Wakuu, tusiongopeane hapa badala yake tuwe wakweli toka moyoni.
Ukweli ni kwamba sikuzote mtaji wa ccm ni wakinamama wa uswazi au
sehemu yoyote yenye uswahili uswahili fulani hivi'na huko ndiko ccm
huwa wanagawa vitu vya bure vikiwemo khanga,tishirts nk.kisha utaona
nyomi ya kinamama kufa mtu....ukweli ni kwamba baadhi ya familia za uswazi
zinaangalia leo tu na si kesho....sasa tukianza kujiongopea hapa eti ooooh tusi
waige ccm basi CDM isahau kupata saport kutoka kwa wamama. Hivi nyie mme
wahi kuona ccm wanagawa kanga Masaki,Posta,Mikocheni,Ostebay na Mbezi?
hamjiulizi ni kwanini? kwavile wanajua kuwa wakinamama wa maeneo hayo wamesoma
na kuelimika na pia hawana shida ndogo ndogo. So ccm wanakimbilia uswazi kwa jamii
inayoangalia mlo wa leo na vazi la leo tu....na mwisho wanashinda. Jamani mazuri tuige?