Kwanini Watanzania tusianze massive constructions of apartments nchi nzima?

Kwanini Watanzania tusianze massive constructions of apartments nchi nzima?

Ni kweli nimekuelewa mkuu
Lakini kwa sasa bora tuanze hata na specific areas mfano kulenga maeneo ya uswazi tu kwa miji ya Dar, Mwanza na Mbeya maana kwa Tanzania nadhani hii ndio top 3 ya miji ya uswazi
Tungeanza hata huko mdogo mdogo

Umewahi kuona view ya Dar ndege zikiwa zinatua airport? Ule uswazi, tungeanza kurekebisha maeneo kama hayo

Nakuelewa vizuri na nimeruka sana na ndege na nakwazika sana kuona hali hiyo. Issue inakuja kwamba ili pabadilike ni kwamba uchumi unakuja kuplay nafasi kubwa kwa kuwa hizo ni nyumba za watu na ni watu maskini so cha kwanza ni kuimarisha uchumi wa watu. Uchumi ukikua ndio mahitaji makazi bora yanakuja na hii inafanywa zaidi kwa kurekebisha policies zitakazoongeza production na kupanua middle class. Then demand na soko la nyumba linakua na kuvuta uwekezaji wa kibiashara na wa makazi binafsi. Makampuni na mitaji (hasa ya massive apartments) yanakuja kunapokuwa na soko na policies zinazotabirika za uwekezaji na liwe na uwezo wa kugharamia hizo nyumba mpya! Vinginevyo ni mtu mmoja mmoja kubadilisha makazi yake mwenyewe!

Ukitazama nchi zilizofanikiwa kwa mfano wanatoa freehold title ya ardhi, hapo kwetu wanasema ardhi ni ya mama na unalease kwa miaka 33, 66 au 99 (zamani kulikua na 999 pia), yani mtu uweke matrilioni then mama akishauriwa kufuta tittle yanakuwa kama ubinafsishaji wa miaka ya azimio la Arusha ilivyokua, hamna mtu atarisk mitaji mikubwa kwa policies za namna hii! Mtu anakwazwa na wakenya watatu anaharibu kabisa biashara na nchi nzima, huu si wehu mkuu?
 
Zanzibar sasahivi wanajenga apartments na Hussein Mwinyi ameeleza vizuri faida zake na kuwa lengo lao ni kupunguza makazi duni. Ni serious project kuliko hizi za huku Tanzania bara ambazo lengo lao ni biashara na sio kupunguza makazi duni
Wachina na Wakorea wanaishi kwenye apartments wengi wao na watoto wao wana malezi mazuri tu.
Pia sio lazima ziwe apartments ndefu, zinaweza kuwa hata za ghorofa 1 au 2 hadi 5
Na pia kunakuwa na ujenzi wa maeneo kama haya pia. Hii ni South Africa, linakuwa chaguo la watu ambao hawataki apartments. Ni bora hivi kuliko uswazi
View attachment 3544391

.
Fananisha na hapa Mbeya
View attachment 3544394
Hiyo Bukina du, kiongozi mda mfupi mabadiriko makubwa hivi anatoa wapi pesa,mbona wenziwe kina Kombo wanashinda kubembeleza wazungu.. Mwinyi anaroho nzuri Zanziber itabadirika huyu Samia analipiza kisasi wabara waliidhulumu Zanziber miaka mingi sasa atawaonesha. yalihitajika mapinduzi hakika.
 
Watanzania hawana utamaduni wa kuishi kwenye ALARTMENTS.

Watanzania wengi ni WAFUGAJI, WAKUKIMA.WADOGO na WAVUVI.

Huwezi kuwaweka kwe ye APARTMENTS.

Halafu suala la ubora wa nyumba, halina mahusiano na APARTMENTS.
Kwenye miji mikubwa kama Dar sidhani kama watu wanaoishi hapa ni wakulima na wafugaji kama unavyodai
1770876634409.jpg
Tanzania kuna shughuli nyingi sana, na kwa mijini shughuli kubwa zaidi ni biashara ya kuuza bidhaa kwenye maeneo yenye watu wengi, na sio ufugaji kama unavyosema.

And hata tuki assume hao watu wanaokaa hapo ni wafugaji still kuna namna nyingi ya kujenga affordable houses ambazo zinafaa sio lazima maghorofa. Zinakuwa kama hizi za South Africa, ziwe na bei ya chini ili watu waweze kumudu. This is way better than uswazi
new-township-kwazulu-natal-south-africa-JJ0R87.jpg
 
Nakuelewa vizuri na nimeruka sana na ndege na nakwazika sana kuona hali hiyo. Issue inakuja kwamba ili pabadilike ni kwamba uchumi unakuja kuplay nafasi kubwa kwa kuwa hizo ni nyumba za watu na ni watu maskini so cha kwanza ni kuimarisha uchumi wa watu. Uchumi ukikua ndio mahitaji makazi bora yanakuja na hii inafanywa zaidi kwa kurekebisha policies zitakazoongeza production na kupanua middle class. Then demand na soko la nyumba linakua na kuvuta uwekezaji wa kibiashara na wa makazi binafsi. Makampuni na mitaji (hasa ya massive apartments) yanakuja kunapokuwa na soko na policies zinazotabirika za uwekezaji na liwe na uwezo wa kugharamia hizo nyumba mpya! Vinginevyo ni mtu mmoja mmoja kubadilisha makazi yake mwenyewe!

Ukitazama nchi zilizofanikiwa kwa mfano wanatoa freehold title ya ardhi, hapo kwetu wanasema ardhi ni ya mama na unalease kwa miaka 33, 66 au 99 (zamani kulikua na 999 pia), yani mtu uweke matrilioni then mama akishauriwa kufuta tittle yanakuwa kama ubinafsishaji wa miaka ya azimio la Arusha ilivyokua, hamna mtu atarisk mitaji mikubwa kwa policies za namna hii! Mtu anakwazwa na wakenya watatu anaharibu kabisa biashara na nchi nzima, huu si wehu mkuu?
Sawa mkuu
 
Ha ha ha hebu tafuta maoni ya wana JF kwenye thread zinazohusu apartments zina,ouzwa na NHC au watu binafsi. Nchi ngumu sana hii. Binafsi nakubaliana na kauli ya Jafo. Zile sehemu kama Buguruni,Tandale etc wabomoe zile nyumba wajenge magorofa wale wakazi wa zamani wapewe unit zao. Maeneo mengine tusimamie mipango miji tu. Kibali cha uje zi kinasema ni aian gani ya nyumba inatakiwa kujengwa eneo fulani.
 
Kusema ukweli Tanzania tunahitaji apartments kwa sasa. Kwa nini tusijifunze kutoka kwa nchi kama China, South Korea, Singapore nk? Hizi nchi watu wake walikuwa wanaishi kwenye makazi duni sana miaka ya 1960s. Serikali zao zikaanza ujenzi wa apartments ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata kuishi kwenye makazi bora. Na leo hii wamefanikiwa, watu wanaishi kwenye makazi mazuri
Nasema hivi kwa sababu clearly hii ya kila mtu kujenga nyumba yake mwenyewe imetushinda. Watu wasijenge nyumba mpaka wajipate, kipindi wanajitafuta wakae kwenye apartments za serikali au kampuni binafsi
NHC wanajenga apartments Dodoma na hata Dar tumeona miradi kama Kawe 711 na Samia Housing Scheme lakini kusema ukweli hii hata haitasaidia kitu. Nyumba za NHC huwa ni expensive ndio maana wanaishia kukaa wahindi na waarabu. Inapaswa zijengwe apartments na bei ziwe rafiki kwa Watanzania wa kawaida ili kupunguza makazi holela, sio hizi za NHC ambazo bei zake Wana afford foreigners tu. Na hata Watanzania wanao afford ni mara kumi wajenge nyumba zao wenyewe maana watapata nyumba nzuri zaidi

Take a look at this

Hapa ni Mbeya
View attachment 3544366
Umeona jinsi nyumba zilivyojengwa bila mpangilio na kuchukua ardhi kubwa bila sababu za msingi? Lakini kama zingejengwa apartment kadhaa, zikapandwa nyasi, miti, mitaro na sewage system mazingira yangekuwa mazuri zaidi ya hivi. Matatizo kama mafuriko, kipindupindu, maeneo kutofikika nk yangepungua na mji ungependeza kimuonekano

Hapa ni Dar
View attachment 3544367
Angalia hicho kipande kidogo kilichojengwa hovyo bila mpangilio
Na hapa pia ni Dar 👇
View attachment 3544369
.
.

Hapa ni MwanzaView attachment 3544368
Hawa watu wote wanaoishi kwenye nyumba zinazoonekana kwenye picha wangetosha kama wangekaa kwenye apartment moja pekee.

Kuzuia mambo kama haya ndio maana Wachina waliamua kujenga apartments nyingi nchi nzima

KWA NINI WACHINA WALIAMUA KUJENGA APARTMENTS NYINGI NCHI NZIMA?

Hapa sababu zote zipo applicable hata hapa Tanzania

1. Ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na mijini
China ina miji mikubwa yenye watu wengi. Kwa sababu ya uhamiaji mkubwa kutoka vijijini kwenda mijini (urbanization), kuna hitaji kubwa la makazi. Apartments ni suluhisho linaloweza kuchukua watu wengi katika eneo dogo. Ni kama tu hapa Tanzania (Jiji la Dar lina watu takribani milioni 5.3, Jiji la Mwanza watu milioni 1, majiji ya Arusha, Dodoma na Mbeya yana watu takribani laki 6 each)

2. Ufanisi wa ardhi na rasilimali
Ardhi mjini ni ya thamani kubwa. Kujenga nyumba za ghorofa nyingi (high-rise apartments) kunaruhusu kutumia ardhi kidogo lakini kufikia idadi kubwa ya familia.

3. Kurekebisha gharama za makazi
Apartments nyingi kwa mpango mmoja (mass housing) zinafanya gharama ya kila nyumba kuwa nafuu zaidi kuliko kujenga nyumba binafsi. Serikali pia inaweza kudhibiti bei za nyumba kwa urahisi zaidi.
View attachment 3544376
4. Kurahisisha huduma za kijamii
Wakati watu wengi wakiishi karibu kwenye buildings za makazi, ni rahisi kutoa huduma kama barabara, maji, umeme, shule, hospitali, na usafishaji wa miji.

FAIDA ZA SERIKALI KUJENGA APARTMENT NYINGI TANZANIA NZIMA
1. Bei nafuu kwa wananchi wa kawaida: Serikali inasaidia baadhi ya gharama, hivyo ni rahisi kwa watu wenye kipato cha kati au kidogo. Kuliko kujichanga na kujenga nyumba ambazo ni below standard ni heri mwananchi apange kwenye apartment za bei nafuu

2. Mpango wa usafi na afya
Miji mipya inafanyiwa urban planning, hivyo barabara, mifereji ya maji, na taka zinapangwa vizuri. Kuliko mazingira ya uswazi. Mpangilio mbovu una attract uchafu, watu wanatupa taka hovyo na hawaoni aibu kwa sababu mazingira yenyewe hayavutii. Hii ni human psychology (Broken window theory)
View attachment 3544375
3. Usalama
Blocks za apartments mara nyingi zina milango ya kudhibiti, CCTV, na wakaguzi wa usalama. Ukiangalia nchi zote ambazo wananchi wake wanaishi sana kwenye apartment ndio zinaongoza kwa usalama duniani (China, South Korea, Japan, Singapore)
View attachment 3544377
4. Huduma zinakuwa karibu
Shule, maduka, vituo vya afya na maegesho ya umma mara nyingi vipo ndani ya maeneo hayo.

MUUNDO NA MPANGILIO WA MITAA YA APARTMENTS KWA AJILI YA WANANCHI CHINA (Chinese residential neighborhoods)
View attachment 3544372
1. Apartments zinaunganishwa na barabara pana za magari na njia za watembea kwa miguu.

2. Zinajengewa bustani ndogo, miti, na maeneo ya michezo kwa watoto.

3. Urban planning
Kila block ina eneo lake la park, shule, soko, frame za maduka ya msingi karibu nk
View attachment 3544373
4. Mfumo wa maji na umeme umewekwa ili kuepuka matatizo ya usafi na msongamano.

5. Kunakuwa na njia za baiskeli na barabara za watembea kwa miguu

Kwa sababu ni housing mass-production, bei inabakia chini kuliko nyumba binafsi.
Apartments ndogo zina bei nafuu zaidi, zinazofaa kwa vijana, wafanyakazi wa maofisini, familia zinazojitafuta, na hata zilizojipata

View attachment 3544374
Mitaa ya apartments inavyokuwa, unaweza kukuta residential compounds yenye ghorofa 10–30.
Kila block ina green space: miti midogo, bustani za michezo, na sehemu za kukaa.
Njia za barabara haziwezi kuwa na msongamano mkubwa kwa sababu zoning imepangwa vizuri: makazi, biashara, na huduma za jamii hazichanganyiki bila mpangilio.
View attachment 3544378View attachment 3544379
Hizi apartments ndio zimesaidia China kutokuwa na mitaa ya hovyo kama ya hapa kwetu Tanzania. Apartments ni better option ya makazi
Fikiria nchi kama USA Ina uchumi mkubwa kuliko China na Ina watu wachache kuliko China (China Ina watu bilioni 1.4, USA Ina watu milioni 350) lakini USA ina homeless people wengi kuliko China. That means Chinese way is more effective
Hapa Tanzania nako homeless sio wengi lakini sasa watu wanakaa kwenye makazi dunia. Ni muda sasa tuanze kujenga apartments nyingi kila kona ya Tanzania ili watu wakae kwenye nyumba nzuri. Kodi ziwe chini na sisi nchi yetu ipendeze, tupunguze urban sprawl, na matumizi ya ardhi yasiyo ya lazima.
NHC waache kujengea nyumba wahindi na waarabu, waweke bei rafiki ili Watanzania waone sababu za kuhamia kwenye apartments.
Wala sio lazima ziwe apartments ndefu kama za China. Huku hata zikijengwa za urefu wa 5 floors each inatosha
Maana hii hali sio nzuri 👇View attachment 3544369
Mkuu naona Ujamaa umekujaa kichwani mno

Promise Everything,Deliver Nothing and then find someone to Blame!

Kazi ya serikali ni kupima na ku-allocate viwanja,wananchi binafsi ni kazi yao kujenga,serikali haiwezi

Nyumba zijengwe na serikali Hela zitoke wapi?

Nyumba zijengwe,wananchi wapewe bure?Jibu ni no,lazima walipie na faida juu,wana uwezo huo?Jibu ni hapana maana hakuna uchumi mkubwa kiasi hicho kuwapa uwezo wa mmoja mmoja kununua

Kila mwananchi haruhusiwi kua na nyumba,wachache ndio wanaruhusiwa kua na ownership

Wananchi wote 70mil wakimiliki homes,uchumi mzima uta-collapse....kila mtu ana nyumba nani akafanye kazi?

Kila mtu ana nyumba maana yake kila mmoja anaweza kukopa,hakuna hela kiasi hicho kukopesha wananchi 70mil

kila mtu ana nyumba,thamani za nyumba zote zitashuka na kua worthless maana hakuna scarcity

Kila mtu ana nyumba nani apange?nani anunue nyumba au jengo kwa nani?hakuna

Ardhi ndio inashika uchumi baada ya gold,ardhi ikiwa worthless uchumi mzima unaenda na maji

Haiwezekani na haikubaliki kila mwananchi awe na nyumba,lazima kuwe na scarcity ili watu wafanye kazi uchumi uende mbele
 
Kwanza ume assume kwamba wananchi wakiwa milioni 70 basi kila mmoja anapaswa kumiliki nyumba moja yani nyumba milioni 70 kwa watu milioni 70 kitu ambacho hakiwezekani. Unasahau kwamba nyumba moja inaweza kubeba familia ya watu 3 hadi 5, na katika hao milioni 70 wengine ni watoto wadogo, wanafunzi, young population ambao hawajafikia muda wa kumiliki nyumba zao bado nk. Nyumba moja ni kwa ajili ya familia moja, sio kwa ajili ya mtu mmoja
Mtu mmoja anahitaji chumba, sio nyumba.

Pili ujenzi wa nyumba kama huu unafanyika maeneo ya mjini (urban areas) ambayo kwa Tanzania ni only 35% of the population ndio wanaishi kwenye urban areas. The rest 65% hawahusiki kwenye miradi ya namna hii

Tatu, sijasema wananchi wapewe nyumba bure. Nimesema walipe kodi ya bei rafiki ambazo zipo ndani ya uwezo wa Watanzania wengi. Ukisema wananchi wapewe nyumba bure hayo ni maneno yako mwenyewe

Nne umesahau kuwa katika hao 35% wanaoishi mjini sio kila mtu ana nyumba mbaya au anakaa uswazi. Ni kama ume assume Tanzania nzima wana nyumba mbaya kwa hiyo nasema serikali iwajengee which is big NO. Kuna watu wengi wana nyumba nzuri au za kati which is fine

Mimi naongelea miradi ya ku get rid of maeneo kama haya
mbeya-tanzania-drone-view-to-city-in-africa-2NAJPB2.jpg
Screenshot_20260215-160426.png
1770876634409.jpg

.
.
Yawe replaced na maeneo kama haya
FB_IMG_1771164412058.jpg
new-township-kwazulu-natal-south-africa-JJ0R87.jpg

.
.
Sijasema serikali ijengee nyumba wananchi milioni 70
 
Hiyo Bukina du, kiongozi mda mfupi mabadiriko makubwa hivi anatoa wapi pesa,mbona wenziwe kina Kombo wanashinda kubembeleza wazungu.. Mwinyi anaroho nzuri Zanziber itabadirika huyu Samia analipiza kisasi wabara waliidhulumu Zanziber miaka mingi sasa atawaonesha. yalihitajika mapinduzi hakika.
Ibrahim Traore anaipenda nchi yake ndio maana inaendelea
Mi nashangaa hapa JF ukisema Tanzania tuanze kutengeneza magari wanakuambia hakiwezekani wakati Burkina Faso wanatengeneza magari ya umeme sasahivi (yanaitwa ITAOUA)
Ukisema tujenge apartment maeneo ya uswazi kuna watu hapa wanasema hela hatuna. Sasa mbona Burkina Faso, Kenya, Angola nk wameanza hizi project. Hapa Tz project zilizopo za NHC hazijalenga Watanzania masikini na wala hawafanyi elimination ya uswazi areas

Hata treni ya umeme watu walisema hakiwezekani kuanzisha. Watanzania inapaswa tubadilike mindset. Hii mindset ya "Hakiwezekani" ni mbaya sana. Traore hana mindset ya hivi ndio maana Burkina Faso imejenga apartments nyingi na wanatengeneza magari ya umeme sasahivi. In short anaweza kuanzisha vitu ambavyo hapa Tz tunabaki kushangaa tu, amewezaje
 
Stori za Burkina Faso zinaaminiwa na wapumbavu na wavivu tu.
 
Kwanza ume assume kwamba wananchi wakiwa milioni 70 basi kila mmoja anapaswa kumiliki nyumba moja yani nyumba milioni 70 kwa watu milioni 70 kitu ambacho hakiwezekani. Unasahau kwamba nyumba moja inaweza kubeba familia ya watu 3 hadi 5, na katika hao milioni 70 wengine ni watoto wadogo, wanafunzi, young population ambao hawajafikia muda wa kumiliki nyumba zao bado nk. Nyumba moja ni kwa ajili ya familia moja, sio kwa ajili ya mtu mmoja
Mtu mmoja anahitaji chumba, sio nyumba.
huna akili timamu

tunasemea watu wazima wenye miaka kuanzia 18 ndio wanastahili kumiliki nyumba

chini ya miaka 18 hao ni wategemezi hawana input yeyote kwenye uchumi ni kama zero members

na wanaozidi miaka 70 au 80 nao ni zero members kwenye uchumi ni wategemezi

fact is,haiwezekani

watu wazima wanaozalisha tanzania ni less than 17mil....hao wote hawawezi miliki nyumba na haitakiwi

wote wakimiliki nyumba then nani afanye kazi za kiuchumi kama kuchimba mitaro,kufanya operation hospitali,kulima shambani,etc?

Hii milioni 17mil wote wakimiliki nyumba kila mmoja uchumi unaanguka siku hiyo hiyo maana hakuna mtu ataenda kazini tena

Pili ujenzi wa nyumba kama huu unafanyika maeneo ya mjini (urban areas) ambayo kwa Tanzania ni only 35% of the population ndio wanaishi kwenye urban areas. The rest 65% hawahusiki kwenye miradi ya namna hii
yaani wanaokaa mijini tu ndio wanadamu wa nchi hii wanaokaa vijijini ambao ndio wanajenga GDP ya nchi hii kwa 75% wao ni mbwa waishi kwenye mapango?

Una akili timamu wewe?
Tatu, sijasema wananchi wapewe nyumba bure. Nimesema walipe kodi ya bei rafiki ambazo zipo ndani ya uwezo wa Watanzania wengi. Ukisema wananchi wapewe nyumba bure hayo ni maneno yako mwenyewe
Nyumba inanunuliwa kwa kulipa kodi?

Unaumwa ndugu?

Nyumba inanunuliwa kwa kulipa morgage kila mwezi kutokana na production yako kazini

kama hufanyi kazi au production yako ni ndogo relatively na bei ya nyumba basi itabidi usimiliki nyumba upange....na kupanga ni vizuri maana ina force people to do real hard jobs to earn that house morgage,otherwise kuna kazi zitakua hazina watu

Eti kodi unazolipa serikalini ndio zikulipie nyumba?

Kazi la malazi,kula na kupumua ni kazi ya mwananchi sio kazi ya serikali

Serikali ni kutoa ulinzi na kusimamia sheria ili kuwe na fair play kwa kila mtu

Kodi tunazolipa hazitoshi kufanya upumbavu huo.....

Leo utasema serikali ikupe malazi...kesho utasema serikali ikupe chakula....keshokutwa utasema ikupe elimu bure.....mbele yake useme serikali ikupe matibabu bure...then baadae useme serikali ikusaidie kupumua

Haiwezekani kwa kodi inayotoka per individual
Nne umesahau kuwa katika hao 35% wanaoishi mjini sio kila mtu ana nyumba mbaya au anakaa uswazi. Ni kama ume assume Tanzania nzima wana nyumba mbaya kwa hiyo nasema serikali iwajengee which is big NO. Kuna watu wengi wana nyumba nzuri au za kati which is fine
mkuu naona upo kwenye abstract sana

kazi ya kupangilia ardhi ni ya serikali....kupangilia majengo juu yake ni kazi ya aliepewa ardhi

kujenga nyumba zipendeze unavyotaka wewe sio kazi ya serikali ni kazi ya kampuni binafsi za real estate sio serikali

Serikali nyumba zake ni weak na bad designed and built....urembo unaotaka wewe ni private sector jobs

Kuwekeza na kuhakikisha miradi ya nyumba inakua na value of money ni private sector sio serikali

serikali ipasue viwanja na kusema vividly vipande hivi vitumike kwa ajili ya nini na nini...kununua cement na kujenga na kuuza nyumba is privage sector job

Slums zimekuja kwa serikali kutokupima maeneo na kuya define yatumike kwa ajili ya nini....wananchi wanakua kila siku wanavamia hayo maeneo waishi hawawezi ishi hewani

Wewe una malaria kudhani unaweza kumpa Serikali kazi ya kuremba miji kwa kupangilia wakati yeye Serikali ndio sababu ya Slums kutokea in the first place?

Kila mwananchi anunue au kujenga nyumba kwa kadiri ya uwezo wake...hakuna nyumba ya bure unavyotaka kufanya hapa

Eti zilipiwe kwa kodi,hizo kodi katoa nani?...Kama ni mlipa kodi binafsi kodi yake binafsi ndio itumike kulipia hiyo nyumba then itamchukua miaka 120 kukamilisha hilo deni....mkopeshaji gani duniani hapa anatoa mkopo wa nyumba wa kulipia miaka 120?

Vichaa wakubwa kabisa nyie
 
huna akili timamu

tunasemea watu wazima wenye miaka kuanzia 18 ndio wanastahili kumiliki nyumba

chini ya miaka 18 hao ni wategemezi hawana input yeyote kwenye uchumi ni kama zero members

na wanaozidi miaka 70 au 80 nao ni zero members kwenye uchumi ni wategemezi

fact is,haiwezekani

watu wazima wanaozalisha tanzania ni less than 17mil....hao wote hawawezi miliki nyumba na haitakiwi

wote wakimiliki nyumba then nani afanye kazi za kiuchumi kama kuchimba mitaro,kufanya operation hospitali,kulima shambani,etc?

Hii milioni 17mil wote wakimiliki nyumba kila mmoja uchumi unaanguka siku hiyo hiyo maana hakuna mtu ataenda kazini tena

yaani wanaokaa mijini tu ndio wanadamu wa nchi hii wanaokaa vijijini ambao ndio wanajenga GDP ya nchi hii kwa 75% wao ni mbwa waishi kwenye mapango?

Una akili timamu wewe?

Nyumba inanunuliwa kwa kulipa kodi?

Unaumwa ndugu?

Nyumba inanunuliwa kwa kulipa morgage kila mwezi kutokana na production yako kazini

kama hufanyi kazi au production yako ni ndogo relatively na bei ya nyumba basi itabidi usimiliki nyumba upange....na kupanga ni vizuri maana ina force people to do real hard jobs to earn that house morgage,otherwise kuna kazi zitakua hazina watu

Eti kodi unazolipa serikalini ndio zikulipie nyumba?

Kazi la malazi,kula na kupumua ni kazi ya mwananchi sio kazi ya serikali

Serikali ni kutoa ulinzi na kusimamia sheria ili kuwe na fair play kwa kila mtu

Kodi tunazolipa hazitoshi kufanya upumbavu huo.....

Leo utasema serikali ikupe malazi...kesho utasema serikali ikupe chakula....keshokutwa utasema ikupe elimu bure.....mbele yake useme serikali ikupe matibabu bure...then baadae useme serikali ikusaidie kupumua

Haiwezekani kwa kodi inayotoka per individual

mkuu naona upo kwenye abstract sana

kazi ya kupangilia ardhi ni ya serikali....kupangilia majengo juu yake ni kazi ya aliepewa ardhi

kujenga nyumba zipendeze unavyotaka wewe sio kazi ya serikali ni kazi ya kampuni binafsi za real estate sio serikali

Serikali nyumba zake ni weak na bad designed and built....urembo unaotaka wewe ni private sector jobs

Kuwekeza na kuhakikisha miradi ya nyumba inakua na value of money ni private sector sio serikali

serikali ipasue viwanja na kusema vividly vipande hivi vitumike kwa ajili ya nini na nini...kununua cement na kujenga na kuuza nyumba is privage sector job

Slums zimekuja kwa serikali kutokupima maeneo na kuya define yatumike kwa ajili ya nini....wananchi wanakua kila siku wanavamia hayo maeneo waishi hawawezi ishi hewani

Wewe una malaria kudhani unaweza kumpa Serikali kazi ya kuremba miji kwa kupangilia wakati yeye Serikali ndio sababu ya Slums kutokea in the first place?

Kila mwananchi anunue au kujenga nyumba kwa kadiri ya uwezo wake...hakuna nyumba ya bure unavyotaka kufanya hapa

Eti zilipiwe kwa kodi,hizo kodi katoa nani?...Kama ni mlipa kodi binafsi kodi yake binafsi ndio itumike kulipia hiyo nyumba then itamchukua miaka 120 kukamilisha hilo deni....mkopeshaji gani duniani hapa anatoa mkopo wa nyumba wa kulipia miaka 120?

Vichaa wakubwa kabisa nyie
Kwa hiyo unaona ukiniambia sina akili timamu na kuniita kichaa ndio itasaidia nisikosoe mawazo yako?
 
Magomeni Kota walipewa waliokuwa wakiishi zamani
Wamegoma lipia usafi, ulinzi, maji

Tatizo la Watz ni wanatukuza na kuona ufahari kuwa masikini
 
Nazisikitia zile Apartments za Mikwambe, Temeke Mbagala, mgeni nani:
Gholofa zinachakaa tu na hazina watu wa kuishi:
Ni Bora basi hata wangewapa Askari wale fresh from college ili waishi hapo, kuliko kuziacha zikaliwe na popo tu:
Ujumbe uwafikie wahusika
 
Idea yako nzuri,
labda mbadilishane na wazungu yani waafrica wote muende mabara mengine na Africa waje wazungu ndio kitu ya namna hio inaweza kutokea
Then after 5 years,Africa itakuwa nzuri na iliyoendelea kuliko Europe, na Europe itakuwa imejaa wezi na mitaro michafu
 
Back
Top Bottom