Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

Sipendi kupingana na wewe,kwani mashabiki ndio wenye macho.

Tupe mda tulifanyie kazi.
Sawa mkuu,tumekuelewa....lakini wakati munasubili kulifanyia kazi, si vibaya na wewe ukatupia hisia zako binafsi
kuhusiana na hili swala. Je, wewe unaona tatizo ni nini? iweje CUF na CCM kwenye mikutano yao wapate wamama
wengi kuliko CDM? funguka mkuu....
 
Mmh! nimecheka sina mbavu!!!!...any wayz acha nikujibu.
Mkuu hili ni jina langu la ukweli kabisa.... i mean ni jina la ukoo wetu (jina la babu)
Babu yangu alipigana vita ya majimaji kule Songeanna yeye kazi yake ilikuwa ni kubeba lichuma likubwa sana
kwa hajili ya kunolea zana za kivita (za jadi) so makamanda wenzake walipenda kumuita Mshikachuma kutokana
na kitengo chake....naitwa Najee Mshikachuma.
:focus:

Mkuu Mshikachuma ni kweli kwamba Wanawake wengi huwa hawahudhurii Mikutano ya Vyama vya Upinzani ( Si Kwa Sababu hawavipendi la hasha). Na si kweli kwamba wanaume wote wanaohudhuria na kuviunga mkono vyama vya Upinzani hufanya hivyo kwa Uhuru na Bashasha.

1. Watanzania Kuunga Mkono Upinzani "Waziwazi"
Mkuu Tukirudi Nyuma miaka ya 1993 wakati Mfumo wa vyama vingi Watanzania ( hasa walioajiriwa katika sekta zilizo rasmi) wamekuwa waoga sana Kuviunga Mkono vyama Waziwazi. na hii ilitokana kwamba pamoja na kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama vingi bado CCM ilikuwa na Nguvu sana ndani ya serikali. Ni Miaka ya Karibuni tu ndio "Wameacha kutuuliza" Itikadi zetu katika Interview za Kazi. Kuna Miaka hata balozi wa Nyumba Kumi kumi alikuwa na Uwezo wa kukupigia Pande ukapata kazi Serikalini au Akakuunguzia Ukafukuzwa kazi Serikalini.

Mambo sasa yamebadilika watu wanathubutu kuonesha Itikadi zao waziwazi Bila Uoga lakini Bado Kuna Kundi Kubwa sana linahitaji Kukombolewa. Unaweza Ukafikiri ni Wanawake peke yao lakini nakuhakikishia bado kuna Watanzania wengi ni CDM kindakindaki lakini Zitto akisema Pipoooooooooooz, Wengi kabla yakitikia salamu wanaangalia Nani yuko Pembeni yao. Hiyo ndiyo hali halisi na si kwa wanawake peke yao.

2. Wanawake wengi (Hasa Watu Wazima na Wazee) bado wameathirika na Mfumo wa Chama kushika Hatamu. Na siwezi kuwalaumu hata kidogo kwa sababu wengi wanaregemea wapate Vijimikopo kutoka kwenye Vikundi vya akina Mama ambako UCCM ni Kigezo cha kupata Mikopo. Mama yangu ni CDM kindakindaki lakini huwa haudhurii mikutano ya CDM na anafanya hivyo ili asije akatengwa na "Walioshika Mpini". Hali ni Tofauti kwa akina Dada.

3. Mkuu kwa wamama wengi wenye kipato cha chini Upande wa Khanga ni wa Maana sana. Sasa hatuwezi kuishaauri CDM iige hayo hapana.

CDM badala ya kuwapa khanga, pilau, sukari na Chumvi ijikite katika kuwakomboa KIFIKRA. Mkuu Go back to 1993 it was not possible kuona hata wanaume wakiunga Mkono Upinzani kama wanavyofanya sasa. So Tuwatie Moyo akina Mama huku tukielewa kwamba Akina Sofia Simba wana wa MANIPULATE sana Mama zetu
 
Mkuu Feedback,salute! imenidadavulia vizuri sana! Na hapo kwenye bold mimi nasema liwalo na liwe'binafsi napendekeza
au ningeshauri uongozi wa CDM wangetengeneza khanga na tishirt kwa hajili ya wakina mama....kuliko kujifanya sizitaki mbichi hizi huku CCM wakichukua ushindi kupitia mbinu hizi
Hata mimi nilikuwa na mawazo hayo, CDM waache kujifanya wao hawawezi kuiga. Hii mbinu ni nzuri provided hawagawi bure wanauza afterall chama kitakuwa na double profit. Kitu kingine ninachokiona CDM wanamiss ni kutokuwa na wanawake wahamasishaji hasa u dormant wa BAWACHA nao unachangia, watafutwe wanawake hata watatu wawezeshwe (permanent job), kazi yao iwe kuzunguka mikoani na gari yao special ya matangazo lengo ni kuhamasisha wanawake na kuanzisha miradi ya kinamama na ku groom wahamasishaji wanawake wa level ya matawi na wilaya. Kwa mimi nionavyo sidhani kama Halima Mdee anafit kwa kazi hii.
 
[/B]
Mkuu Feedback,salute! imenidadavulia vizuri sana! Na hapo kwenye bold mimi nasema liwalo na liwe'binafsi napendekeza
au ningeshauri uongozi wa CDM wangetengeneza khanga na tishirt kwa hajili ya wakina mama....kuliko kujifanya sizitaki mbichi hizi huku CCM wakichukua ushindi kupitia mbinu hizi

Hapana Mkuu Hapo tutakuwa tunatengeneza Ukombozi wa Muda. We need Permanent Changes Mkuu. Na Permanent Changes inaanzia kwenye Watu WANAVYOFIKIRI.

CDM ikisema ichuke Ushauri wako itakuwa imeungana na CCM katika KUWATWEZA Mama na Dada zetu
 
Mkuu,kwa hapa ni BIG NO....yaani binafsi naona ni bora Chadema wakaiga hii kitu haraka wawezavyo. Hivi kuna ubaya
gani Chadema kutoa tenda ya kutengenezewa khanga na Tishirts na kuwauzia au kuwapa bure wakinamama kwa masirahi
ya chama? Kama alivyosema Feedback hapo juu....ni bora kuanzisha hili jambo kuliko kuuchelewesha ukombozi kwa madai
ya sizitaki mbichi hizi.
 
Mkuu kama CDM hakiwezi kufanya kitu Tofauti na CCM na kikafanikiwa basi hakina Haja ya Kukimbilia Ikulu. Naamini CDM kuna watu makini tunachoweza kushauri ni kuwakomboa akina Mama zetu VICHWANI kwanza. Yaani unataka akina Mama wapige huku na Kule? Yaani wapige Khanga za CCM na wapige Khanga za CDM? Kama alivyosema Mmoja wa Makada wa CDM Ben ni kwamba CDM inahitaji kujenga a Loyal Base na mimi nawaomba waanzie kwa akina Mama. CCM has a lot of Money Mkiamua Kuchagua Kupambana nao katia UTOAJI Pumzi itawaishia kabla ya 2015. Ninyi Mtato moja wao watatoa kwa Ukoo Mzima
 
Aldedo

Nakubaliana na wewe kuwa zamani ilikuwa vigumu sana kujiunga na vyama vya upinzani, lakini naona kadri siku zinavyokwenda watu hata serikali yenyewe inalazimika kuikubali hali halisi ya mabadiliko. Lakini sikubaliani na wewe kuwa kuiga mambo ya CCM hasa mazuri ni kuungana na CCM kuwatweza wanawake, hapana. Kuna mchangia amesema hata wewe umegusia CCM ili invest sana kwa wanawake kwa kuwaanzishia vikundi vidogo vidogo kiasi kwamba mwanamke asipojiunga anaonekana kama amejitenga. Hiyo mbinu si mbaya kuiiga, CDM wanaweza kuanzisha hivyo vikundi vya uzalishaji ambavyo vinaweza kutumika kama base ya kutolea elimu ya uraia na uhamasishaji kwenye maeneo yao.
 
Wakuu Mnaonaje na CDM ianze kununua Shahada za Wapiga Kura? Ina Ubaya gani hii Kwani tuonachotaka si ni Ushindi tu? Goli ni goli maana hata goli la Maradona la Mkono mwaka 1986 liliipeleka Argentina nusu Fainali na hatimaye ikatwa Ubingwa wa Dunia.

Hii Imekaaje Wakuu?
 
Wanawake kwa haiba na hulka yao hawapendi MILITANCY, wanapenda PEACE. Chadema ni militants (angalia hata magwanda yao) na CCM ni peaceful party.

Unadhani mwanamke atapenda nini kati ya magwanda yale wanayovaa akina Josephine Mushumbusi, na kanga wanazovaa akina Amina Makilagi? Ili wanawake wakipende Chadema, lazima wabadilike waache militancy. Nchi hii haihitaji kukombolewa, ilishapata uhuru. Inahitaji tu maendeleo, na maendeleo hayaletwi na ukamanda huu wa Chadema, bali hoja tu na sera nzuri za maendeleo.
 
Wakuu Mnaonaje na CDM ianze kununua Shahada za Wapiga Kura? Ina Ubaya gani hii Kwani tuonachotaka si ni Ushindi tu? Goli ni goli maana hata goli la Maradona la Mkono mwaka 1986 liliipeleka Argentina nusu Fainali na hatimaye ikatwa Ubingwa wa Dunia.

Hii Imekaaje Wakuu?
Hapana! hii siungi mkono kamwe....tuige yale ambayo ni mazuri kwa faida ya chama! lakini haya ya kununua shahada ni BIG NO
 
Wanawake kwa haiba na hulka yao hawapendi MILITANCY, wanapenda PEACE. Chadema ni militants (angalia hata magwanda yao) na CCM ni peaceful party. Unadhani mwanamke atapenda nini kati ya magwanda yale wanayovaa akina Josephine Mushumbusi, na kanga wanazovaa akina Amina Makilagi? Ili wanawake wakipende Chadema, lazima wabadilike waache militancy. Nchi hii haihitaji kukombolewa, ilishapata uhuru. Inahitaji tu maendeleo, na maendeleo hayaletwi na ukamanda huu wa Chadema, bali hoja tu na sera nzuri za maendeleo.

Mkuu Unatawala wowote Unaotumia Dola/Nguvu kujikita Madarakani Unawafundisha Watawaliwa/Wananchi wake kutumia Nguvu hizo hizo Kuupinga

So Usiwalaumu Wananchi kwa kuwa kama Militants bali Ilaumu Serikali yako ya CCM kuwafundisha kuwa Hivyo
 
Asante kwa makala nzuri na nafikiri Chadema watalifanyia kazi.

Ni juzi tu kulikuwa na makala kuwa BAWACHA wamelala sana Tanzania. Hata Dr. Slaa akasema atalifanyia kazi na hapo ndiyo ikaja ile statement yao juzijuzi.

Kuna kila sababu ya kubadilisha uongozi wa BAWACHA ikibidi maana wao kwa kweli wamelala sana. Ukiacha Marehemu Regina (RIP) ambaye alikuwa yupo kila sehemu, wanawake wengine wa Chadema kwa kweli wanasuasua sana. Mtu kama dada yake Lissu (heshima sana kwa kaka yake) na wengine wengi ambao walichaguliwa kama wabunge wa kuteuliwa, siwasikii kabisa na wanakuwa kama hawana mambo ya kushawishi au kuyafanya kwenye majimbo wanayotoka.

Labda wanafanya ila hawajitangazi ila hiyo nayo ni mbaya sana kwenye Siasa. Inabidi wawepo akina mama wenye kusumbua kidogo walau nusu ya John Mnyika au Zitto ili kila wakifika sehemu na kuitisha mikutano ya akina mama, itakuwa rahisi sana akina mama/wanawake kwenda kuwasikiliza.

Mwisho niseme kuwa inawezekana baadhi ya mikoa akina mama wachache ila kuna sehemu unakuta wanafunika na wanaimba kwa furaha kabisa kama dada zao akina Mura huko Msoma........ CCM PURESHA INAPANDA INASHUKA.

Last edited by a moderator:
Hapana! hii siungi mkono kamwe....tuige yale ambayo ni mazuri kwa faida ya chama! lakini haya ya kununua shahada ni BIG NO

Kwa Hiyo tugawe khanga, Tugawe Sukari, Tugawe Chumvi. Ndicho unachomaanisha? Na kama Ndicho unachomaanisha Khanga ngapi? Sukari kiasi gani? Chumvi kiasi gani? Be Open maana hapa Viongozi wa CDM huwa wanapitapita kuchukua Mawili Matatu
 
Wakuu Mnaonaje na CDM ianze kununua Shahada za Wapiga Kura? Ina Ubaya gani hii Kwani tuonachotaka si ni Ushindi tu? Goli ni goli maana hata goli la Maradona la Mkono mwaka 1986 liliipeleka Argentina nusu Fainali na hatimaye ikatwa Ubingwa wa Dunia.

Hii Imekaaje Wakuu?
Mkuu Albedo, si kila kitu lazima uige na si vyote vya CCM ni vibaya, ndiyo maana tunasema tunaweza kuchambua kilicho kizuri. CDM inafanya mengi sana yaliyotofati na CCM hata CCM nao kuna baadhi wanaiga toka CDM, kwa nini CDM isiigetoka CCM? Unajua kadri tunavyobadilishana uzoefu ndivyo tunavyolijenga taifa tusiwe rigid sana kwa yale tunayoyaamini tu. Juzi rais kakubali kuandikwa kwa katiba mpya jambo ambalo lilikuwa si ajenda ya CCM, angalia hili la posho, haya mambo tunapokubaliana kwa pamoja ingawa tuko kwenye itikadi tofauti ndiyo kujenga nchi.
 
Mkuu Unatawala wowote Unaotumia Dola/Nguvu kujikita Madarakani Unawafundisha Watawaliwa/Wananchi wake kutumia Nguvu hizo hizo Kuupinga

So Usiwalaumu Wananchi kwa kuwa kama Militants bali Ilaumu Serikali yako ya CCM kuwafundisha kuwa Hivyo

Wananchi ni kina nani mkuu hapa..militancy si wananchi ila chadema (viongozi)..

Wamekaa kishari kishari utafikiri wanakulaga ile kitu inaitwa bange..

sasa unafikiri wanawake hawataki hizo..
 
Wananchi ni kina nani mkuu hapa..militancy si wananchi ila chadema (viongozi)..

Wamekaa kishari kishari utafikiri wanakulaga ile kitu inaitwa bange..

sasa unafikiri wanawake hawataki hizo..

Noted with Thanks
 
Mkuu Albedo, si kila kitu lazima uige na si vyote vya CCM ni vibaya, ndiyo maana tunasema tunaweza kuchambua kilicho kizuri. CDM inafanya mengi sana yaliyotofati na CCM hata CCM nao kuna baadhi wanaiga toka CDM, kwa nini CDM isiigetoka CCM? Unajua kadri tunavyobadilishana uzoefu ndivyo tunavyolijenga taifa tusiwe rigid sana kwa yale tunayoyaamini tu. Juzi rais kakubali kuandikwa kwa katiba mpya jambo ambalo lilikuwa si ajenda ya CCM, angalia hili la posho, haya mambo tunapokubaliana kwa pamoja ingawa tuko kwenye itikadi tofauti ndiyo kujenga nchi.

Mkuu ni vizuri ukashari nini cha Kufanya ila Kujaribu Kupambana na CCM katika UTOAJI sidhani kama itakuwa ni Njia bora. Mimi nashauri Uongozi Mzima wa BAWACHA uangaliwe na Ikibidi itankwe kwamba wameshindwa Kufanya Kazi yao. Ona BAVICHA they are doing a very good Job. Ni Kazi ya BAWACHA kuwakomboa KIFIKRA wanawake wenzao
 
Chadema wasianze mchezo wa kutowa Takrima kwa Wanawake/wananchi wa Tanzania. Kwanza wanapitisha bakuli la kuomba michango kwa Watanzania na hapo Watanzania wanakuwa wanajua kabisa ni chama chao. Hii ya kuwapa watu vya bure, katika mbio za Marathon itaiingiza Chadema huko huko wanakokwenda CCM.

Chaguzi za Chadema zitaanza kuwa aghali sana na ufisadi utaanza hapo. Kama chaguzi za Chadema zitakuwa za bei nafuu, Wabunge watakuwa wanashinda bila ya kuwa na madeni makubwa kama CCM. Matokeo yake, misingi itakuwa imeshajengwa kuwa "Kama wewe ni kiongozi mzuri ila huna hela - NENDA CHADEMA."

Takrima Chadema lazima ipigwe chini kwa nguvu zote na ikibidi mtu akisikika katoa Takrima basi aondolewe kwenye uchaguzi mapema (wasimruhusu kugombea) na hili liwe linasimamiwa kwa nguvu zote. Mwanzo wa Ufisadi Tanzania ni hizo Takrima.

TANZANIA BILA UFISADI - INAWEZEKANA.

NB: Kama ni kugawa nguo, basi zigawiwe kwa Watoto yatima, wazee na vilema.
 
mwanamke anatakiwa akate kiuno kwa mmewe si kwenye public hapo ni kujidhalilisha,wengi wanaofanya hivyo ni wale wanaitwa lelemama na wamefadhiliwa na ccm،au kikundi cha ccm,cdm hawana kikundi chochote hata hivyo idadi ya kina si mtaji kigezo kwamba wanapenda chama husika,jiulize jimbo la musoma ilikuwaje kina mama wengi walienda kwenye mikutano ya ccm na mws wa siku walichagua cdm!labda wanafuata wanamuziki(bendi)
 
WanaJF, Heshima mbele wakuu!.

Hivi ni kwanini wanawake waliowengi wanaisaport Chadema kwa woga?
Nilianza kufatilia kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,baadae ikaja
ule uchaguzi mdogo wa Igunga na sasa ni huu wa Arumeru ulioanza kampeni
zake jana.
Katika mikutano yote ya kampeni za Chadema ni nadra sana kuona wanawake
wamejitokeza kwa wingi....sana sana watakuwa wachache sana na wanahesabika.
Tena kibaya zaidi wanakuwa hawana shamra shamra zozote za kuashiria kweli wao
ni people's power mpaka kieleweke.

Lakini ukifatilia kampeni na mikutano ya CCM na CUF utawaona wakinamama wame
furika kibao kupita maelezo! yaani utaona wanakata viuno,wanaimba na kucheza huku
wakishauti kwa kelele za kufa mtu.
Jamani kwa nini isiwe hivyo na kwa Chadema?

Hapo mkuu ujue kuna wakina nchemba wanotuharibia wake zetu. maisha magumu ndugu yangu na hawa magam,ba wamefanya makusudi ili sijui wawateke wanawake ambao kimsing ni dhaifu sana?

Kwa wale waliofuatilia ufunguzi wa kampeni za CDM jana kupitia StarTv live kutoka A
rumeru watakubaliana na mimi kwa 100% yaani uwanja mzima ulifurika wanaume...wa
nawake walikuwa wachache sana!
nakumbuka kuna mbunge mmoja mwanamke wa CDM
alisimama na akauliza kwa masikitiko makubwa sana'kwanini wanawake hawajajitokeza
kwa wingi kama wanaume?

Kidogo hapo umejichanganya mkuu. mbele tena unasema walikuwa wachache sana? Ooohoooo! Kumbe walikuwepo walau hao waaminifu kwenyendoa zao? Dah. thanx kwa hilo.

Wanabodi, Je,tatizo ni nini? kwanini wanawake waliowengi hawaisaport CDM? Na hao
wachache wakijitokeza basi huwa kama wamenyeshewa na mvua. Je tatizo ni nini?
1.Je wanaiogopa serikali ya ccm? au
2.wamelishwa propaganda na ccm kuwa Chadema ni chama cha fujo?

wanauchungu mkubwa hao mkuu. hao ndo wachache waliobakiwa ambao manyang'au ya ciciem hayajawapitia

Na mwisho Je,kifanyike nini ili CDM nao kwenye mikutano yao iwe inapata wamama wa kutosha?

ila kwa yote thanx for a perfect observance
 
Back
Top Bottom