Kwanini wenye uraia wa nje wanateuliwa kushika nafasi za juu kwenye Utumishi wa Umma?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Naomba kuuliza Watanzania wenzangu, kuna watu nawafahamu tulisoma nao nje wazazi wao wakiwa ni raia wa Tanzania. Lakini baada ya kukaa kwa muda walibadili uraia wakapata uraia wa kigeni na wakawa wakija nchini Tanzania wanakuja kama wageni.

Wengi wao familia zao ni za wasomi waliopelekwa nje miaka ya 1970-1990 na Sasa ni Wakuu wa Idara, Wizara na Mashirika mbalimbali. Watoto wao nao wanafanya kazi Serikalini na wanaishi kama wabongo.

Swali langu linajikita hapa; hawa raia wa Marekani, uingereza, Australia, sweeden nk ambao waliukataa utanzania wanaruhusiwa kuteuliwa kushika wadhifa kwenye mfumo wa Utumishi wa Umma.

Natama nitaje baadhi waliopo Bugando, Muhimbili, UDSM, foreign affairs, wizara ya mifugo, wizara ya madini, TANROADs na TPA lakini siyo mahala pake. Naomba tu kujua sheria inawawajibisha vipi Hawa watu wanaolipwa ulaya na Tanzania? Watoto wao wanasoma free kwa uraia wa wazazi wao na huku wazazi wameshikilia nafasi za wazawa. Je, sheria inasemaje na ukitaka kuwafichua unaripoti kwa Nani?
 
Sheria haikatazi kuwaajiri unaowasema. Kinachotakiwa ni kupata vibali. mbona kuna wahindi wamarekani, waiongereza, n.k. wanafanya kazi Tanzania kwa vibali? Mbona kuna Watanzania maelfu wanafanya kazxi USA, Australia, Uingereza, n.k. bila kuwa raia wa nchi hizo?

wewe unawezakuwa unachanganya uraia na "permanent residency". Nawajuwa watanzania wanaofanya kazi USA kwa miaka mingi, lakini siyo raia wa huko. Hao huwa wana permanent residency na sdiyo muraia. Wanaposafiri hutumia passport ya TZ.

LAKINI NAONA UNASUMBULIWA NA KAWIVU!
 
Naomba kuuliza Watanzania wenzangu, kuna watu nawafahamu tulisoma nao nje wazazi wao wakiwa ni raia wa Tanzania. Lakini baada ya kukaa kwa muda walibadili uraia wakapata uraia wa kigeni na wakawa wakija nchini Tanzania wanakuja kama wageni...
Acha uchawi,kama una damu ya Kitanzania,we ni Mtanzania,bila kujali makaratasi yanasemaje,Cha msingi hiyo kazi uliyo nayo unaifanya kwa ujuzi na weredi unaotakiwa?

Haya mambo ya kuamini kwamba kwa vile mtu kazaliwa nje ya nchi,akipewa kazi sehemu nyeti, ataisaliti nchi ni fikra mfu, kuzaliwa Nchini na wazazi wote watanzania hakukufanyi uwe mzalendo zaidi ya Yule aliyezaliwa nje na mzazi mmoja Mtanzania.
 
Bado watu waliosoma nje wanaonekana kuwa na weledi na elimu bora kyliko tuliosoma ndani.

Nakubaliana na ukweli huu, ukiacha waliosoma nje vyuo vya kimaghumashi vya India na China, watu waliosomea nje vyuo credible, ni weledi kuliko wa humu ndani. Taifa liwatumie tuu japo wanakwamishwa na mifumo ya serikali
 
Sheria haikatazi kuwaajiri unaowasema. Kinachotakiwa ni kupata vibali. mbona kuna wahindi wamarekani, waiongereza, n.k. wanafanya kazi Tanzania kwa vibali? Mbona kuna Watanzania maelfu wanafanya kazxi USA, Australia, Uingereza, n.k. bila kuwa raia wa nchi hizo?

wewe unawezakuwa unachanganya uraia na "permanent residency". Nawajuwa watanzania wanaofanya kazi USA kwa miaka mingi, lakini siyo raia wa huko. Hao huwa wana permanent residency na sdiyo muraia. Wanaposafiri hutumia passport ya TZ.

LAKINI NAONA UNASUMBULIWA NA KAWIVU!
Hao wahindi wenye vibali wanafanya serikalini?
 
Hata sie wazazi wenu tuna wasiwasi na vyeti vyenu, kusoma gani wenzenu wanapitishwa juu ya vichwa vyenu wanapewa kazi.

Niliwahi kumbeba binti yangu hadi katibu mkuu wa elimu huko, nikamuuliza ni shida gani hapewi mkopo binti yangu.

Alitoa ki meno tukapeleka huko kwenye mikopo na akapewa mkopo muda huo huo.

Haya tuwabebe tena twende huko kwa samia na ma vyeti yenu akasema shida iko wapi hawapi kazi.

Poleni wanangu.
 
Hoja fikirishi. Upande mmoja inahitaji uchanganuzi wa sheria zetu juu ya uraia, ajira, na/au vibali vya kazi. Upande wa pili ni uhitaji wa wataalamu kwenye sekta nyeti nchini.

Wasiliana na Idara ya Uhamiaji kwa ufafanuzi zaidi na/au kuwasilisha ushahidi wako juu ya hao wageni haramu.

Itambulike kuwa ni moja kati ya haki za kibinadamu mtu kuishi popote anapohitaji. Hivyo ni haki ya mtu kubadili uraia kadri ya matakwa yake na kutimiza masharti yanayotakiwa kwa nchi husika.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom