Kwanini wananchi wana chuki kubwa na Jeshi la Polisi?

Kwanini wananchi wana chuki kubwa na Jeshi la Polisi?

Wanadhulumu raia mali zao?

Wanabambikia raia kesi?

Wanachukua rushwa kwa nguvu?

Wanapiga raia hovyo hovyo?

Wananachukua wake za watu kwa nguvu?

What' s wrong with PT?
Mkuu alichofanyiwa mbatia na kamati yake Jana, nadhan swali hili linaweza kukupa mwanga wa jibu
 
Maaskari wengi Ni wahalifu na wanababikimbia Raia kesi na kutaka rushwa ndio maana hamza kawanyoosha baadhi
Mimi mwenyewe nilishabambikiziwa kesi na polisi sina nao hamu
 
Sure.

Polisi wetu wanafanya kazi masaa 24. hakuna kulala iwe Mvua liwe Jua.
Tena kazi hatari za kupambana na Wahalifu wa aina zote ili kumlinda Mwananchi wa Mjini, Vijijini na Vitongoji vyake vya mbali sana huko.
Usiku wa manane wako kazini iwe Mvua Liwe Jua.
Na maisha yao tunayaona yalivyo duni sana.
Kipato chao ni duni.

Kazi ya Jeshi liwe la Polisi
ni ya kujitolea tu, malipo yao ni kama Posho tu ya Asante kwa kazi ngumu.
Kwa nchi zetu za dunia ya Tatu na ya Pili, tunashindwa kuwalipa watumishi wa Jeshi la Polisi sawasawa na kazi zao.
Kutokana na Uchumi mdogo.
Ndo wabambikie kes, kudhulum, kupiga watu ovyo, rushwa za kuforce? Kwa kua wanalala nje kazin ? Kama mshara mdg wameforciwa kufanya iyo kaz?
 
Ndo wabambikie kes, kudhulum, kupiga watu ovyo, rushwa za kuforce? Kwa kua wanalala nje kazin ? Kama mshara mdg wameforciwa kufanya iyo kaz?
Mbona hata madaktari, wajeda hulala nje ya familiar zao wakifanya kaxi zao lakini ni waadilifu.in Short jeshi letu la police halina credibility asilimia 98 ni wahalifu. Bora lifanyiwe reformation
 
Ruyama,
Yanatoka moyoni haya?

Dallas green,
Ndo wabambikie kes, kudhulum, kupiga watu ovyo, rushwa za kuforce? Kwa kua wanalala nje kazin ? Kama mshara mdg wameforciwa kufanya iyo kaz?
..........................................................
Angalia kuna Mada humu Serikali imetangaza nafasi za Jeshi la Polisi.
Tazama Sifa zilizopendekezwa.
Alaf uje utuambie tatizo liko wapi.

Serikali inafanya juhudi zote kuajiri Polisi waadilifu.
Tatizo linatoka katika mzizi wa malezi wa vijana kuanzia ngazi za Familia hadi vyuoni.
 
Wewe walikufanya nini Polisi hadi upaniki namna hii ?
Naona hadi busara imekutoka kabisa.
Tuelezee ulionewa nini ?
Una cheo gani?? Wewe ni msemaji was polisi mitandaoni??? Msipojirekebisha mtakuwa hunted....Time will tell
 
Hawachukiwi na watu wote, wanaowachukia ni baadhi tu ya raia kutokana na sababu mbalimbali kama.

1. Baadhi ya wananchi ni wahalifu adui yao ni Polisi.
2. Baadhi ya Polisi (wachache sana) hawazingatii kufanya kazi kwa miiko ya Jeshi la Polisi.
3. Baadhi ya raia wanasikia tu kuwa Polisi ni wabaya na wanaamini bila kujiridhisha.
4. Baadhi ya raia hata hawajui majukumu ya Polisi na hawataki kuyaelewa.
5. Hakuna elimu ya kutosha ya kuwafahamisha raia majukumu ya Polisi.
6. Baadhi ya Polisi wanajiweka kando na raia. (Mtoto akimwona Polisi anakimbia anamwogopa kwani kila akimwona basi anakuja kukamata wahalifu, hajawahi kumwona akishirikiana na raia ktk jambo lolote zuri)
7. Baadhi ya Polisi ni wakali sana hata kwenye jambo lisilohitaji kufanyika kwa ukali, wanatumia nguvu kupita busara. Inasababisha Polisi kumwona
kila raia ni mhalifu, hali kadhalika raia naye kumwona kila Polisi ni Adui.
8.Baadhi ya Polisi wanawadharau raia, hivyo kukosa ushirikiano wa karibu na raia.
9. Baadhi ya Polisi wanawatisha raia. Wanajiweka katia hali ya kutisha.
Hata raia akiona jambo baya mahali anaogopa kuliripoti Polisi ili kuondokana na hasara anayoweza kuipata binafsi kama, kugeuziwa kesi nk.
10. Ukosefu wa Elimu ya kutosha ya "Mahusiano ya Polisi na Raia" yaani ( Civil Police Relations) katika jamii ya Police na Raia.

Kuna haja ya kusisitiza mtaala wa (Thamani ya Raia kwa Polisi)
Katika vyuo vyetu vya Polisi.
Pia Nadharia ya Polisi Shirikishi itiliwe mkazo.
Elimu ya, wajibu wa Polisi, inabidi nayo itolewe kwa vijana mashuleni na kwa wananchi wote. Ili wajue majukumu yao halisi na wasaidiane nao kwa kiwango gani.

Machache ninayoweza kusema.
Well clarified[emoji106]
 
Luka 3:
Luke

14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.

14 Likewise the soldiers asked him, saying, "And what shall we do?" So he said to them, "Do not intimidate anyone or accuse falsely, and be content with your wages."
Kuna wazee walikuwa polisi wakaacha kazi wakasema ni kazi yenye laana sana kutokana na dhuruma, wakaenda mbali zaidi na kusema dhuruma zingine ni za kushinikizwa na wakubwa, "...muda mwingine unashinikizwa kudhurumu uhai wa mtu asiye na hatia" alisikika akinung'unika "...nikamkumbuka Daudi Mwangosi alivyodhurumiwa uhai wake kinyama"
 
Una cheo gani?? Wewe ni msemaji was polisi mitandaoni??? Msipojirekebisha mtakuwa hunted....Time will tell
Hoja iko mezani, inachangiwa kwa hoja.
Wewe unaleta matusi, kejeri na vitisho.
Badala ya kuchangia hoja.

Halafu unawalaumu Polisi kwa kutokuwa na Maadili mema.

Je hayo ndiyo maadili tunayoyazungumzia hapa ?

Kuwa hunted ndio kitu gani ?
 
Soma tena nilichoandika. Una panic kizembe Sana....Una mihemko na mahaba ya hiyo ajira yako ya upolisi...

Jirekebisheni.. muda ni mwamuzi mzuri.

Nipo kipembeni nadere
Hapa tunachangia Mada.

" Kwanini Jeshi la Polisi linachukiwa na wananchi "

Wewe unataka kuni hunt mimi, huoni kuwa unakiuka maadili.
 
Kuna polisi alinidhulumu laki na 80.mzee siro anatakiwa aunde dawati la mwananchi katika vituo vikubwa.kwa ajili ya wananchi kupeleka malalamiko yao dhidi ya polisi hii itasaidia kuweka mahusiano mazuri kati ya raia na jeshi la polisi.
 
Hahahaha.....sio kosa langu wewe kutokuwa na exposure na lugha za wengine..

Pole sana
Siku nyingine, changia mada husika, acha kushambulia wachangiaji.
Humjui unayemshambulia, anaweza kuwa baba yako mzazi.
 
Back
Top Bottom