Joyboy
JF-Expert Member
- Sep 16, 2023
- 1,386
- 3,455
Habari zenu wadau.
Ninachosema hapa wengi mnaweza kuwa mashahidi.
Wanaume wengi tukifikisha miaka 50 kwenda juu huwa ndo muda ambao wanawake wengi wanatutapeli, wanatudanganya sana na wengi wetu ndo muda ambao tunaibiwa mali zetu na wanawake, haswa wanawake wadogo(20-30)
Nimesikia na kuona visa vingi kutoka kwa ndugu na marafiki.
Katika huo umri wanaume wengi tunaanza kuwa na tamaa za michepuko, michepuko inatutapeli sana hela, wakitudanganya wanatupenda huku wakitupa joto la ujana, bac tunapagawa tunagawa hela tuu na kuwanunulia vitu vya dhamani hadi michepuko mingine wanapangishiwa nyumba na kufunguliwa biashara, utapeli mtupu.
Katika huohuo umri wanaume wengi tunadanganywa sana na vitoto vidogo, kama kuna babu flani hapa mtaani kipindi cha nyuma kidogo, alikuwa ana uwezo wa kifedha, kuna kitoto cha miaka 22 eti kilimwambia "babu si uinoe tuu" bac yule mzee akamuoa, akaona kama kaokota embe chini ya mnazi, akasema "mapenzi si ndo haya sasa uzee wote huu nimependwa na damu changa".
Bac yule mzee bhana kuna nyumba walikuwa wanakaa watoto wa mke wa kwanza, akawafukuza wote akamweka mke wake mpya(mke wa tatu) akawa anakaa naye, kulitokea mgogoro mkubwa sana hadi mke wake wa kwanza akafariki kwa presha, yule mzee bado akakaza kichwa, haikupita muda yule mzee akafariki na yule mwanamke akaridhi ile nyumba, huu ni ujambazi wa hali ya juu.
Hata Role model wangu sikuamini na yeye atadanganywa na kuingia kweny mtego kirahisi, mzee Reginald Mengi, aliachana na mke wake wa ujana ambaye alianza nae maisha, akaja kuoa kasichana kadogo(Shetani mzima mzima), nayeye alivofariki yule mwanamke akaridhi mali zake.
Mama yangu alishawahi kuniambia, "mwanaume akiwa na miaka 40 kushuka chini anakuwa wamoto sana, humgusi, mwanamke hawez kumpelekesha, anakuwa makini sana na wanawake matapeli, ila akigusa tuu 50 bac anakuwa kama zoba, anadanganywa na kutapeliwa kirahisi sana na wanawake"
Hata kweny ndoa nyingi za ndugu na marafiki naonaga hii hali, wanaume below 40 wanakuwa maridadi sana ila wakifikisha 50 tuu na kuendelea umaridadi wote unaondoka, ule ujanja ujanja haupo tena, na kama ana tamaa na vitoto vidogo ndo atatapeliwa hadi hela ya uzeeni.
Ushawahi kujiuliza kwann wasichana wengi wanapenda wazee?
Tuwe makini tunapoelekea huko uzeeni, usikubali kutapeliwa.