Jamani mimi ni kijana mwenye miaka 28 baada ya kumaliza masomo nimepata kazi hapa mjini, sasa nikaamua kutafuta mke ili nioe niache kumbwela mbwela nisije kufa kwa ngoma, nimepata mtoto wa kihehe wa kule mafinga tayari nimempeleka kwetu(Tarime) na amekubalika kwa wazazi wangu, kimbembe kimekuja baada ya kwenda kwao wazazi wake wamekataa wamesema mtoto wao hawezi kuolewa na mkurya kwani eti si watu wazuri wanapiga wanawake na ni wakorofi, nifanyeje kwa sababu nampenda sana huyu binti.