Kwanini Watanzania tusianze massive constructions of apartments nchi nzima?

Kwanini Watanzania tusianze massive constructions of apartments nchi nzima?

Kwa hiyo unaona ukiniambia sina akili timamu na kuniita kichaa ndio itasaidia nisikosoe mawazo yako?
mawazo yako ndio very very flawed

china imejengwa kwa makampuni binafsi kama evergreen wajenge majumba na kuuza commercially

hakuna mahali serikali ya china imejengea wananchi majumba bure

USA yote inamejengwa na private real estate companies kwa kukopeshwa na mabenki,sio serikali

Singapore the same

kukaa hapa na kuiingiza serikali kwenye biashara ya real estate ni ukichaa

kibaya zaidi unataja kodi,kodi inayokusanya serikali ijengeshe majumba wapewe watu,unajua bei ya kujenga nyumba kwanza?serikali hata ikusanye kodi zote dunia nzima haiwezi jenga hizo nyumba ni too expensive mara 50 ya GDP nzima...

Maana yake ni mapato ghafi ya nchi nzima kwa miaka 50 yasifanye chochote yajengee majumba ya kenge kama wewe kukaa ambae unatumia miaka 120-150 kufanya marejesho

Stupidity unaongea hapa

Kila kizazi wenye uwezo wajenge kwa nguvu zao as years go along....huwezi force malazi kama present consumption ya population yote ya wajenga uchumi 17mil waliopo

Ukitoka nyumba...utataka chakula..ukitoka chakula utata matibabu...ukitoka matibabu utataka elimu.....etc etc..na vyote utadai ni "haki za binadamu"....utadai ni "kodi zetu"

Mwenye nguvu na kipato cha kujenga ajenge,asie na kipato au nguvu za kujenga alale nje afanye kazi mpaka aweze kujenga hapo thamani ya real estate na scarcity ndio italeta maana

otherwise kila mtu atalala kwenye nyumba yake hakuna kwenda kazini tena..atalima bustani nje awe anachuma mboga hakuna kufanya kazi tena maana hakuna kitu kinachofanya enforcement ya yeye kwenda kufanya kazi ngumu ili apate malazi au ugali ili uchumi uende

Yes natukana ndio
 
Ukitaka video za dark side hata za China au USA utapata. Mimi sisemi Traore ni perfect lakini kama wao wameweza kuwa na kiwanda cha magari badi hata sisi tunaweza
Kuhusu apartments hata sio lazima nitolee mfano Burkina Faso, hata Kenya tu hapo wanajenga kwenye slums zao
Hiyo video siyo dark side. Ni street vlogging

Hakuna kiwanda cha magari BF. Hiyi source umeweka hapo ni blog ya mtu tu, anatafuta traffic
 
Progress nzuri, ingawa naona CGTN labda kuna wachina na sijaona assembling plant.
Assembling plant ipo na moja ya model wanazotengeneza ni ITAOUA SAHEL
Ongawa yeah, inawezekana wafanyakazi wengi ni wachina
 
Nazisikitia zile Apartments za Mikwambe, Temeke Mbagala, mgeni nani:
Gholofa zinachakaa tu na hazina watu wa kuishi:
Ni Bora basi hata wangewapa Askari wale fresh from college ili waishi hapo, kuliko kuziacha zikaliwe na popo tu:
Ujumbe uwafikie wahusika
Hawajali kwasababu lengo lao kwenye ujenzi huo ni 10% sio kutatua tatizo la maka,I duni. Ndio maana wanajenga sehemu za ajabu na kuweka bei za ajabu.
 
Hili mtaliweza vipi kama kila mtu anataka kuiba??

Nimemsikia mtu mmoja majuzi anaomba vijana waje na mkakati wa kupunguza foleni , unaweza kudhani tupo 1961 sasa ndio nchi imepata uhuru haina wataalam hivyo wanahitajika watu wa kujitolea kuanza kuisukuma nchi mbele .

Si mnaona uwanja wa taifa ulivyogeuka mradi wa vibaka kuchota pesa, wakijisikia tu wanaufunga na kusema wanafanya marekebisho.
 
Kusema ukweli Tanzania tunahitaji apartments kwa sasa. Kwa nini tusijifunze kutoka kwa nchi kama China, South Korea, Singapore nk? Hizi nchi watu wake walikuwa wanaishi kwenye makazi duni sana miaka ya 1960s. Serikali zao zikaanza ujenzi wa apartments ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata kuishi kwenye makazi bora. Na leo hii wamefanikiwa, watu wanaishi kwenye makazi mazuri
Nasema hivi kwa sababu clearly hii ya kila mtu kujenga nyumba yake mwenyewe imetushinda. Watu wasijenge nyumba mpaka wajipate, kipindi wanajitafuta wakae kwenye apartments za serikali au kampuni binafsi
NHC wanajenga apartments Dodoma na hata Dar tumeona miradi kama Kawe 711 na Samia Housing Scheme lakini kusema ukweli hii hata haitasaidia kitu. Nyumba za NHC huwa ni expensive ndio maana wanaishia kukaa wahindi na waarabu. Inapaswa zijengwe apartments na bei ziwe rafiki kwa Watanzania wa kawaida ili kupunguza makazi holela, sio hizi za NHC ambazo bei zake Wana afford foreigners tu. Na hata Watanzania wanao afford ni mara kumi wajenge nyumba zao wenyewe maana watapata nyumba nzuri zaidi

Take a look at this

Hapa ni Mbeya
View attachment 3544366
Umeona jinsi nyumba zilivyojengwa bila mpangilio na kuchukua ardhi kubwa bila sababu za msingi? Lakini kama zingejengwa apartment kadhaa, zikapandwa nyasi, miti, mitaro na sewage system mazingira yangekuwa mazuri zaidi ya hivi. Matatizo kama mafuriko, kipindupindu, maeneo kutofikika nk yangepungua na mji ungependeza kimuonekano

Hapa ni Dar
View attachment 3544367
Angalia hicho kipande kidogo kilichojengwa hovyo bila mpangilio
Na hapa pia ni Dar 👇
View attachment 3544369
.
.

Hapa ni MwanzaView attachment 3544368
Hawa watu wote wanaoishi kwenye nyumba zinazoonekana kwenye picha wangetosha kama wangekaa kwenye apartment moja pekee.

Kuzuia mambo kama haya ndio maana Wachina waliamua kujenga apartments nyingi nchi nzima

KWA NINI WACHINA WALIAMUA KUJENGA APARTMENTS NYINGI NCHI NZIMA?

Hapa sababu zote zipo applicable hata hapa Tanzania

1. Ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na mijini
China ina miji mikubwa yenye watu wengi. Kwa sababu ya uhamiaji mkubwa kutoka vijijini kwenda mijini (urbanization), kuna hitaji kubwa la makazi. Apartments ni suluhisho linaloweza kuchukua watu wengi katika eneo dogo. Ni kama tu hapa Tanzania (Jiji la Dar lina watu takribani milioni 5.3, Jiji la Mwanza watu milioni 1, majiji ya Arusha, Dodoma na Mbeya yana watu takribani laki 6 each)

2. Ufanisi wa ardhi na rasilimali
Ardhi mjini ni ya thamani kubwa. Kujenga nyumba za ghorofa nyingi (high-rise apartments) kunaruhusu kutumia ardhi kidogo lakini kufikia idadi kubwa ya familia.

3. Kurekebisha gharama za makazi
Apartments nyingi kwa mpango mmoja (mass housing) zinafanya gharama ya kila nyumba kuwa nafuu zaidi kuliko kujenga nyumba binafsi. Serikali pia inaweza kudhibiti bei za nyumba kwa urahisi zaidi.
View attachment 3544376
4. Kurahisisha huduma za kijamii
Wakati watu wengi wakiishi karibu kwenye buildings za makazi, ni rahisi kutoa huduma kama barabara, maji, umeme, shule, hospitali, na usafishaji wa miji.


FAIDA ZA SERIKALI KUJENGA APARTMENT NYINGI TANZANIA NZIMA
1. Bei nafuu kwa wananchi wa kawaida: Serikali inasaidia baadhi ya gharama, hivyo ni rahisi kwa watu wenye kipato cha kati au kidogo. Kuliko kujichanga na kujenga nyumba ambazo ni below standard ni heri mwananchi apange kwenye apartment za bei nafuu

2. Mpango wa usafi na afya
Miji mipya inafanyiwa urban planning, hivyo barabara, mifereji ya maji, na taka zinapangwa vizuri. Kuliko mazingira ya uswazi. Mpangilio mbovu una attract uchafu, watu wanatupa taka hovyo na hawaoni aibu kwa sababu mazingira yenyewe hayavutii. Hii ni human psychology (Broken window theory)
View attachment 3544375
3. Usalama
Blocks za apartments mara nyingi zina milango ya kudhibiti, CCTV, na wakaguzi wa usalama. Ukiangalia nchi zote ambazo wananchi wake wanaishi sana kwenye apartment ndio zinaongoza kwa usalama duniani (China, South Korea, Japan, Singapore)
View attachment 3544377
4. Huduma zinakuwa karibu
Shule, maduka, vituo vya afya na maegesho ya umma mara nyingi vipo ndani ya maeneo hayo.

MUUNDO NA MPANGILIO WA MITAA YA APARTMENTS KWA AJILI YA WANANCHI CHINA (Chinese residential neighborhoods)
View attachment 3544372
1. Apartments zinaunganishwa na barabara pana za magari na njia za watembea kwa miguu.

2. Zinajengewa bustani ndogo, miti, na maeneo ya michezo kwa watoto.

3. Urban planning
Kila block ina eneo lake la park, shule, soko, frame za maduka ya msingi karibu nk
View attachment 3544373
4. Mfumo wa maji na umeme umewekwa ili kuepuka matatizo ya usafi na msongamano.

5. Kunakuwa na njia za baiskeli na barabara za watembea kwa miguu

Kwa sababu ni housing mass-production, bei inabakia chini kuliko nyumba binafsi.
Apartments ndogo zina bei nafuu zaidi, zinazofaa kwa vijana, wafanyakazi wa maofisini, familia zinazojitafuta, na hata zilizojipata

View attachment 3544374
Mitaa ya apartments inavyokuwa, unaweza kukuta residential compounds yenye ghorofa 10–30.
Kila block ina green space: miti midogo, bustani za michezo, na sehemu za kukaa.
Njia za barabara haziwezi kuwa na msongamano mkubwa kwa sababu zoning imepangwa vizuri: makazi, biashara, na huduma za jamii hazichanganyiki bila mpangilio.
View attachment 3544378View attachment 3544379
Hizi apartments ndio zimesaidia China kutokuwa na mitaa ya hovyo kama ya hapa kwetu Tanzania. Apartments ni better option ya makazi
Fikiria nchi kama USA Ina uchumi mkubwa kuliko China na Ina watu wachache kuliko China (China Ina watu bilioni 1.4, USA Ina watu milioni 350) lakini USA ina homeless people wengi kuliko China. That means Chinese way is more effective
Hapa Tanzania nako homeless sio wengi lakini sasa watu wanakaa kwenye makazi dunia. Ni muda sasa tuanze kujenga apartments nyingi kila kona ya Tanzania ili watu wakae kwenye nyumba nzuri. Kodi ziwe chini na sisi nchi yetu ipendeze, tupunguze urban sprawl, na matumizi ya ardhi yasiyo ya lazima.
NHC waache kujengea nyumba wahindi na waarabu, waweke bei rafiki ili Watanzania waone sababu za kuhamia kwenye apartments.
Wala sio lazima ziwe apartments ndefu kama za China. Huku hata zikijengwa za urefu wa 5 floors each inatosha
Maana hii hali sio nzuri 👇View attachment 3544369
Ni wazo zuri ila shida inakuja kwenye uongozi kila unaoingia unakuja na miradi yake mipya sijui nchi haina mikakati yake ya kipaumbele
 
Heko mwenzetu ulipatwa maokoto yatokanayo kumsifia mama wakati wakati wa kampeni.
 
Back
Top Bottom