#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Msweet unapotosha kwa makusudi. Hakuna dawa au chanjo duniani yenye success rate ya 100%

Ni sawa na kusema eti kma ARV haiponeshi Ukimwi wala haizuii kuambukiza mtu basi tusitumie kabisa..... Mtu akiugua VVU aachwe tu mpaka afe maana hta akitumia ARV sio guarantee ya kupona au kutoambukiza? Are you out of ur senses.

Then anasema ukipata madhara serikali haipo liable? Hvi ukipata madhara kwa kutumia Panadol kuna compensation? Ama ukitumia Radiotherapy ikaleta madhara kuna fidia? Hta operation huwa una sign ikifeli (sio kwa uzembe wa daktari) hakunaga compensation!! Sasa kipi kipya hapo?

Kuvaa barakoa na social distance haziwezi kuachwa kisa umechanjwa sababu risk ya kupata tena ipo hta kma ni 0.0001% so why take chances? Ukitumia dawa mseto huwa bado tunaambiwa tulale ndani ya neti..... Huwa hatuachi eti sababu tunatumia dozi!! Precaution ni muhimu.....
 
Attachments

  • VID-20210326-WA0012.mp4
    6 MB
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.
Tuwekee pia nakala ya utafiti ulioufanya.
 
Mkuu inaonyesha haujui ugonjwa wa korona ulivyo!! Hapa tunalilia protection ya 3% population wasiondoke na korona.....3% ndio wahanga wa corona ...97% wana survive kwahiyo sizungumzia hao 97% wasiojali kabisa....tuwajali hao 3% wasiondoke na korona.....

Unajua kwamba katika 100 watakaopata korona 85 wanaweza kupona bila kuonyesha dalili? Kujazana kwenye masoko au madaladala bila kuvaa korona haimaanishi kwamba watu hawaambukizani au ugonjwa haupo....

ukitaka kujua stats za ugonjwa fika hospital.....Madaktari wanajua ila mimi na wewe ambao hatupo kwenye hizo kada tutaona kwamba korona hakuna coz watu hawavai barakoa na wanajazana kwenye masoko.
Hii kauli ya madaktari kujua inatumika kizushi tu kwa sababu huko hospitali kungekuwa na tahadhari ya hali ya juu kwa sababu wanajua uhalisia ila ndio kwanza wamelegeza masharti, mwanzo ilikuwa huingii bila barakoa ila sasa sio lazima tena halafu ndio useme wansjua kuwa kuna corona? Hata ile kamati basi ingetuambia vitu kama hivyo ila wapi.
 
Mie sijawahi kuzungumza hivyo vitu, halafu cha ajabu bongo huku huwa mnasema corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka ndio sababu sasa bongo inaonekana hakuna corona ila huko vaccine ndio mnaisimia kuondoa maambukizi.
Hujaelewa..... Chanjo sio mpaka ugonjwa uwepo ila unajihami kabla ya mlipuko kufika.

Ila ningeomba maoni yako juu ya ugonjwa kupungua nchi kma UK na Israel baada ya chanjo kuzagaa zaidi ya 60% ya population.
 
Sasa si ndio nimekwambia Tanzania tukisema mbona tunakusanyana tu na hatuoni kinachotokea huwa mnajibu kuwa corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka kwa maana sasa umepungua na bila ya chanjo, ila huko kwa wenzetu mnatuambia chanjo ndio zimepunguza maambukizi na si kwamba corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka.
 
Hii kauli ya madaktari kujua inatumika kizushi tu kwa sababu huko hospitali kungekuwa na tahadhari ya hali ya juu kwa sababu wanajua uhalisia ila ndio kwanza wamelegeza masharti, mwanzo ilikuwa huingii bila barakoa ila sasa sio lazima tena halafu ndio useme wansjua kuwa kuna corona? Hata ile kamati basi ingetuambia vitu kama hivyo ila wapi.
Nimemsikia dakatari kutoka MAT(Mwenyekiti wao) alikuwa anahojiwa na Azam alikiri kabisa kwamba wana wagonjwa wa corona.....Swala la kujilinda ni jikumu la mtu mwenyewe ,kila siku wanatoa matangazo jinsi ya kujikinga na malaria lakini kuna watu bado wanalala bila net ,kulala bila net hakumaanishi kwamba hakuna malaria.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1) Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa

2) Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea

3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo

4) Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Huu ujinga kauleta jiwe
 
Nionavyo mimi, wanaokataa chanjo hawana sababu zozote za msingi, isipokuwa waliaminishwa kwamba chanjo zinatulenga sisi kwenye vita ya kiuchumi na ndiyo maana baadhi ya watu wakaanza kuwa na mtazamo hasi na kuamini kuwa waliogundua chanjo hawana nia njema nasi. Lakini ukimuuliza mtu yeyote anayekataa chanjo kama ana ushahidi wowote wa kisayansi (na siyo ramli) hakuna mwenye huo ushahidi kwamba chanjo wanayoikataa ina madhara gani kwao. Baadhi wanapinga kutokana tu na 'ignorance' na hasa kwa sababu ya kudanganywa na wao kudanganyika kwa sababu mpaka leo hii watoto wao bado wanapata chanjo ambazo hazikugunduliwa hapa nchini, lakini hakuna aliyewahi kupinga chanjo ya surua, porlio, tetekuwanga nk. Jambo la kuzingatia ni kwamba tunaposhauriwa na wataalamu wa afya tuwe na 'trust' kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wetu na kama tukikataa jambo angalau tuwe na sababu za msingi za kufanya hivyo na siyo tu kufuata mkumbo wa watu wenye mtazamo hasi kuhusu utafiti ambao umefanywa na wataalamu kama wa Shirika la Afya Duniani. Tujifunze kufanya mambo kisayansi na tutafika mbali kuliko kukalia kupiga ramli.
 
Hili la chanjo ni jambo tata kidogo, limekaa ktk sura ya hiari ila ndani yake kuna ulazima flani kwa wenye mataifa yao.
Tunaweza kuamua kama nchi tukakataa huo ulazima na ikabaki katika uhiari kwa mwenye kutaka, ila kama jambo hili ni mkakati wa wenye mataifa yao tusitegemee kupata viza bila chanjo, na hapo ndipo ulazima wa wenye jambo lao unapo chukuwa nafasi.
 
Nimemsikia dakatari kutoka MAT(Mwenyekiti wao) alikuwa anahojiwa na Azam alikiri kabisa kwamba wana wagonjwa wa corona.....Swala la kujilinda ni jikumu la mtu mwenyewe ,kila siku wanatoa matangazo jinsi ya kujikinga na malaria lakini kuna watu bado wanalala bila net ,kulala bila net hakumaanishi kwamba hakuna malaria.
Nazungumzia huko hospitali ambako kulikuwa na masharti ya kutokuingia bila barakoa na kunawa mikono kwa sababu ya corona ila sasa hakuna hayo masharti.
 
Kwahiyo kama hakuna masharti ina maana ndio ugonjwa hakuna? Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania amesema bado kuna wagonjwa wa korona hospital mim na wewe ambao ni mangubaru inakuwaje tubishe?
 
Hoja ni kwamba huko hospitali ndio wanajua uhalisia wa corona ndio nimeuliza mbona huko hakuna masharti kama zamani na wakati huko ndio kwenye wagonjwa wa corona?
 
Back
Top Bottom