Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

Mkuu ni vizuri ukashari nini cha Kufanya ila Kujaribu Kupambana na CCM katika UTOAJI sidhani kama itakuwa ni Njia bora. Mimi nashauri Uongozi Mzima wa BAWACHA uangaliwe na Ikibidi itankwe kwamba wameshindwa Kufanya Kazi yao. Ona BAVICHA they are doing a very good Job. Ni Kazi ya BAWACHA kuwakomboa KIFIKRA wanawake wenzao
You are missing the point, kuiga si kupambana ina maana rais anapoiga ya CDM mfano kuanzisha katiba anapambana na CDM, hapana ila anajenga nchi. Ninachoshauri, moja, kama nilivyosema BAWACHA ipewe nguvu watafutwe wanawake wachache(permanent) na wawezeshwe watakaokuwa wanazunguka mkoani kufungua miradi na kusaidia kuanzisha vikundi vya akina mama, pili, kwenye hivyo vikundi ikibidi wawe na mikakati yao wakati wa mikutano ya CDM ikiwa ni pamoja na kuhamasishana na njia mojawapo ni kuwa na sale ya kikundi hii sidhani kama ni mbaya.
 
Mkuu Albedo, si kila kitu lazima uige na si vyote vya CCM ni vibaya, ndiyo maana tunasema tunaweza kuchambua kilicho kizuri. CDM inafanya mengi sana yaliyotofati na CCM hata CCM nao kuna baadhi wanaiga toka CDM, kwa nini CDM isiigetoka CCM? Unajua kadri tunavyobadilishana uzoefu ndivyo tunavyolijenga taifa tusiwe rigid sana kwa yale tunayoyaamini tu. Juzi rais kakubali kuandikwa kwa katiba mpya jambo ambalo lilikuwa si ajenda ya CCM, angalia hili la posho, haya mambo tunapokubaliana kwa pamoja ingawa tuko kwenye itikadi tofauti ndiyo kujenga nchi.
Mkuu naunga mkono maono yako! zile trick mzuri za ccm si vibaya CDM wakiziiga...na zile trick mbaya za ccm hatuna budi kujiepushanazo kwa faida ya chama. Unajua sometime huwa najiuliza,kwanini CDM nao wasikodishe wanamziki wa bongo fleva kwenye mikutano yao kama wafanyavyo ccm? kwanini wasiwape wakinamama khanga na tishirts bure tu ili kuwavutia kwenye chama? Jamani yale mazuri ni lazima tuyaige kwa manufaa ya chama. Hivi kuna ubaya gani kumlipa pesa Lady Jaydee au TID ili haje kutumbuiza kwenye kampeni zenu?
 
Mkuu Unatawala wowote Unaotumia Dola/Nguvu kujikita Madarakani Unawafundisha Watawaliwa/Wananchi wake kutumia Nguvu hizo hizo Kuupinga

So Usiwalaumu Wananchi kwa kuwa kama Militants bali Ilaumu Serikali yako ya CCM kuwafundisha kuwa Hivyo

Albedo,

Nakubaliana na wewe,Kama watawala wanatumia nguvu lazima tu na wananchi watatumia nguvu,Kumbuka issue ya Wamachinga wa mbeya,Kule songea n.k.CHADEMA sio millitant,ntalipinga hilo kwa hoja zifuatazo;

1.Millitant party must be dictatorial-Ni ukweli usiopingika kwamba CDM imejipambanua kuwa chama cha kidemokrasia kwa kweli,Chaguzi zake nyingi zimekuwa huru na haki,Vitendo vya rushwa vinakemewa kwa matendo.

2.CDM Inapambana kwa hoja,katika hoja zote ambazo CDM Imekua ikisimamia ni nguvu ya hizo hoja ndiyo imeweza kuipambanua CHADEMA kutoka kwenye vyama vingine.

3.Pale ambapo umeona nguvu zikitumika juu ya CDM ni kwamba watawala wameshindwa hoja na kuamua kutumia nguvu ya dola(Jeshi na Polisi).Mfano Mauaji ya Arusha.

4.Kama kuna mtu anaweza kunipa mfano ambapo CDM wamechukua silaha ya aina yoyote ile dhidi ya yeyote hapo anaweza kunishawishi kuwa CHADEMA ni millitant.

5.Dhana ya Ukombozi ni Pana,Ukombozi sio lazima kutoka kwa wakoloni tu.Ukombozi tunaouhitaji sasa ni wa kifikra utakaowezesha watanzania kujitambua na hatimaye kuiweka CCM Pembeni.Ni ukweli usiopingika kwamba Thinking Capacity ya CCM imeshaisha katika kuchanganua changamoto za kimaendeleo tulizo nazo.

Kwa Hoja ya Akina mama

1.Naturally mwanamke ni mtu anayehitaji kupewa attention,kuwa Cared,kudanganywa kidogo tu (Samahani kwa akina mama).Ni mtu anayehitaji kubebwa taratibu(kubembelezwa).CDM kimekua ni chama cha watu kuamua kutoka mioyoni mwao kwamba wanachagua CHANGE.Initiative inachukuliwa na mtu mwenyewe.Kwa bahati mbaya wanawake wanaachwa nyuma.

2.CHADEMA inatakiwa kujiangalia upya katika eneo la kuwaweka wanawake juu,Wanawake wanatakiwa waonekane ili kuwapa moyo wanawake wenzao kwamba CHADEMA pia wamo.Kuna mchangiaji mmoja amesema waajiriwe watu rasmi kwa ajili ya ku wahamasisha wanawake.Nakubaliana na hilo.

3.Sikubaliani na kugawa T shirt na kanga kwa wanawake,Acha CDM ijipambanue kama chama cha hoja na cha watu wanaofuata hoja na waliokombolewa kifikra.Ukombozi wa kweli wa fikra kwa watanzania wote ni Process,ni process ya mda mrefu,Inahitaji resource za kutosha.CDM Katika kipindi hiki inatakiwa kujituma kweli kweli.

Otherwise Topic ni nzuri
 
Mkuu naunga mkono maono yako! zile trick mzuri za ccm si vibaya CDM wakiziiga...na zile trick mbaya za ccm hatuna budi kujiepushanazo kwa faida ya chama. Unajua sometime huwa najiuliza,kwanini CDM nao wasikodishe wanamziki wa bongo fleva kwenye mikutano yao kama wafanyavyo ccm? kwanini wasiwape wakinamama khanga na tishirts bure tu ili kuwavutia kwenye chama? Jamani yale mazuri ni lazima tuyaige kwa manufaa ya chama. Hivi kuna ubaya gani kumlipa pesa Lady Jaydee au TID ili haje kutumbuiza kwenye kampeni zenu?

RIP chadema
 
You are missing the point, kuiga si kupambana ina maana rais anapoiga ya CDM mfano kuanzisha katiba anapambana na CDM, hapana ila anajenga nchi. Ninachoshauri, moja, kama nilivyosema BAWACHA ipewe nguvu watafutwe wanawake wachache(permanent) na wawezeshwe watakaokuwa wanazunguka mkoani kufungua miradi na kusaidia kuanzisha vikundi vya akina mama, pili, kwenye hivyo vikundi ikibidi wawe na mikakati yao wakati wa mikutano ya CDM ikiwa ni pamoja na kuhamasishana na njia mojawapo ni kuwa na sale ya kikundi hii sidhani kama ni mbaya.

Mkuu Feedback inawezekana kwamba "Nina Miss Point Fulani hapa". Kama nitakuwa nimewapata vyema wachangiaji ni kwamba.

1. CCM huwa WANAGAWA ( Siyo Kuuza) khanga kwa akina Mama ambao wengi wao kweli wanazihitaji hizo khanga kutokana na level zao za Vipata. Vile vile huwa wanagawa Sukari na Vitu kama hivyo na Ndio Maana Ikaja Point ya KUIGA

Sasa nisichokuelewa hapa (Ndio maana unasema ninamiss point) Ni Kwamba Una Suggest CDM nao WAGAWE Khanga na Other PA Materials au WAWAUZIE hao akina Mama?

Twende Pamoja kaka naamini mwisho wa siku tutakubaliana na Ikibidi Kukubaliana kutokukubaliana
 
Mkuu humo nilimobold....natamani hata wangekuwa wanawatafuta wanawake wauza-bar, wanawapa darasa la kutosha
na wanakuwa wahamasishaji wa wanawake wengine kwenye mikutano ya Chadema na huku jukwaani Lady Jaydee akitumbuiza live. Jamani vizuri viigwe! wakinamama wanamiminika kwenye mikutano ya ccm kwa vitu vidogo kama hivi.
 
Hii kali wanawake wauza bar lol..rip chadema
 
Chaguzi za Chadema zitaanza kuwa aghali sana na ufisadi utaanza hapo. Kama chaguzi za Chadema zitakuwa za bei nafuu, Wabunge watakuwa wanashinda bila ya kuwa na madeni makubwa kama CCM. Matokeo yake, misingi itakuwa imeshajengwa kuwa "Kama wewe ni kiongozi mzuri ila huna hela - NENDA CHADEMA."
Kwenye bold mkuu hapo ndipo Chadema watakapopata viongozi wazuri, uchaguzi wa CCM umekuwa wa pesa, kuna jamaa yangu ni mwana CCM mzuri kweli kweli ninajua uwezo wake, nilimshauri agombee ubunge kwenye jimbo lake kupitia chama chake akasema yeye hana pesa za kuhonga wajumbe ingekuwa zamani angegombea. CDM wakiendelea kuchaguana kama walivyofanya uteuzi wa Nassari naamini vijana wengi kama hao wa CCM watavutika kujiunga na kugombea kupitia CDM.
 
Kwanza inategemea na mkoa, mfano Kigoma wanawake wengi sana Chadema, pili, Chadema hawana mda wa kutoa rushwa ya Kanga, Kofia, Tshirts na pia mda wa kuleta Bongo fleva, taarabu n.k. Katika mikutano yao, wanawake wengi hawapendi mambo serious kama yanayofanyika katika mikutano ya Chadema. Wakati utafika maisha yatawafanya waujue ukweli na hapo ndipo wataiunga mkono Chadema. Bakora za maisha zitawarudisha kwenye mstari, muhimu Chadema iendelee kutoa elimu ya uraia kwa nguvu sana hatimae matunda yatatokea.
 
Mkuu Feedback inawezekana kwamba "Nina Miss Point Fulani hapa". Kama nitakuwa nimewapata vyema wachangiaji ni kwamba.

1. CCM huwa WANAGAWA ( Siyo Kuuza) khanga kwa akina Mama ambao wengi wao kweli wanazihitaji hizo khanga kutokana na level zao za Vipata. Vile vile huwa wanagawa Sukari na Vitu kama hivyo na Ndio Maana Ikaja Point ya KUIGA

Sasa nisichokuelewa hapa (Ndio maana unasema ninamiss point) Ni Kwamba Una Suggest CDM nao WAGAWE Khanga na Other PA Materials au WAWAUZIE hao akina Mama?

Twende Pamoja kaka naamini mwisho wa siku tutakubaliana na Ikibidi Kukubaliana kutokukubaliana
Mkuu kama ukifuatilia post zangu zote nimesema chama kinaweza kuuza na kupata double profit na si kugawa. Mfano sasa wanavyouza CD, skafu n.k hawagawi kwa nini isiwezekane kwenye sale za akina mama. Najua hapo litakuja suala la vipato sawa ndiyo maisha yetu wengine wanacho wengine hawana.
 
CHADEMA huongea vitu logical ambavyo ni nadra wanawake kupenda kuvisikia. Wao huvutiwa zaidi na vitu vidogo vidogo kama Khanga, pilau, taarab za TOT na vilemba bila kusahau fulana zenye picha ya mgombea.

Kama unabisha jikumbushe wakati unamtongoza huyo mkeo/demu wako je, ulimuweka kwenye laini kwa kumueleza mipangoyako ya muda mrefu au kwa pipi pipi na kitop?
 
Back
Top Bottom