Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Mar 11, 2012.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  WanaJF, Heshima mbele wakuu!.

  Hivi ni kwanini wanawake waliowengi wanaisaport Chadema kwa woga?

  Nilianza kufatilia kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,baadae ikaja ule uchaguzi mdogo wa Igunga na sasa ni huu wa Arumeru ulioanza kampeni zake jana.

  Katika mikutano yote ya kampeni za Chadema ni nadra sana kuona wanawake wamejitokeza kwa wingi....sana sana watakuwa wachache sana na wanahesabika.

  Tena kibaya zaidi wanakuwa hawana shamra shamra zozote za kuashiria kweli wao ni people's power mpaka kieleweke.

  Lakini ukifatilia kampeni na mikutano ya CCM na CUF utawaona wakinamama wamefurika kibao kupita maelezo! Yaani utaona wanakata viuno,wanaimba na kucheza huku wakishauti kwa kelele za kufa mtu. Jamani kwa nini isiwe hivyo na kwa Chadema?

  Kwa wale waliofuatilia ufunguzi wa kampeni za CDM jana kupitia StarTv live kutoka Arumeru watakubaliana na mimi kwa 100% yaani uwanja mzima ulifurika wanaume...wanawake walikuwa wachache sana! nakumbuka kuna mbunge mmoja mwanamke wa CDM
  alisimama na akauliza kwa masikitiko makubwa sana'kwanini wanawake hawajajitokeza kwa wingi kama wanaume?

  Wanabodi,
  Je, tatizo ni nini? Kwanini wanawake walio wengi hawaisapoti CDM? Na hao wachache wakijitokeza basi huwa kama wamenyeshewa na mvua.

  1. Je wanaiogopa serikali ya ccm? au
  2. Wamelishwa propaganda na CCM kuwa Chadema ni chama cha fujo?

  Na mwisho Je, kifanyike nini ili CDM nao kwenye mikutano yao iwe inapata wamama wa kutosha?
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  wanasubiria kupatiwa afueni toka kwa waume zao..
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We hujui tu Arusha wanawake wanaisapoti sana chadema kama huamini siku kukiwa na mkutano wa chadema Atown njoo.
   
 4. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu,kwahiyo wanawake wa Arusha wakiisaport CDM ndiyo kusema wanawake wa mikoa yote wanaisaport CDM?
  Je, wanawake wa Ilala na Temeke? vipi kuhusu wanawake wa Arumeru na Lindi?
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  cdm wamejaza vijana na kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba hawa vijana wa cdm ni wasumbufu sana kwa hawa dada zetu.
   
 6. dudupori

  dudupori JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mkuu mi nadhani wanawake walio wengi wanahadaika na vijikanga vya CCM, mnajua tena mwanamke na kanga, labla na CDM waige haka ka utaratibu ka kugawa kanga, leso tutawaona kwa wingi.
  Ni mawazo tu wadau.
   
 7. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  hoja yako ina mashiko..suluhu ya hili ni kwa viongozi wa CDM kulitazama hili kwa jicho la tatu..
  naweza kuifikiria sababu kuwa ni viongozi wa kike ndani ya CDM kutopewa nafasi ya kutosha kuzungumza na kushawishi...mfano mzuri ni jana katika uzinduzi wa kampeni kwa kweli alipaswa kusimama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa kwa kina mama ili basi waonapo wa kina mama na kuguswa na maongezi yake bila shaka watakuwa wanajitokeza kwa wingi..
  tunao watu wenye ushawishi mkubwa kama vile Halima Mdee huyu alizua gumzo kubwa katika mazishi ya marehemu Sumari pale ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa waliomtangulia kuingia msibani watu walikuwa kimya wakiwatizama alipoingia Mdee kelele zikaanza huku nyingi zikiwa za akina mama, huyu alipaswa kupewa muda mwingi wa kuzungumza kwa siku kama ya jana
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Albedo

  Mkuu, huwa naheshimu sana michango yako hapa jamvini....please tupia neno moja kwa hii mada.
  Je ni semalo ni kweli au ni uongo? na je ni nini kifanyike?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Unataka Niseme Nini?

  Wewe Umesema kuwa jana 100% (Yaani Hakukuwa na Mwanamke hata Mmoja) Walikuwa ni Wanaume Halafu Ukasema kwamba Wanawake walikuwa Wachache. Sasa sijui ni Mathematics za Sayari gani
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jibu ni rahisi sana, wanawake ni watu wa kususasusa ili wapewe attention, sasa wakiona na jinsia nyingine nayo ni hivyo hivyo "psychologically" wanaweka boundary ya kuwa huko hakuna wa kuwapa attention, wenyewe wanataka attention kwa mbinu zilezile.
   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sawa labda nilijichanganya jinsi ya kuidadavua....swali langu ni kwanini wanawake hawajitokezi kwa wingi kwenye
  mikutano ya CDM kama ilivyo kwa CCM na CUF?
   
 12. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wanawake asilimia kubwa wapo CCM. CCM imetia nguvu zake kubwa sana huko kama njia ya kuwa kamata kupitia Mtoto wao Chama cha wanawake. Kama ilivo wazi wapiga kura wengi ni wanawake. Haina mana CDM hawako. wapo ila bado ni wachache sio kiasi cha CDM kuweza jigamba.
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Vitu kama hivi ndio wanavyopenda wakina mama,si unajua wanapenda sana dezo.
   
 14. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii....sasa wewe unaona kifanyike nini ili na CDM nao wawe na wanawake wengi?ukizingatia kama ulivyosema kuwa wanawake ndiyo wapigakura wa uhakika?
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mshikachuma hoja yako ni nzuri,

  Siwadharau wanawake lakini ukweli ni kwamba wanawake wengi hasa wa kiafrika huhitaji faraja ya muda mfupi, huwa hawafikirii faraja ya muda mrefu. Na hii inatokana na mfumo dume, baba yuko kwa kutafuta na mama kutunza familia(daily activities). Kwa hiyo mama akipewa kanga au kilo ya chumvi anaona ahueni atapitisha siku mbili tatu bila kwenda kuomba kwa jirani wakati huo hatakuwa na mawazo kuwa chumvi itakwisha. Hapo ndipo CCM inapowapatia. Naweza kusema wanawake ni rahisi sana kudanganywa kuliko wanamme, kwa mambo mengi, hata kwenye masuala ya mapenzi atambiwa nitakununulia gari wakati anayemwambia hata baiskeli hana.

  Suala la kuhudhuria mikutano linaendana na hayo niliyoeleza, wanawake wanajiuliza je kuna nini kwenye mkutano, niende wakati hata chumvi ya mboga sina. Nikienda Chadema je wana sale za kanga- kama picha moja hapo juu. CCM na CUF wana vitu hivyo, CUF hasa upande wa Zanzibar wanawake huwa na sale yao hasa ya kanga tofauti na CDM. Nafikiri haya yanaweza kuwa sababu kwa nini wanawake hawahudhurii mikutano ya CDM. Labda cha kujiuliza je CDM nao waanze kutumia hii mbinu ya kuwa na sale sale kwa wanawake, faida na hasara zake ni zipi.
   
 16. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmh! nimecheka sina mbavu!!!!...any wayz acha nikujibu.
  Mkuu hili ni jina langu la ukweli kabisa.... i mean ni jina la ukoo wetu (jina la babu)
  Babu yangu alipigana vita ya majimaji kule Songeanna yeye kazi yake ilikuwa ni kubeba lichuma likubwa sana
  kwa hajili ya kunolea zana za kivita (za jadi) so makamanda wenzake walipenda kumuita Mshikachuma kutokana
  na kitengo chake....naitwa Najee Mshikachuma.
  :focus:
   
 17. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Mkuu Feedback,salute! imenidadavulia vizuri sana! Na hapo kwenye bold mimi nasema liwalo na liwe'binafsi napendekeza
  au ningeshauri uongozi wa CDM wangetengeneza khanga na tishirt kwa hajili ya wakina mama....kuliko kujifanya sizitaki mbichi hizi huku CCM wakichukua ushindi kupitia mbinu hizi
   
 18. Josephine

  Josephine Verified User

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Sipendi kupingana na wewe,kwani mashabiki ndio wenye macho.

  Tupe mda tulifanyie kazi.
   
 19. d

  davidfrance82 Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ni hivi CCM wanamtandao mpana sana kuanzia ngazi za chini kabisa kama kata NA kijiji....NA huku kote akina mama wanajishughulisha na shughuli mbalimbali kama vikoba nk,pia mashina mengi ya ccm yana shughuli flan ndogondogo kama shule za chekechea,parking za magari,maduka na bar,bila kusahau vijiwe vya kupiga soga
  so kimtazamo ccm toka zamani ilienvest kwenye jamii direct...that's y ni rahisi kuorganize akina mama kwenda kwenye kampeni wakiwa wamejipanga kwa nyimbo nk.
  Chadema mtandao wao ndio unakuwa sasa lakini kwa historia ni vijana sana tena wengi ni wenye elimu ya juu au kiasi ndio wamekuwa mstari WA mbele....
  itachukua muda na resources nyingi to build up ....Ila inawezekana
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  inategemea na mkoa au mji, kuna maeneo wanawake hawadanganyiki kirahisi
   
Loading...