Mimi kifo sikiogopi, alianza kufa mama alipata ajali ya bus nimetoka kumsindikiza asubuhi ibungo mida ya mchana tumeongea akasema karibia afike nusu saa napigiwa simu kuna ajali na mwanye simu amefariki,, wacha kabisa nilikuwa kazini sikuaga kiumbe nilichomoka, mshua Nae alishazipata habari tukafarijiana. Alafu unakuwa auamini hadi ukishazika.... Miaka michache nikampoteza tena mzee aliumwa ghafla kumpeleka hosp asubuhi kesho yake Muda kama alioripoti hosp akatutoka..... Kufiwa kunauma asikuambia mtu..... Mzee na mama walikuwa watafutaji Sana na kama ni urithi wameacha wa kukumbukwa..... Waliangaika Sana walijitesa usiku na mchana kununua maeneo kujenga nyumba zote wameziacha na awakuna mawazo kama watakufa mapema hata Mimi sikuwai kuwaza vifo vyao.... Mimi Bado Nina mipangp mingi Sana kichwani na kuna vitu nataka kuvifanya Ila ninapowaza kifoooooooo ninavyunjika Moyo Nipo above 25.last Saturday nilikuwa kilimanjato st marygoreti graduation ya mdogo wangu nikasalimiana na mzee mmoja na yeye alikuja kwenye graduation ya mtoto wake, ninavyoandika Nipo kwenye msiba wa huyo mzee alipata ajali alhamisi usiku maeneo YA mlandiz bahati mbaya alifariki.
Mshana Jr. Ebu toa wazo kijana wa mzee anae subiri kuanza paper la six mwezi may tumpe taarifa au tuuchune na kuna mdogo wake yupo form three hapohapo yeye atakuwa likizo YA Ester next week atakuja nyumban na atapata taarifa zote na baada YA Wiki mbili atarudi shule ataweza kujizuia akionana na ndugu yake asiweze kumwambia majanga yaliyopo nyumbaniii.... Ebu oneni kifo kilivyo hadi kuna wakati nasema kwanini Mungu aliweka kifo....