kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Naomba kuuliza Watanzania wenzangu, kuna watu nawafahamu tulisoma nao nje wazazi wao wakiwa ni raia wa Tanzania. Lakini baada ya kukaa kwa muda walibadili uraia wakapata uraia wa kigeni na wakawa wakija nchini Tanzania wanakuja kama wageni.
Wengi wao familia zao ni za wasomi waliopelekwa nje miaka ya 1970-1990 na Sasa ni Wakuu wa Idara, Wizara na Mashirika mbalimbali. Watoto wao nao wanafanya kazi Serikalini na wanaishi kama wabongo.
Swali langu linajikita hapa; hawa raia wa Marekani, uingereza, Australia, sweeden nk ambao waliukataa utanzania wanaruhusiwa kuteuliwa kushika wadhifa kwenye mfumo wa Utumishi wa Umma.
Natama nitaje baadhi waliopo Bugando, Muhimbili, UDSM, foreign affairs, wizara ya mifugo, wizara ya madini, TANROADs na TPA lakini siyo mahala pake. Naomba tu kujua sheria inawawajibisha vipi Hawa watu wanaolipwa ulaya na Tanzania? Watoto wao wanasoma free kwa uraia wa wazazi wao na huku wazazi wameshikilia nafasi za wazawa. Je, sheria inasemaje na ukitaka kuwafichua unaripoti kwa Nani?