Kwanini wanawake wanaiunga mkono CHADEMA kwa woga?

mshika chuma zisi sredi is very critical and important indeed...

uhamasishaji mdogo miongoni mwa wanawake katika chadema ndicho kinachoianguisha siku zote na kuibeba sisiemu...

kutokana na kwamba wanawake kimsingi ni WENGI na HUPIGA KURA kwani mara nyingi hawasafiri de facto residents...

na ni waaminifu kwa wanayoyaahidi...ndio maana wakiishagaiwa kanga ya mgombea....huwa waaminifu kumpa kura

nadhani CCM ina mengi inayowadanganya nayo...eg maji na huduma za afya zinazotolewa afisi za sisiemu....

na pia wanaume wengi wenye nguvu bado wako sisiemu..so huwainfluence hawa kina mama....

lakini kubwa kulikoyote.....IDARA YA KINA MAMA YA CHADEMA BADO IMESINZIA....

HII INATAKIWA KUFANYA KAZI IKIFEATURE BOTH PRACTICAL AND STRATEGICAL NEEDS ZA KINA MAMA...

UKITAKA MAONI ZAIDI NIPM!
 
Seriously, nakubaliana na mada kiukweli,ni vizuri tuliangalie kwa kufanya research ya kuwa inakuwa vipi upande wa magamba wanakuwa wengi.....Jibu si jepesi kwa upande mwingine ni jepesi,kwa risechi yangu niliyofanya wakati wa kampeni za uchaguzi 2010 nikiwa jijini Mwanza niliona magmba mbinu wanayotumia kuwapata wanawake.Kuna makada wa kike katika kata ambao kazi yao ni kuhakikisha kina mama wamepewa khanga,kofia na t-shirts na siku ya mikutano ya magamba kunatolewa usafiri bure kutoka kila pande,kwa mfano katika mkutano wa kampeni ya uraisi,magamba walitoa magari yalochukua watu sana sana kina mama coz walikuwa wameshavaa sare tayari,wakpelekwa Misungwi tokea mjini na wale wa Misungwi,Magu,Sengerema waliletwa CCM kirumba.Niambieni kwa stairi hii utapata idadi gani kwa wingi kati ya wanawake na wanaume?definetely watakuwa kina mama.....
 
Seriously, nakubaliana na mada kiukweli,ni vizuri tuliangalie kwa kufanya research ya kuwa inakuwa vipi upande wa magamba wanakuwa wengi.....Jibu si jepesi kwa upande mwingine ni jepesi,kwa risechi yangu niliyofanya wakati wa kampeni za uchaguzi 2010 nikiwa jijini Mwanza niliona magmba mbinu wanayotumia kuwapata wanawake.Kuna makada wa kike katika kata ambao kazi yao ni kuhakikisha kina mama wamepewa khanga,kofia na t-shirts na siku ya mikutano ya magamba kunatolewa usafiri bure kutoka kila pande,kwa mfano katika mkutano wa kampeni ya uraisi,magamba walitoa magari yalochukua watu sana sana kina mama coz walikuwa wameshavaa sare tayari,wakpelekwa Misungwi tokea mjini na wale wa Misungwi,Magu,Sengerema waliletwa CCM kirumba.Niambieni kwa stairi hii utapata idadi gani kwa wingi kati ya wanawake na wanaume?definetely watakuwa kina mama.....
Well said! pamoja sana mkuu!....ndiyo maana mie nimeamua kuwashauri CDM kuwa si vibaya tukiiga mazuri toka kwa CCM
na CUF. Jamani leo si tumejionea CUF walivyokodi malori kibao kwa hajili ya wanachama wake huku Afande Sele akitumbuiza? jamani si tumeona wakinamama walivyojazana kwenye mapokezi ya Lipumba? Binafsi napendekeza malori,
khanga,na bongo fleva vitumiwe rasimi na CDM ili kuvutia wamama wengi....tukisema eti tuwasubilie BAWACHA au mambo
ya sizitaki mbichi hizi basi CDM musahau kushika dola. Jamani mazuri tuyaige kwa faida ya chama letu.
 
Wanawake ndio sehemu kubwa ya waathirika wa umasikini (rejea umasikini una sura ya mwanamke TZ). Pia kielimu wengi wake nyuma Sana. Ukichanganya na mfumo dume unaowakandamiza kijamii, wengi fikra zao huishia kwenye misaada na watu wa kuwabeba (affectionate) hata wakiwa walaghai. CCM wanaitumia karata hiyo vyema. Lakini huo ni udhalilishaji kwa kasi zaidi wa mama/dada zetu. Tunahitaji kukazania ukombozi wa kifikra zaidi. Tumeona akina mama walioamka jinsi wanavyofanya vitu vya uhakika (Bisimba, Ananilea, Josephine, Halima, Regia-RIP, n.k.). Wako wengi tu wasio na majina. Kwanza sikubaliani na dhana nzima ya kuiga "mazuri" ya CCM. That now is almost a mafia party!
 
Vyama vyote vya Upinzani haviwalengi wananchi ktk jamii zao isipokuwa siasa za majitaka. Chadema vs CUf au NCCR au CCM...na kuzungumzia WATU kajamba nani ndio siasa zilizopo.. Chadema wanatakiwa kuacha siasa hizi na kuanza kulenga wananchi ktk jumuiya zao. Chadema itawafanyia nini Wanawake, Itawafanyia nini Wakulima na Wafanyakazi, wachimba madini, wafanya biashara. Nini msimamo wao ktk hoja na maswala ya Muungano na dini..
 
hii inshu ina ukweli kimtazamo,nilifanya project kijijini si ya siasa, lakini nikiwa huko niligundua wale wajumbe wa magamba hupita kwa akina mama kuwaalika kuhudhuria shughuli za kichama ikiwa ni pa1 na kushiriki ufunguzi wa kampeni na hupewa khanga na kwa kweli akina mama wengi ni waaminifu kwa viongozi wao ni vigumu kukaidi mialiko kama hiyo. kwa CDM hakuna k2 kama hicho wao huamini kwenye nguvu ya umma.
 
Vyama vyote vya Upinzani haviwalengi wananchi ktk jamii zao isipokuwa siasa za majitaka. Chadema vs CUf au NCCR au CCM...na kuzungumzia WATU kajamba nani ndio siasa zilizopo.. Chadema wanatakiwa kuacha siasa hizi na kuanza kulenga wananchi ktk jumuiya zao. Chadema itawafanyia nini Wanawake, Itawafanyia nini Wakulima na Wafanyakazi, wachimba madini, wafanya biashara. Nini msimamo wao ktk hoja na maswala ya Muungano na dini..

Katika post zako zote nilizowahi kusoma, leo umeongea cha maana.

Malaria Sugu, aliwahi kuulizia hilo kwenye nyekundu, akaitwa "mdini".
 
Wanawake walio CCM ni wale wasiojitambua na kujua mustakabali wa maisha yao,kama walivyo baazi ya wanaume walio CCM.Sizani kama hoja hii inamsingi sana kusema kuwa CDM haina support ya kina mama.
 
Jibu ni rahisi ni kwasababu ya MFUMO DUME. Tunafahamu kwamba CCM kwasasa mtaji wake MKUBWA ni kwa Watanzania wenye UFAHAMU mdogo wa masuala mbalimbali (ELIMU DUNI). It is very unfortunate kundi kubwa lililothirika na huo mfumo ni WANAWAKE. AND It more unfortunate kwamba kundi hili ndiyo WAPIGAJI kura wazuri. I'm sorry to say this viongozi wetu tunachaguliwa na watu wenye ELIMU DUNI.

Hivyo CCM inajua kuwa imewekeza UJINGA kwa WANAWAKE ili iendelee kupata kura UNQUESTIONABLE. Ukifika vyuoni ni TOFAUTI kabisa, wanafunzi wa KIKE wa VYUONI wao na CCM ni mbalimbali.

DEMOCRASY IS A SLOW PROCESS, We still have a long way to go. Demokrasia ya kweli itapatikana pale majority ya wapiga kura watakapokuwa basic education ya kuweza kuchambua PUMBA na MCHELE na sio kugawiwa kanga!
 
Vyama vyote vya Upinzani haviwalengi wananchi ktk jamii zao isipokuwa siasa za majitaka. Chadema vs CUf au NCCR au CCM...na kuzungumzia WATU kajamba nani ndio siasa zilizopo.. Chadema wanatakiwa kuacha siasa hizi na kuanza kulenga wananchi ktk jumuiya zao. Chadema itawafanyia nini Wanawake, Itawafanyia nini Wakulima na Wafanyakazi, wachimba madini, wafanya biashara. Nini msimamo wao ktk hoja na maswala ya Muungano na dini..
Mkuu Mkandara,ahsante kwa mchango wako japo hujagusia mada yetu inayohusu wanawake na Chadema.
Alafu hapo nilipobold unamaanisha nini? Muungano na dini!!!? hebu funguka ili tukusome.
 
Katika post zako zote nilizowahi kusoma, leo umeongea cha maana.

Malaria Sugu, aliwahi kuulizia hilo kwenye nyekundu, akaitwa "mdini".
Dah, yaani siku zote naandika pumba!.. Kama hoja hii ilivyo pengine siku zote sijazungumzia vitu vinavyokugusa na kukuvutia wewe leo nimekugusa na mapenzi yako yameonekana - Karibu sana.
 
Mkuu Mkandara,ahsante kwa mchango wako japo hujagusia mada yetu inayohusu wanawake na Chadema.
Alafu hapo nilipobold unamaanisha nini? Muungano na dini!!!? hebu funguka ili tukusome.
Majibu ya vitu vyote navyovisema vipo ktk Katiba ya Chadema lakini hazitumiwi ktk kampeni na wanachama au viongozi wetu hadharani kwa kuchelea kuonekana vibaya ila huyagusia tu kukana kama kuna tuhuma fulani maana siasa zetu ni kupakana matope tu.

Pia kuna tabia ya watu kuwa na mtazamo tofauti na katiba ya Chadema, hili halizungumziwi maana wapo wanachama wa CDM na wengine viongozi wanapingana na katiba inapofikia maswala ya haki kimtazamo kuhusiana na jamii zetu Kimuungano na Kidini. Ndio maana husema siasa za Bongo ni Unafiki mtupu na hili halikwepeki. Jamii isokuwa na Principals, Ethics na Values isipokuwa zile za ku-copy na kupaste kutoka nchi za Ulaya huunda Jamii iliyopoteza tamaduni zake na ndiko tunakoelekea.

Huwezi kuwakuta viongozi na vijana wa Chadema wakivizungumzia ktk mikutano ama mijadala kama hii in a positive way. Tunapenda sana kuzungumzia WATU kama Jussa wanaofanya makosa japokuwa ndio wakweli ktk mitazamo na nafsi zao zinavyowatuma hata kama sio msimamo wa chama kuhusiana na swala hilo hilo. Na hata mtu kama Tundu Lissu anapozungumzia maswala ya Muungano huzungumzia ya Kitaifa na kikatiba (ya taifa) na sio msimamo wa CDM kuhusiana na muungano..The all point ni kwamba - Je, Chadema itawafanya nini kuboresha mahusiano ya kijamii (pale tunapogongana) - Hatuna majibu toka midomoni mwa viongozi.
 

Na Stephano Mango, Songea
WANAWAKE nchini wametakiwa kuzisikiliza sera za Chama chaDemokrasia na Maendeleo Chadema na kujiunga na chama hicho chenye malengo yakuleta ukombozi kutoka mikononi mwa Chama cha Mapinduzi ambacho kimewanyonyawatanzania kwa muda mrefu na kuwafanya maskini

Wito huo umetolewa jana na Katibu wa wanawake wa ChademaJimbo la Songea Asia Ngonyani akiwahutubia mamia ya wananchi baada ya kufunguaTawi la Chadema na Ofisi ya Chama hicho mtaa wa Kuchile kata ya SeedfarmHalmashauri ya Manispaa ya Songea kwenyeziara yenye lengo la kuimarisha chamakatika kata za pembezoni mwa mji

Ngonyani alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kimekuwakikiwatumia wanawake kwenye chaguzi mbalimbali na kuwavesha vilemba na vitengeambavyo hata ukivaa vinaangaza na baada ya kumaliza uchaguzi na kuunda Serikaliambayo imekuwa ikikosa mipango na vipaumbele vya kuwakomboa wanawake kiuchumina kijamii

Alieleza kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imekuwa ikiwanyanyasana kuwadhalilisha sana wanawake wanapokuwa kwenye biashara zao ndogondogo kwakuwakamata na kuwanyang’anya vitu vyao kwa kutumia mgambo wa mji hali ambayoinaendelea kuwaondolea utu katika jamii

Alisema kuwa kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikiwadanganyawakina mama kuwa huduma za kujifungua ni bure na matibabu ya mtoto wa chini yamiaka mitano ni bure wakati wakina mama wanalipia huduma hizo kwa fedha nyingi

Alifafanua kuwa licha ya wakina mama kulala wanne wannekwenye kitanda kimoja na wengine kulala chini , basi ukitaka kufa au kupotezamtoto katika vituo vya afya au Hospital za Serikali usiwe na fedha au umwambiemuuguzi kuwa natakiwa kupata huduma za matibabu bure

Naye Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kataya Mjini Joseph Fuime akiwahutubiawananchi hao alisema kuwa Serikali imeshindwa kuwaheshimu watanzania kutokanana matendo yao katili dhidi ya wananchi kutokana na kuwapandishia gharama zamaisha kila kukicha,kushindwa kutekeleza ahadi ya maisha bora kwa kilamtanzania,kuwatoza kodi nyingi huku wakishindwa kutoa huduma stahiki kulinganana kodi zinazotozwa kwa wananchi

“Ili kufanya mabadiliko katika nchi hii ni lazima wananchiwaamue kuchukua hatua za kuzisikiliza sera za Chadema na kujiunga nacho ilikuweza kuleta ukombozi stahiki mara uchaguzi wa Serikali za Vijiji,Mitaa nakatika uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Urais”alisema Fuime

Alisema kuwa leo tumefungua Ofisi ambayo imegharamiwa nabaadhi ya wanachama wa Chadema katika kata yenu hivyo tumewaletea chama chenyeuhai na matumaini kwa watanzania na ambacho kina dhamira ya kweli ya kuwakomboawatanzania

Alieleza kuwa hakuna anayelazimishwa kukipokea na kujiunganacho hivyo kama mnataka kuendelea kukandamizwa na Serikali ya Ccm miaka 50ijayo ya uhuru,mnahiyali ya kukipokea au kukikataa kwa faida yenu na vizazivijavyo
MWISHO

 

NA ASHTON BALAIGWA

24th July 2012


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Morogoro, CDM kimesema wanawake ndio kikwazo cha mabadiliko ya mageuzi nchini na kuwataka wanaume kuwalazimisha wake zao kukiunga mkono chama hicho hata ikiwezekana kuwatishia kwa talaka.

Chadema kimesema mikutano mingi ya chama hicho imekuwa ikiungwa mkono na wanaume huku kukiwa na idadi ndogo ya wanawake jambo ambalo ni kikwazo kwa chama hicho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jirani la ofisi za Kikosi cha Zima Moto mjini hapa juzi, Katibu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) Wilaya ya Morogoro, Mercy Maula, alisema wanawake wamekuwa mtaji wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika chaguzi licha ya kundi hilo kukabiliwa na changamoto nyingi.

AlisemA ipo haja kwa wanaume kuwashawishi wake zao kushiriki katika mikutano inayoitishwa na chama hicho ili kuwa na chachu ya mabadiliko bila woga.

"Jitahidini katika mikutano mingine mje na wake zenu na wale wenye girlfriend (rafiki wa kike) waleteni pia ili kutambua madhaifu ya CCM na kujua kwanini Chadema inataka mabadiliko nchini"alisema Maula.

Naye Mhamasishaji wa Chadema Taifa, Steven Daza, alisema chama hicho kinakusudia kufanya maandamano katika mkoa wa Morogoro ya kupinga ugumu wa maisha na kutaka wananchi kuyaunga mkono.




CHANZO: NIPASHE


 
Hii ndio Voting Block kama CHADEMA inataka kushinda 2015 inahitaji kuwashawishi hawa...

Sababu ndio wengi kuliko wanaume; ndio ambao hawabadiliki kirahisi Mara nyingi ndio wanaoichagua CCM
 

NA ASHTON BALAIGWA

24th July 2012


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Morogoro, ccmkimesema wanawake ndio kikwazo cha mabadiliko ya mageuzi nchini na
kuwataka wanaume kuwalazimisha wake zao kukiunga mkono chama hicho hata ikiwezekana kuwatishia kwa talaka.

CHANZO: NIPASHE



say it again? Siasa ni fani, kama sio fani zenu msikurupuke jamani.
 
Come down. Nilikuwa kwenye huo mkutano, she was just joking...

Mwandishi namjua wewe sikujui, mwandishi hajaandika popote kuwa msemaji alikuwa anajoke. No serious leader can joke on serious issues. Tell me she is not a serious leader, I will understand.
 
Back
Top Bottom