Tahadhari kwa watumiaji wa TECNO, Infinix na iTel

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
776
2,404
Mimi ni fundi simu upande wa hardware na ni mzoefu kwa miaka 10 na 90% ya simu ninazotengeza ni tecno, infinix na itel. ni kweli kila simu inaharibika na kila siku napokea simu zenye matatizo mengi na matatizo mengi ni yale tuliyo yazoea.
Lakini kuna mengine ni mapya kulingana na teknolojia inavyo kuwa.

Lakini kuna matatizo ambayo nimeyagundua kwenye hizo simu tatu kwa hii wiki nimepokea
Simu karibia 15 ambazo zimezima Peke yake na kwa maelezo ya wateja wanasema walikuwa wameziweka tu ndani.

Na kwa sababu mbali mbali Na mwisho wa siku wakakuta zimezima peke yake Na hizo simu mara nyingi huwa nikizipima na nakuta zina umeme mdogo ambao hauwezi kuwasha simu. hata ukibusti betri haziwaki kabisa hata ukiweka betri mpya zenye moto wa kutosha haziwaki na hata tukichomeka kwenye kwenye computer ili kuziflashi zinakuwa hazionekani kabisa. Na hivyo ndivyo zinakuwa imekufa moja kwa moja.

Lakini baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu nimegundua hizo simu nyingi zinazozima kwa namna hiyo ni zile simu zilizo Isha warranty na nimeyagundua hizo simu ni zile toka zimetengenezwa baada ya mwaka mmoja na ikikaa siku 30 ikiwa imezima chaji hiyo simu ujue itakufa moja kwa moja.

Na nimegundua hiyo inatoka na mikataba mibovu waliyo Ingia hayo makampuni yanayo wauzia software kwamba wao wanao wauzia software wanawapa security ya mwaka mmoja tu.

Kwahiyo ushauri wangu kwa watumiaji wa infinix tecno na itel usiiache simu yako iishe chaji kabisa na ikae siku 30 bila kuichaji.

Wakati tunaendelea kutafuta solution.
 
Back
Top Bottom