Father and Daughter( Hadithi ya Kiswahili)

Aug 25, 2022
9
14
eva.png


Mwandishi wa kitabu: Peter Charlz
Mchoraji: Peter Charlz
Instagram / Twitter / Facebook: petercharlz255
Email: petercharlz255@gmail.com


Shukrani za dhati kwa kila alieshiriki kuandaa kitabu hiki.
Mhakiki : Augustino Peter
Instagram : babadenze
BOBOtheBEST Studios
Instagram:
bobothebeststudios & bobothebestcomics
Facebook:
bobothebestproduction
Email: bobothebestproduction@gmail.com

LUGHA
Lugha iliyotumika ni kiswahili ambacho kinatumika katika mazingira yetu ya kilasiku. Hatujatumia ufasaha wa lugha ya kiswahili lakini tumeangalia mazungumzo ya kawaida yanayofanyika mitaani, kwenye familia n.k. Baadhi ya misamiati imetumika lugha ya kingereza ili kuweka uhalisia wa mazungumzo ya kilasiku katika jamii zetu, hasa katika hiki kizazi kipya.


1664197848385.png
BOBOtheBEST Studios
Presents


Episode 01

BABA BORA

1664197848599.png

Karibu jiji la Dar-es-salaam katika nyumba moja ya kifahari ya tajiri mmoja mwanamitindo Bwana Moses (Mr Moses). Mr Moses amekuwa tajiri mkubwa kutokana na kampuni yake ya mavazi inayoitwa Proud (Fahari) inayofanya kazi zake nchini na nchi jirani. Amejipatia umaarufu mkubwa nchi nzima kutokana na bidhaa zake nzuri na zenye ubora wa hali ya juu. Na leo katika nyumba yake ametembelewa na wandishi wa habari ambao wamekuja kufanya mahojiano na binti yake Mr Moses ambae hivi karibuni anatarajia kuzindua toleo jipya la nguo. Binti huyu anaitwa Eva Moses, mtoto wa tajiri mkubwa mwanamitindo Mr Moses…

Mtangazaji (ke): Wewe ni binti mdogo sana umesema una-umri wa miaka 17 tu, unawezaje ku-design (kubuni) mavazi mazuri hivi kama mtu ambae umri wake ni mkubwa?
Eva (binti): Woow!! Labda kitu ambacho watu wengi hawajui kuwa, hii ni talent kutoka kwa wazazi wangu. Wazazi wangu wote wawili ni wanamitindo na pia wanaendesha kampuni kubwa za mavazi. So, naweza sema hii nimezaliwa nayo lakini kwa kuongezea tu, hii kitu ndio nayosomea yaani nasomea maswala ya mavazi.
Mtangazaji (ke): Unasomea ubunifu wa mavazi?
Eva: Yeah!! Nasomea fashion kama modeling, designer, marketing n.k. katika maswala ya mavazi.
Mtangazaji (ke): Oooh!! Hongera sana!
Eva: Asante!! Asante sana.
Mtangazaji (ke): Ok! Swali ambalo napenda kumalizia nataka kujua au mtazamaji anayetaka kujua, Eva anapenda nini kuliko kitu chochote katika maisha yake?
Eva: Kitu nachokipenda kuliko chochote!?
Mtangazaji (ke): Ndio.
Eva: Wooow!! Kitu amabacho napenda kuliko kitu chochote katika maisha yangu ni baba yangu. Baba yangu Mr Moses nampenda sana, sana yani siwezi hata kuelezea ila kwangu yeye ndio namba moja.

Wakati mahojiano yanaendelea Mr Moses alikua pembeni kidogo akimuangalia binti yake akifanya mahojiano, mwandishi mmoja alimfata Mr Moses.

Mwandishi (me): Hongera Mr Moses kwa mambo makubwa unayoyafanya.
Mr Moses (baba): Asante sana!!, Asante kwa mchango wenu pia.
Mwandishi (me): Vipi muingize binti yako sasa katika kampuni yako, maana anafanya mambo makubwa pia.
Mr Moses : Yeah!! ni Kweli, lakini nataka kwanza amalize kusoma na umri uende kidogo yaani walau akiwa hata na miaka 19 au 20 hivi.
Mwandishi (me): Ooohh! Kweli akili ikue pia.

Wakati wakiendelea na mazungumzo Eva alikua amemaliza kufanya interview (mahojiano), anaenda alipo baba yake.

Mwandishi (me): Oohoo!! naona wamemaliza, ok sawa Mr Moses tutaonana siku nyingine.
Mr Moses : Sawa asante sana aisee, karibuni tena. (wakaagana)
Eva: Baba…!! (kwa furaha)
Mr Moses : Eva binti yangu, hongera kwa bonge la interview. Umefanya interview ya dunia.
Eva: ha ha ha ha ha..! Acha utani baba.

Basi siku hiyo ilikua siku ya furaha kwa familia hiyo ambayo ina-jumla ya watu 27 na 25 kati yao ni wafanyakazi ukimtoa Mr Moses na Eva. Siku iliyofuata asubuhi na mapema Mr Moses anaamka anaingia bafuni anapiga mswaki kisha anoga na ananza kujiandaa, inaonekana kunasehemu anataka kwenda. Baada ya muda anamaliza kujiandaa anatoka chumbani kwake.

Mr Moses : Heloo!! Eva, Eva umejiandaa tuondoke?
Eva: Ndio baba, Madam Sarrah anamalizia kuniandaa hapa.
(Madam Sarrah/Bi Sarrah ni kijakazi wa Eva)
Mr Moses : Ooohhoo!! Nimegundua kitu, naona unataka upendeze mpaka umshinde mwenye sherehe.
Bi Sarrah: Nimemvalisha nguo hiyo kwasababu ni rangi anayoipenda sana mama yake.
Mr Moses : Yeah!! Mama yake akiona atafurahi, atafurahi hasa akiona amevaa mtoto wake.
Eva: Wooow!! leo tunaenda kumuona mama, nataka nimuone mama harisi sio picha tena. Na nikimaliza muda wa likizo nitamwambia mama turudi wote huku.
Mr Moses alishtuka kidogo baada ya kusikia hivyo lakini akapotezea.
Mr. Moses: Yeah! vizuri.
: Aya sawa, sasa uko tayari twende maana tunachelewa.
: Bi Sarrah umemuwekea vizuri mizigo yake?
Bi Sarrah: Ndio tayari nimeweka vitu vyote alivyonielekeza.
Mr Moses : Eva umekumbuka kuchukua vitabu?
Eva: Ndio baba, nimekumbuka.
Mr Moses : Vizuri usiache kusoma unatakiwa ufanye vyote ulivyokuwa unafanya huku. Sawa?
Eva: Sawa baba.

Baada ya kuchukua mizigo yao Mr Moses na Eva walingia kwenye gari safari ikaanza, wakiwa ndani ya gari mazungumzo yaliendelea kati ya baba na binti.

Eva: Baba leo ni siku ya kuzaliwa mama?
Mr Moses: Hapana mwanangu..!! Sherehe tuanyoenda ni harusi.
Eva: Mmmh!! OK.

Baada ya safari ya masaa mawili (2) njiani hatimaye safari yao imefika eneo husika, eneo la sherehe. Ni katika jumba jingine kubwa la kifahari na inaonekana kuna watu wengi sana, sherehe imefana kweli kweli. Mr Moses na binti yake walipokelewa.

Mlinzi: Karibu mheshimiwa!! samahani nione Kadi zenu.
Mr Moses: Kadi hii hapa, tunatumia kadi moja ya double.
Mlinzi: Ok VVIP unapita mlango huu utakuta meza yenye jina lako.
Mr Moses: Sawa boss asante!! Eva tangulia twende mwanangu kipenzi.
Eva: Wooow!! puzuri pamependeza.
Mr Moses: Pamendeza sana kama ulivyo pendeza leo mrembo wangu.

Walifika katika meza za VVIP kisha wakakaa kwenye meza yao huku sherehe ikaendelea, Sherehe husika ilikua ni harusi kubwa ya kifahari inaendelea pale mbele, huku bwana harusi pamoja na bi harusi wakisalimiana na wageni walikwa. Ilikuwa ni siku nzuri ya furaha.

Bwana hurusi (Damian): Bado sijamuona Mr Moses?
Bi harusi (Joyce): Mimi nachohitaji kwa sasa ni kumuona mtoto wangu tu. Ni miaka mingi sasa nipo mbali nae.
Damian: Vipi hujamkumbuka mumeo ha ha ha ha !? (kejeri)
Joyce: Sipendi kuliongelea hilo hapa, ukizingatia leo ni siku gani kwetu.
Katika meza aliyokaa Mr Moses na binti yake mazungumzo yanaendelea taratibu huku wakipata vinywaji.
Eva: Oooph!! watu ni wengi nimejaribu kuangalia labda naweza kubahatisha nimuone mama lakini sijapata chochote.
Mr Moses: Usijari Eva muda ukifika utamuona.
Eva: Oooh woow!! Baba nimemuona mama!! yulee.( kwa furaha)

Eva alinuka kwenye kiti alichokuwa amekaa kisha akanza kumkimbilia mama yake lakini kabla hajamfikia mama yake alisimama ghafla!! Amepigwa butwaa baada ya kuona mama yake amemshika mkono mwanaume mwingine, Lakini…

Mr Moses: Oooh! Usiogope twende kwa mama.
Eva: Mama amemshika mkono huyo! huyo ni nani?
Mr Moses : Ndio, ndio nimekumbia leo tunakuja kwenye sherehe ya mama yako sawa, usiogope twende.
Wakasogea karibu.
Damian: Aaahhaa! Karibu Mr Moses… Naona upo na binti yako.
Mr Moses: Asante sana Mr Damian mambo vipi!?
Damian: Tuko poa kama unavyona watu wanafurahi naamini hakuna aliejutia au sio Mr Moses.
Mr Moses: Ni kweli, ni kweli kabisa Damian, sherehe ni nzuri kuanzia mazingira, chakula, muziki mpaka wahusika nyinyi wenyewe mmependeza... Mambo vip Joyce?
Joyce: Mi niko poa, karibuni sana… Woow!! Eva binti yangu hujambo, niliku-miss sana mumy.
Eva: Mama huyu nani?
Joyce: Huyu? (Kwa wasiwasi)
Eva: Ndio.
Joyce: Aaaahh mmh!!
Mr Moses: Eva huyu ni baba yako.
Eva: Baba yangu ni wewe tu.
Mr Moses: Namanisha huyu ni baba yako mlezi na mimi ni baba yako mzazi. yaani huyu ni baba yako mwingine, baba wa kambo.
Eva: Hapana haiwezekani.
Mr Moses: Kwanini, ni baba yako, anakupenda… anakupenda kama anavyokupenda mama yako... Ni baba mzuri, sawa usimuogope. (akibembeleza)
Eva: Kwaiyo likizo yote nitakuwa nakaa na mama na huyu baba mwingine.?
Mr Moses: Ndio… Huyo sasa ni baba yako kwasababu leo amefunga ndoa na mama yako.
Eva: Inamaana leo ni harusi ya mama...!! Mbona sielewi... Yaani!! namanisha wewe baba harusi yako lini? (kwa mshangao)
Mr Moses: Harusi yangu!?, haipo na wala hautakuja kuiona.
Eva: kwanini baba!! Wakati mama yeye ameolewa?
Mr Moses: kwasababu harusi yangu ilikuwa kabla ya wewe kuzaliwa.
Eva: Unamanisha harusi yako na mama?
Mr Moses: Ndio mwanangu.
Eva: Sasa mbona wewe baba haukai na mama mwingine?
Mr Moses: Sina uhitaji kwasababu.., kwasababu maishani mwangu nimepata kilakitu.
Eva: kilakitu!!? Nini, kwasababu wewe ni tajiri?
Mr Moses: Hapana, kilakitu ambae ni wewe. Wewe ndio kila kitu kwangu.
Eva alifarijika kwa maneno hayo mpaka ikampelekea akamkumbatia baba yake na kujibu.
Eva: Wewe ndio kilakitu kwangu baba, nakupenda kuliko kitu chochote na sitaki uwe na mama mwingine lakini mama ni mbaya kwanini hakukaa na wewe baba.
Mr Moses: Usiseme hivyo mimi ndio niliemkosea mama, sio yeye. (kumfariji)
Eva: Unasema kweli baba, wewe ndio ulimkosea?
Mr Moses: Ndio mwanangu, Lakini unajua nini kilitokea baada ya kumkosea?
Eva: Hapana sijui, kilitokea nini !?
Mr Moses: Nilimuomba msamaha mama yako na akanisamehe. Alinisamehe kwasababu sisi ni binadamu na sio mara zote tunafanya kilicho sahihi, kuna muda tunakosea ndio maana inatubidi tusamehe kabla haijafika kipindi ambacho na sisi tunahitaji msamaha tunapokosea. Kwahiyo wewe pia unatakiwa utusamehe mimi na mama yako tulishindwa kukaa pamoja.
Joyce: Inatosha sasa Moses, nafikiri mtoto amekuelewa na atafanya kama ulivyomuelekeza.
Mr Moses: Ok sawa!! Eva kwa muda wa likizo yote hii, utabaki kwa mama pamoja baba hapa arafu baada ya likizo nitakuijia sawa.
Eva: Usichelewe kunijia maana nitakuwa nimekukumbuka sana.(kwa utani)
Mr Moses: Usijali nitamuambia dereva anikumbushe nisije sahau (utani). Aya Eva, Joyce na Damian mi niwaache sasa, lakini nilikua na hii zawadi kwa Joyce.
Joyce: Asante Mr Moses kwa zawadi yako.

Mr Moses akam-kiss Eva kisha akaingia kwenye gari akaondoka. Eva akamuangalia mama yake pamoja baba yake wa kambo, akawambia.

Eva: Nawapenda mama na baba yangu, nitawapenda kama nilivyoambiwa niwapende na baba yangu.
Damian: (Akawaza) inaonekana anampenda, anamsikiliza na kumuamini sana baba yake.​
(kisha akamuuliza:)...
* ITAENDELEA *

Episode 02

BABA ASIE BORA

1664198012691.png

...
Damian: (Akawaza) Inaonekana anampenda, anamsikiliza na kumuamini sana baba yake.
(kisha akamuuliza)Unakumbuka baba amekuambia nini kuhusu mimi..?
Eva: Amenambia nikuamini wewe ni baba mzuri, unanipenda kama ambavyo mama ananipenda.
Damian: Usiogope mwanangu baba yako hajakudanganya, unachotakiwa ni kumsikiliza baba yako alichokuambia.

SIKU ILIYOFUATA.
Eva anaamka asubuhi mapema, anakula chakula cha asubuhi baada ya hapo anafanya kazi ndogo ndogo za nyumbani, baadae mida ya saa 7: 00 mchana anakula chakula cha mchana na kusoma vitabu baadae mida ya jioni mama yake anarudi kutoka kazini. Gari nzuri aina ya Rolls Royce inaingia katika jumba lile la kifahari anashuka mama yake Eva pamoja na baba yake wa kambo.Eva anawaona anatoka ndani anaenda kuwapokea.

Joyce: Woooow!! Mwanangu kipenzi Evaa, umeshindaje binti yangu..?
Eva: Nimeshinda salama, shikamo mama.
Joyce: Marahaba mwanangu, nilikukumbuka sana.
Eva: Nimekukumbuka pia mama... Leo nime-enjoy kushinda hapa nyumbani, ni pazuri.
Joyce: Wooow!! vizuri mtoto wangu mzuri, nafurahi kusikia mwanangu umepapenda nyumbani.
Eva: Oohh!! lakini nimeshindwa kufanya kitu kimoja...
Joyce: Kipi hicho mwanangu ?
Eva: Leo sijaongea na baba.
Joyce: Kwanini sasa..!?
Eva: Naona simu yangu kama inashida kwenye mtandao toka asubuhi.
Damian akamjibu...
Damian: Usijari Eva nitahakikisha unaongea na baba yako.
Eva: Wow!! nitafurahi sana baba.
Damian: Usijari mwanangu njoo uongee na baba yako.

Eva akaondoka pamoja na baba yake wa kambo wakaenda kukaa sehemu ya kupumzikia ambayo imejengwa vizuri kwa mfano wa nyumba ya msonge, pembeni kidogo ya kijumba hicho cha msonge kuna swiming pool kubwa lenye umbo duara. Sehemu hiyo inaupepo mzuri kutokana na miti mizuri ya aina mbalimbali iliyozunguka eneo hilo. Damian akatoa simu yake, akampigia Mr Moses kwa njia ya video (video call). Wakati huo Mr Moses alikuwa kazini simu yake ikaita.

Mr Moses: Ooh!! naona Mr Damian kanitafuta…!
Akapokea
Eva: hallooo baba..!!
Mr Moses: halloo Eva!, hujambo mwanangu.
Eva: Sijambo baba, nimekukumbuka kweli baba yangu kipenzi, sijui nitakuja lini kukuona.
Mr Moses: Nimekukumbuka pia Eva wangu, likizo ikisha tu nitakuja kukuchukua... Ila hujawasumbua kweli baba na mama?
Eva: Hapana sijawasumbua hata, nimefanya kila kitu ambacho nilikua nafanya nikiwa huko.. Ninafuraha sana, mama ananipenda na baba pia ananipenda sana.
Mr Moses: Woow! Nilikuambia utanisahau tu (utani)
Eva: Siwezi kukusahau baba yangu, iyo siku haipo.
Mr Moses: Najua hilo mtoto wangu, nilikuambia baba pamoja na mama yako wanakupenda.. Sasa unajionea mwenyewe.
Eva: Ndio baba sahivi naelewa.
Muda huo simu ya ofisini ilikua inaita, ikabidi Mr Moses amuage mtoto wake ili apokee ile simu nyingine.
Mr Moses: Aya!! Sawa Eva nitakutafuta kesho saivi napigiwa simu ofisini. Sawa byee!!
Eva: Byee!! Nakupenda sana baba.
Mr Moses: Nakupenda sana pia binti yangu.
Mr Moses akakata simu ya Eva kisha akapokea ile simu ya ofisini iliyokuwa inaita.
Mr Moses: hallo.
Mfanyakazi (mapokezi): Boss tayari waandishi wamefika eneo husika, wanakusbiri wewe tu.
Mr Moses: Sawa nakuja sasa hivi.
Upande wa Eva akiwa na baba yake wa kambo Mr Damian.
Damian:
Umefurahi sana kuongea na baba yako?
Eva: Ndio nimefurahi sana, nampenda sana baba yangu.
Damian: Mmhh!! kati ya baba na mama yako unampenda nani zaidi?
Eva: Nampenda zaidi baba.
Damian: Mmh!! kwanini baba na sio mama?
Eva: Kwasababu yeye amekaa na mimi siku zote, ila mama yeye aliniacha akaja huku. (kwa kujiamini)
Damian: Ooohh!!Mungu msamehe binti huyu, anahukumu bila kujua chochote.(kwa sauti ya chini)
Eva: Kwanini Mungu anisamehe?
Damian: Nasikitika hujui nini sababu ya mama yako kuja huku na kwanini alikuacha wewe huko pamoja na baba yako.
Eva: Kwanini mama aliniacha na kuja huku?
Damian: Nikikuambia utaniamini?
Eva: Ndio nitakuamini ikiwa ni kweli… Ila kwanini unaogopa siwezi kukuamini?
Damian: Kwasababu unamuamini sana baba yako.
Eva: Ndio baba yangu namuamini sana.
Damian: Hilo ndio kosa ulilofanya na ndio sehemu ambayo baba yako amefanikiwa.
Eva: Kivipi..!?
Damian: Baba yako amefanikiwa kukufunga akili yako umuamini yeye tu. Hii ndio sababu huwezi kuamini wengine. Unajiuliza kwanini sasa amefanya hivyo…? Amefanya hivyo ili usiujue ukweli mbaya ambao upo nyuma ya kutengana na mke wake, mama yako.
Eva: Sawa niambie sababu ni nini.
Damian: Sawa nitakuambia ila nasikitika baba yako amekupumbaza sana… Ukweli ni kwamba Baba yako ni mtu mbaya sana,baba yako ni mtu mkorofi sana, baba yako ndio aliefanya ukae mbali na mama yako. Baba yako huyo huyo unaempenda alikua anampiga sana mama yako, anamnyanyasa, anamtukana sana. Baba yako anakuambia hajawai kuwa na mwanamke mwingine anakudanganya.
Eva: Muongo!! umewezaje kujua hayo yote?
Damian: Mimi nilikutana na mama yako akanieleza yote hayo. Kwakua sikupendezwa na alichokifanya baba yako na nilikua bado sijaoa nikaamua kuishi na mama yako na kumfanya awe na furaha tena kama ulivyomkuta sahivi. Pia mama yako aliniambia ana-mtoto ambae ni wewe kwahiyo nikafanya jitihada niwezavyo ili nikulete tukae wote. Lakini yote hayo huyajui.
Eva: We muongo!! Nitakuamini vipi? Baba yangu hayupo hivyo, namjua.
Damian: Kama huniamini basi, ila kesho muulize mama yako akuthibitishie labda akisema yeye utamuamini. Lakini kumbuka nimekuambia hayo sio kwajili unipende na kuniamini mimi ila nimekuambia ili upendo uliompa baba yako umpe mama yako, kwasababu ndie anaestahiri upendo huo.
Eva: Sawa nenda, niache kwanza. (kwa hasira)
Damian: Sawa Eva najua nimekumiza lakini ndio ukweli. Aya badae mwanangu.
Eva akabaki na mawazo mengi akiwa pekee yake pale sehemu ya kupumzikia. Akijiuliza maswali na kujibu mwenyewe. Akakumbuka baba yake alimwambie kuwa yeye ndie alimkosea mama yake.
Eva: Baba kweli wewe ndio ulimfanyia hivi mama, ulikukosea nini mama, baba sema sio ya kweli haya.
Upande wa Mr Moses akiwa ofisini kwake na waandishi wa habari.
Mr Moses :
Kwa mwaka huu tumejipanga kuboresha huduma zetu kuwa nzuri zaidi tofauti na miaka iliyopita, kama mnavyojua kampuni yetu iliyumba kidogo miaka kadhaa iliyopita baada ya kufarakana kati yangu mimi na aliyekuwa mke wangu na mshirika wangu wa biashara Madam Joyce, lakini sasa na ahidi tumerudi kwenye mstari kama awali.
Wakati akiendelea na mazungumzo mwandishi mmoja alitumiwa sms:
Sms: Akiruhusu swali la mwisho, mulize lile swali.
Mr Moses: Ok!! niruhusu swali la mwisho... Eeeehh!! ok pale nyuma we uliza?
Mwandishi: Mmh!! Asante Mr Moses, Swali langu ni kuhusu aliekuwa mke wako pmaoja na mshirika wako wa biashara Madam Joyce, kwasababu na yeye umemgusia kwenye mazungumzo yako, watu wanataka kujua kuhusu madai ya kwamba ulikua ukimtolea lugha chafu,kumpiga na kumfanyia matendo mengine ya unyanyasaji kwa mwanamke, vipi unalizungumziaje hili!?
Mr Moses: Ooohhpp!! Ni kweli unayoyasema, mi' pia nayasikia, lakini hayana ukweli wowote zaidi ni ushindani wa kibiashara na makampuni mengine ikiwemo kampuni yake Madam Joyce ambayo pia ni mshindani wetu, so… jambo hili halina ukweli. Mimi na yeye tuliachana vizuri kwa makubaliano ya wote wawili na ukweli yeye ndio aliomba taraka, nikajaribu kutatua ikashindikana ndio maana leo hatupo pamoja. Huo ndio ukweli sio hayo mengine unayoyasikia. Asanteni.
Baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari Mr Moses alitambulisha toleo la nguo mpya kutoka kwenye kampuni yao. Nguo waliyoipa jina Daughter (binti) nguo kwajiri ya watoto wa kike.
Mr Moses: Sasa nawakaribisha kutazama toleo letu jipya la nguo,Nguo imetengenezwa kwa kuzingatia asiri ya kiafrika zaidi na nguo hii inaitwa Daughter mbunifu wa vazi hili ni Eva binti yangu pamoja na mimi mwenyewe kwenye baadhi ya vitu. Nguo hii tumetoa matoleo kwa kuzingatia kila lika. Karibuni sana.
Watu: hongera sana style nzuri ya nguo, inavutia sana./ Woow nimependa sana hii/ Itapatikana wapi/ Inauzwa shi-ngapi n.k.

* ITAENDELEA *

EPISODE 03

MAMA ASIE BORA

1664198206125.png


SIKU ILIYOFUATA
Ni siku ya mapumziko weekend Mama Eva (Joyce) hajenda kazini na leo yupo jikoni akipika chakula kwajili ya mlo wa mchana, Eva akaenda jikoni alipo mama yake.

Joyce: Eva mwanangu mbona unaonekana leo hauna furaha, Kuna nini mwanangu kipenzi. Sijazoe kukuona ukiwa hivyo!?

Eva: Hapana mama, hamna kitu hata. (Akatabasamu)

Joyce: Nambie mwanangu wala usiogope, mama yako nimeona haupo sawa.

Eva: Sawa mama.

Joyce: Aya nambie mwanangu kipenzi.

Eva: Je ni kweli aliyoniambia baba wa kambo?

Joyce: Oooh!! kumbe shida ni hilo tu mwanangu.

Eva: Ndio mama, nataka kujua.

Joyce: Ndio yote aliyokuambia baba yako wa kambo ni ya kweli, unatakiwa umuamini baba yako wa kambo kama unavyo muamini baba yako Mr Moses na hata baba alikuambia huyu ni baba yako pia, sawa Eva.

Eva: Sawa, nakupenda sana mama yangu, sijui kwanini sikukaa pamoja na wewe muda wote huo.

Joyce: Mi pia nilitamani kuwa na wewe mwanangu muda wote.

Eva: Sawa mama ngoja mi niende nikaangalie tv.

Joyce: Sawa mwanangu mi namalizia kuweka mambo sawa hapa ili ule ushibe.

Baada ya Eva kutoka Damian akaingia jikoni alipo Joyce, akaingia kwa kunyata akamkumbatia kwa nyuma huku mikono yake yote miwili akipitisha kiunoni.

Damian: Naona unaongea na binti yako.

Joyce: Ndio!! Lakini nashangaa leo hana furaha kabisa.

Damian: kwani anasemaje?

Joyce: Anauliza maswali kuhusu baba yake, wewe.

Damian: Na wewe umemjibu nini?

Joyce: Nimemjibu kama inavyotakiwa.

Damian: Sawa vizuri kumwambia mtoto ukweli.

Walipokuwa wakizungumza wakasikia sauti ya Eva akiwaita.

Eva: Mama mama!! Njoo umuone baba kwenye tv.

Mama yake pamoja na baba yake wa kambo wakatoka jikoni wakaenda sebureni kuangalia, yalikuwa ni mahojiano yale ya Mr Moses wakati anafanya uzinduzi wa nguo yao mpya kutoka katika kampuni yake, wakasikiliza kwa makini mpaka ilipofikia wakati anaulizwa swali kuhusu kumnyanyasa mkewe... Ukimya ulitawala kidogo kudhihirisha wote wanasikiliza kwa makini. Eva pia anataka kumsikia baba yake anajibu nini. Akasikiliza...

( Mr Moses: ooohh!! Ni kweli unayoyasema…) tv ikazima ghafla!!.

Joyce: Eva kwanini umezima tv!? (kwa hasira)

Eva: Hapana mama!! Yani hata sielewi.

Eva akanyanyuka akaenda chumbani kwake. Mama Eva (Joyce) akachukua rimoti akawasha tv akaendelea kuangalia mahojiano yale. Lakini chumbani alipo Eva pamewaka moto, Eva anahasira, kachukua picha ya baba yake akaitupa chini…

Eva: Baba!! Wewe ni mbaya hivi!? wewe ni mbaya, nakuchukia baba, nakuchukia sana aaahhh!! Kwanini ulimtesa mama yangu. Kwaniniiii…!! (Akiwa anainyoshea kidole ile picha)

BAADA YA WIKI MOJA.

Mr Moses amemkumbuka sana binti yake. Umepita muda mrefu hawajawasiliana na Eva.

Mr Mose: Nimekuwa bize sana, ni wiki moja sasa sijawasiliana na binti yangu, ngoja nimpigie.

Akapiga simu ya Eva lakini ikaita haikupokelewa ikabidi ampigie mama yake, akampigia Madam Joyce akapokea…

Mr Moses: hallo!!?

Joyce: Eeeh hallo!!

Mr Moses: Samahani kwa usumbufu, nashida na Eva nampigia simu yangu lakini hapokei.

Joyce: Ok! ngoja nimuite uongee nae.

: Eva, Evaa njoo uongee na baba.

Eva: Baba mbona nimetoka kuongeanae sahivi!

Joyce: Baba yako Mr Moses.

Eva: Hapana sitaki… sitaki kuongeanae.

Joyce: heeehh!! hutaki?

Eva: Ndio!!

Joyce: Amekataa kuongea na wewe eti.

Mr Moses: Shida nini!? Kuna tatizo gani kwani?

Joyce: Sifahamu, ila toka wiki iliyoisha hana raha kabisa. Lakini nafikiri atakaa sawa tu.

Mr Moses: Labda itakuwa amekasilika maana sijamtafuta wiki nzima.

Joyce: Inawezekana.

Mr Moses: Sawa Joyce, mwambie baba nampenda.

Joyce: Wala usijari nitamuambia.

Mr Moses: Joyce nakukumbuka sana. (Kwa sauti ya chini)

Joyce: Naku-miss sana pia Moses, lakini hatuwezi kuwa pamoja tena.(Kwa sauti ya chini)

Mr Moses: Yeah kweli!! Ok vipi leo hujaend kazini? (Akapotezea)

Joyce: Ndio leo sijaenda, sahivi kila kitu anasimamia Damian na muda sio mrefu amenda kazini.

Mr Moses: Vizuri, naona mnashirikiana. Ok poa utamsalimia Eva.

Joyce: Aya sawa byee.

Mr Moses: byee.

Kazini katika kampuni ya madam Joyce inayoitwa JOY (Furaha). Mr Damian akiwa ofisini anaongea na simu.

Damian: Wewe nivumilie tu… Sahivi imebaki kidogo tu… Aaaah! Siwezi kusahau nakumbuka makubaliano tuliyokubaliana na sahivi nataka nichukue na ile nyingine.

Simu: Sawa mi nakutegemea. (sauti ya mwanamke)

Damian: Wewe usijari mi nitalikamilisha… byee!!

Baada ya kumaliza kuongea na mtu huyo kwenye simu yake Mr Damian akachukua simu ya ofisini kisha akapiga.

Damian: hallo!!, umefatilia vizuri toleo lao jipya?

Simu(mfanyakazi): Ndio boss nimkamilisha.

Damian: Ok! hakikisha tunatengeneza toleo zuri zaidi kuliko hilo la Mr Moses nataka liwe bora kuliko toleo lao.

* ITAENDELEA *
 

Attachments

  • 1664198207312.png
    1664198207312.png
    76.7 KB · Views: 21
Back
Top Bottom