nayo ni mabadiliko. Usilalamike bac, acha wengine ndo walakamike.
 
Back
Top Bottom