Kwanza nani kasema China ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi.Muongo huyo China 1980 haikua sawa na Tanzania kiuchumi. China ilikua top 10 duniani kwa uchumi mkubwa
Uchumi unapimwa kaa per capita tu?Unaelewa maana ya per capita income?
Nimekuuliza hapo uchumi unapimwa kwa per capita tu? Wanaojenga hiyo miradi ni serikali, niambie kwa uchumi huu wa nusu kulipa deni nusu kulipa mishahara wapi watapata pesa za kujenga kama China?Kwanza nani kasema China ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi.
Mwenzako kaongelea per capita income kasema pato la Mtanzania kwa mwaka ni 2.5 million Tsh, yani unafananisha mapato vs population. China leo hii ni ya pili kwa uchumi mkubwa duniani lakini inazidiwa per capita income na nchi nyingi duniani.
Miaka ya 1980s China ilikuwa na per capita income ya $195, wananchi wengi walikuwa hawajiwezi
Mfano rahisi, unajua kuwa India ipo top 5 nchi zenye uchumi mkubwa duniani lakini wananchi wake wengi ni masikini wa kutupwa?
Vitu vingine kama vipo nje ya uwezo wako sio lazima uchangie. Huelewi vitu tunavyoongea halafu unatumia lugha kali ni kama uko na anger issues ndio maana nilikuwa najaribu kuignore comment zako
🤣Idea yako nzuri,
labda mbadilishane na wazungu yani waafrica wote muende mabara mengine na Africa waje wazungu ndio kitu ya namna hio inaweza kutokea
Kuna vitu unachanganya. China ilikuwa na $300B economy huo mwaka 1980 lakini at the same time ilikuwa na wananchi milioni 900+ meaning ilikuwa na watu wengi sana wa kuwahudumia lakini bado walihangaika kusaidi population yao mdogomdogo hadi leo wamefanikiwa kugusa population kubwaUchumi unapimwa kaa per capita tu?
China ya 1980 ambayo ilikua na gdp ya $300 billion ukafananishe na Tanzania ambayo hata sasa haijafika hata $100billion
In short unauliza Tanzania yenye $95B na wananchi 65M+ itapata wapi pesa za kujenga kama China yenye $300B ilivyowajengea wananchi milioni 900+???Nimekuuliza hapo uchumi unapimwa kwa per capita tu? Wanaojenga hiyo miradi ni serikali, niambie kwa uchumi huu wa nusu kulipa deni nusu kulipa mishahara wapi watapata pesa za kujenga kama China?
Hakika mkuu, ujenzi wa makazi ya watu wengi kwa eneo dogo ndio unafaa kwa dunia ya sasa. Dogo alikuwa sahihi na ni great thinker, kwa sasa miji yetu ipo kwenye rapid urbanisation and we have to do something now maana tukiendelea hivi hadi miaka 30 ijayo hali itakuwa mbayaTuko wengi mkuu wenye mawazo kama Yako.
Juzi kati Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi, mtoto mdogo kabisa (Yuko darasa la nne au Tano ) akamuuliza baba yake "Baba Kila sehemu mnajenga nyumba, kwanini usijenge nyumba kuuubwa Ili watu wote waje wakae humo?
Unajaribu kufananisha Mchina na Mtanzania kweli ?Hadi kufikia 1980 China ilikuwa na umasikini wa kutupwa na per capita income ndogo kuliko hata ya Tanzania leo hii. Mwaka 1980 China ilikuwa na per capita income ya $195 na wananchi wake walikuwa ni masikini waliokubuhu
Lakini hapohapo 1980 China iliamua kujivuta kufanya miradi yote kupunguza umasikini na kujenga apartments
Walianzisha viwanda vingi, mashamba makubwa, wakaboresha elimu ya ufundi walifanya vitu vingi vya kupunguza umasikini at the same time wakaanza kuwajengea wananchi apartments licha ya uchumi mdogo. Miaka 40 imepita sasa, nchi yao ina makazi bora
Hawakusubiria wawe matajiri kwanza ndio wajenge, bali walianza kujenga makazi tangu wananchi wakiwa hawajiwezi
Wewe umeassume kwamba eti nataka Tanzania iache shughuli zote ianze kujenga apartment tena zote ziwe zimekamilika in 5 years kwa kila Mtanzania, kitu ambacho ni wrong
Ujenzi wa apartments haufanyiki overnight, ni kwamba kila mwaka budget inatengwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi, kila mwaka unavyopinduka apartments zinaongezeka. Mpaka miaka 20 inakuja kupita makazi holela yanapungua kwa asilimia kubwa sana. China ndio walifanya hivyo. Hawakusubiria per capita yao ifike hadi $10000 ndio waanze kujenga.
Nonsense,hii haihitaji VyamaTuwekeze kwenye kuitoa ccm madarakani kwanza
Mkuu umesoma uchumi ?Kuna vitu unachanganya. China ilikuwa na $300B economy huo mwaka 1980 lakini at the same time ilikuwa na wananchi milioni 900+ meaning ilikuwa na watu wengi sana wa kuwahudumia lakini bado walihangaika kusaidi population yao mdogomdogo hadi leo wamefanikiwa kugusa population kubwa
Tanzania ina $95B economy, na wananchi takribani 65M+ kwa hiyo uchumi wa Tanzania unatosha kabisa kuanza project za makazi sasahivi kama China ilivyoanza miaka ya 1980 kwa 300B huku wana watu milioni 900+ wa kuwahudumia
View attachment 3544493View attachment 3544494
Nchi haina Rais ina kiazi, unategemea nini?Kusema ukweli Tanzania tunahitaji apartments kwa sasa. Kwa nini tusijifunze kutoka kwa nchi kama China, South Korea, Singapore nk? Hizi nchi watu wake walikuwa wanaishi kwenye makazi duni sana miaka ya 1960s. Serikali zao zikaanza ujenzi wa apartments ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata kuishi kwenye makazi bora. Na leo hii wamefanikiwa, watu wanaishi kwenye makazi mazuri
Nasema hivi kwa sababu clearly hii ya kila mtu kujenga nyumba yake mwenyewe imetushinda. Watu wasijenge nyumba mpaka wajipate, kipindi wanajitafuta wakae kwenye apartments za serikali au kampuni binafsi
NHC wanajenga apartments Dodoma na hata Dar tumeona miradi kama Kawe 711 na Samia Housing Scheme lakini kusema ukweli hii hata haitasaidia kitu. Nyumba za NHC huwa ni expensive ndio maana wanaishia kukaa wahindi na waarabu. Inapaswa zijengwe apartments na bei ziwe rafiki kwa Watanzania wa kawaida ili kupunguza makazi holela, sio hizi za NHC ambazo bei zake Wana afford foreigners tu. Na hata Watanzania wanao afford ni mara kumi wajenge nyumba zao wenyewe maana watapata nyumba nzuri zaidi
Take a look at this
Hapa ni Mbeya
View attachment 3544366
Umeona jinsi nyumba zilivyojengwa bila mpangilio na kuchukua ardhi kubwa bila sababu za msingi? Lakini kama zingejengwa apartment kadhaa, zikapandwa nyasi, miti, mitaro na sewage system mazingira yangekuwa mazuri zaidi ya hivi. Matatizo kama mafuriko, kipindupindu, maeneo kutofikika nk yangepungua na mji ungependeza kimuonekano
Hapa ni Dar
View attachment 3544367
Angalia hicho kipande kidogo kilichojengwa hovyo bila mpangilio
Na hapa pia ni Dar 👇
View attachment 3544369
.
.
Hapa ni MwanzaView attachment 3544368
Hawa watu wote wanaoishi kwenye nyumba zinazoonekana kwenye picha wangetosha kama wangekaa kwenye apartment moja pekee.
Kuzuia mambo kama haya ndio maana Wachina waliamua kujenga apartments nyingi nchi nzima
KWA NINI WACHINA WALIAMUA KUJENGA APARTMENTS NYINGI NCHI NZIMA?
Hapa sababu zote zipo applicable hata hapa Tanzania
1. Ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na mijini
China ina miji mikubwa yenye watu wengi. Kwa sababu ya uhamiaji mkubwa kutoka vijijini kwenda mijini (urbanization), kuna hitaji kubwa la makazi. Apartments ni suluhisho linaloweza kuchukua watu wengi katika eneo dogo. Ni kama tu hapa Tanzania (Jiji la Dar lina watu takribani milioni 5.3, Jiji la Mwanza watu milioni 1, majiji ya Arusha, Dodoma na Mbeya yana watu takribani laki 6 each)
2. Ufanisi wa ardhi na rasilimali
Ardhi mjini ni ya thamani kubwa. Kujenga nyumba za ghorofa nyingi (high-rise apartments) kunaruhusu kutumia ardhi kidogo lakini kufikia idadi kubwa ya familia.
3. Kurekebisha gharama za makazi
Apartments nyingi kwa mpango mmoja (mass housing) zinafanya gharama ya kila nyumba kuwa nafuu zaidi kuliko kujenga nyumba binafsi. Serikali pia inaweza kudhibiti bei za nyumba kwa urahisi zaidi.
View attachment 3544376
4. Kurahisisha huduma za kijamii
Wakati watu wengi wakiishi karibu kwenye buildings za makazi, ni rahisi kutoa huduma kama barabara, maji, umeme, shule, hospitali, na usafishaji wa miji.
FAIDA ZA SERIKALI KUJENGA APARTMENT NYINGI TANZANIA NZIMA
1. Bei nafuu kwa wananchi wa kawaida: Serikali inasaidia baadhi ya gharama, hivyo ni rahisi kwa watu wenye kipato cha kati au kidogo. Kuliko kujichanga na kujenga nyumba ambazo ni below standard ni heri mwananchi apange kwenye apartment za bei nafuu
2. Mpango wa usafi na afya
Miji mipya inafanyiwa urban planning, hivyo barabara, mifereji ya maji, na taka zinapangwa vizuri. Kuliko mazingira ya uswazi. Mpangilio mbovu una attract uchafu, watu wanatupa taka hovyo na hawaoni aibu kwa sababu mazingira yenyewe hayavutii. Hii ni human psychology (Broken window theory)
View attachment 3544375
3. Usalama
Blocks za apartments mara nyingi zina milango ya kudhibiti, CCTV, na wakaguzi wa usalama. Ukiangalia nchi zote ambazo wananchi wake wanaishi sana kwenye apartment ndio zinaongoza kwa usalama duniani (China, South Korea, Japan, Singapore)
View attachment 3544377
4. Huduma zinakuwa karibu
Shule, maduka, vituo vya afya na maegesho ya umma mara nyingi vipo ndani ya maeneo hayo.
MUUNDO NA MPANGILIO WA MITAA YA APARTMENTS KWA AJILI YA WANANCHI CHINA (Chinese residential neighborhoods)
View attachment 3544372
1. Apartments zinaunganishwa na barabara pana za magari na njia za watembea kwa miguu.
2. Zinajengewa bustani ndogo, miti, na maeneo ya michezo kwa watoto.
3. Urban planning
Kila block ina eneo lake la park, shule, soko, frame za maduka ya msingi karibu nk
View attachment 3544373
4. Mfumo wa maji na umeme umewekwa ili kuepuka matatizo ya usafi na msongamano.
5. Kunakuwa na njia za baiskeli na barabara za watembea kwa miguu
Kwa sababu ni housing mass-production, bei inabakia chini kuliko nyumba binafsi.
Apartments ndogo zina bei nafuu zaidi, zinazofaa kwa vijana, wafanyakazi wa maofisini, familia zinazojitafuta, na hata zilizojipata
View attachment 3544374
Mitaa ya apartments inavyokuwa, unaweza kukuta residential compounds yenye ghorofa 10–30.
Kila block ina green space: miti midogo, bustani za michezo, na sehemu za kukaa.
Njia za barabara haziwezi kuwa na msongamano mkubwa kwa sababu zoning imepangwa vizuri: makazi, biashara, na huduma za jamii hazichanganyiki bila mpangilio.
View attachment 3544378View attachment 3544379
Hizi apartments ndio zimesaidia China kutokuwa na mitaa ya hovyo kama ya hapa kwetu Tanzania. Apartments ni better option ya makazi
Fikiria nchi kama USA Ina uchumi mkubwa kuliko China na Ina watu wachache kuliko China (China Ina watu bilioni 1.4, USA Ina watu milioni 350) lakini USA ina homeless people wengi kuliko China. That means Chinese way is more effective
Hapa Tanzania nako homeless sio wengi lakini sasa watu wanakaa kwenye makazi dunia. Ni muda sasa tuanze kujenga apartments nyingi kila kona ya Tanzania ili watu wakae kwenye nyumba nzuri. Kodi ziwe chini na sisi nchi yetu ipendeze, tupunguze urban sprawl, na matumizi ya ardhi yasiyo ya lazima.
NHC waache kujengea nyumba wahindi na waarabu, waweke bei rafiki ili Watanzania waone sababu za kuhamia kwenye apartments.
Wala sio lazima ziwe apartments ndefu kama za China. Huku hata zikijengwa za urefu wa 5 floors each inatosha
Maana hii hali sio nzuri 👇View attachment 3544369
CCM sio CCP kwamba itajifanyia reforms na kubadilisha hali za wachina.Nonsense,hii haihitaji Vyama
Ni lazima tuitoe ccm madarakani kwanza hili halihitaji kejeli wala mjadala..Nonsense,hii haihitaji Vyama
Urban spraw kwenye well organized plots sio shida na inaweza kuhimilika kuliko squatters.Tatizo ni urban sprawl. Africa miji yetu Ina sprawl sana which is bad for the next 50 years
Miji kama Los Angeles, Atlas au Philadelphia USA sasahivi wanajuta kwa namna miji hiyo ilivyopanuka (extreme urban sprawl). Miji mizuri ni kama ile inavyojengwa Ulaya.
Au China. China miji yao imepanuka sawa lakini unakuta mji una ukubwa sawa na Los Angeles lakini una watu milioni 20 wakati Los Angeles Ina watu milioni 3. Maana yake for the same size, China inaweza kuhudumia watu wengi zaidi, something which is better for environment
Urban sprawl sio nzuri na hapa Africa ndio itatushinda. Kadri kila new neighborhood inavyojengwa ndio jinsi serikali unapata shida kuanza kuwafikishia maji, umeme, shule, hospitali, barabara, mifereji nk hata uchafuzi wa mazingira unakuwa uncontrollable pia
Wakazi wote wanapaswa kuwa karibu na huduma za msingi which is why apartments ni more practical for long term use
"The Worst of All Worlds: Los Angeles, California, and the Emerging Rea" by Eric Eidlin The Worst of All Worlds: Los Angeles, California, and the Emerging Reality of Dense Sprawl
Sawa mtajua wenyewe kikubwa Mimi siwezi ishi kwenye apartment sijashindwa kujenga bangaloo langu.CCM sio CCP kwamba itajifanyia reforms na kubadilisha hali za wachina.
Endelea kusoma.Yes only in secondary school, ila higher learning institutions nimesomea vitu vingine, sio uchumi