Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,826
- 730,248
Ndani za hizo makala kuna nyingine ni za kutiana moyo na kuondoana hofu huku nyingine zikielezea dhana mbalimbali na nyingine zikiwa ni masimulizi ya kweli
Nia yangu si kuleta hofu wala kumtisha mtu bali kupandikiza mbegu ya uzoevu katika vitu visivyozoeleka.... Hasa kifo
Hofu ya wengi kwenye kifo ni hii
Kwamba hatutaonana na wapendwa wetu tena
Kwamba miili yetu hii itaharibika na kuoza kabisa
Kwamba hatuna hakika na huko tuendako
Kwamba je ni kweli kuna pepo jehanam au rebirth/reincarnation?
Kwamba tunaachana na starehe za dunia hii na mali zote tulizochuma?
Lakini kubwa zaidi ni ule upweke kile kiza na zile kilo za mchanga ndani chini ya kaburi pekeyako kabisa .....na zile hari za kifo mwili unapotengana na roho I mean yale mateso yake zile dakika na sekunde za mwisho
Mbali ya hayo yote ni zile fikra za wale wapendwa wetu waliotangulia huko, kwamba wako wapi sasa na wanafanya nini huku ukionyeshwa mapicha ya marehemu Waliobaki mifupa tuu.....
Usimlaumu anayeogopa kifo ndani ya kaburi lililofunikwa kuna siri nyingi tusizozijua