Kifo cha Mjamzito Irene Tillya na mwanaye utata mtupu

Kifo cha Mjamzito Irene Tillya na mwanaye utata mtupu

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
254
Reaction score
258
KIFO CHA MAMA MJAMZITO,MTOTO AKIJIFUNGUA UTATA

Barnaba Tillya mme wa marehemu Irene Tillya mpaka sasa haamini kama kweli mke wake kipenzi hayupo duniani na kila anapofikiria kilichotokea ndani ya wodi ya wazi na baadaye chumba cha upasuaji ndivyo anavyozidi kuchanganyiikiwa.

Ni tukio linaloumiza hasa ikizingatia kuwa serikali yetu ipo katika kampeni kubwa sana ya kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na ikiwezekana kuvitokomeza kabisa.

Juni 4 mwaka huu katika Hospital ya Marangu inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT),Dayosisi ya Kaskazini.Irene Tillya,alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wa kiume ambaye naye alifariki.

Simulizi ya mmewe anayoitoa akirejea tukio hilo ni dhahiri kuwa kabla ya Irene kufariki dunia na kichanga chake alipitia matese makali ambayo madaktari waliokuwa wakimhudumia waliona ni jambo la kawaida mjamzito kupiga kelele za kuomba msaada awapo wodi ya uzazi.

Tillya alikuwepo mlangoni mwa wodi ya wazazi kuanzia saa moja jioni akishudia kelele nyingi zikipigwa na mkewe akiomba msaada hadi saa 6 usiku hali ilipotulia na alichoshuhudia ni kuona mwili wa mke wake mpendwa ukitolewa wodi ya wazazi na kupelekwa chumba cha upasuaji.

Anakumbuka baada ya muda madaktari ambao hawakumpa msaada alipoomba aingie wodini kuona ni nini anahitaji mke wake ,walimfuata na kumuuliza ananukuu “mzee una watoto wangapi na mke wako”,swali ambalo lilimwogofya na kuhoji kulikoni.

Anasema baadae akaelezwa ya kwamba mkewe na mtoto hawapo tena duniani hali iliyoibua kilio si kwake pekee bali ndugu zake wote waliokuwa wamefurika Hospitalini kushuhudia ndugu yao kipenzi akijifungua na hatimaye kurejea nyumbani akiwa na zawadi yake ya mtoto kwa mmewe.

Tilya ambaye kwa sasa ni kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na mkasa huo,anasema siku ya tukio mkewe ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa kuuza ndizi jijini Dar es salaam na biashara nyingine katika soko kubwa la nguo la Memorial mkewe alikuwa ni mwenye afya nzuri tu.

Anasema mkewe aliamka na kwenda sokoni kukusanya ndizi na kuweka tayari kusafrishwa na kurejea nyumbani na aliingia jikoni kuandaa chakula cha jioni kabla ya kuhisi uchungu na kuanza kujiandaa kwenda Hospital kwa hatua zaidi za kujifungua.

Irene kutokana na hali hiyo hakuweza kula na alimweleza mmewe aweke chakula kwenye Friji akimwahidi chakula hicho atakila kesho yake pindi atakaporejea kutoka Hopsitalini lakini Irene alirejea nyumbani baada ya siku saba akiwa ndani ya jeneza.

Tilya anaomba serikali ifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo cha mke wake pamoja na mtoto na endapo itabainika kulikuwa na uzembe uliopelekea vifo hivyo basi hatua stahiki zichukuliwe kwa waliohusika na uzembe huo ili kunusuru maisha ya wajawazito wengine wanaofika Hospitalini hapo kujifungua.

Tillya anasema yapo mambo kadha yanayotia shaka kuhusiana na kifo hicho,anasema awali madaktari walimweleza mke wake wakati anahudhulia kliniki kuwa atalazimika kufanyiwa upasuaji kutokana na mke wake kukaa muda mrefu bila kushika ujauzito (miaka 13)lakini siku ya tukio pamoja na kumjulisha daktari aliyekuwa akimhudumia mara kwa mara ya kwamba anaelekea Hopsitalini,daktari huyo alimjibu kwa kuchelewa na alipomjibu alimpa hongera na kumweleza atajifungua kawaida na hapana shaka.

Jambo jingine anasema mke wake alifanyiwa vipimo mara mbili ambavyo vilileta majibu tofauti kipimo cha kwanza kikionyesha kiumbe kilichopo tumboni ni cha kike na Irene akaanza kuandaa mahitaji ya mtoto wa kike lakini kipimo cha pili kikaonyesha kiumbe cha kiume hivyo akaanza tena kuandaa mahitaji ya mtoto wa kiume vipimo vyote vikifanywa na madaktari wale wale katika hospitali hiyo hiyo.

JE UNAJUA DMO NA DED MOSHI DC WAMEJIBU NINI JUU YA TUKIO HILO?

NA JE UNAJUA NI MAMBO GANI YANAWEZA KUSABABISHA KIFO CHA MJAMZITO WAKATI WA KUJIFUNGUA?,NITARUDI HAPA BAADAE

PICHANI BARNABA TILLYA IKIANGALIA MAKABURI MAWILI YA WAPENDWA WAKE, KUSHOTO NI KABURI LA MWANAYE NA KULIA NI KABURI LA MKE WAKE KIPENZI.

KABURI.JPG
 
Nimehuzunika sana baada ya kusoma bandiko, Mwenye Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi, na mamlaka husika zichukue hatua stahiki kama Kuna uzembe waliohusika wawajibishwe
 
Back
Top Bottom