Aisee...Kwema wakuu,
Nimekutana na mwalimu kwenye daladala ambaye alinifundisha zaidi ya miaka 20 iliopita na bado yupo ngangari, muonekano ule ule,
Nilimtambua japo yeye hakunikumbuka kirahisi, nina mifano mingi ya walimu ambao bado wanaonekana vizuri hata baada ya miaka mingi kupita,
Swali langu ni je? kwanini walimu hawazeeki kirahisi? Huwa hawana stress za maisha kama watu wengine au siri ni nini?
Ama kweli walimu wamebarikiwa sana.
Kuna wale waliosoma Zanaki P/S miaka ile kulikuwa na mwalimu mmoja bomba kweli anaitwa Mwalimu Seifu
Baada ya miaka 25, nilikutana nae mnazi mmoja sikuamini macho yangu, yuko vile vile bomba hata ningekuwa mshenzi ningeaanza kumtamani. na kumtongoza.....
Lakini nilimuamkia na mindevu yangu kwa heshima na taadhima na nikamkatia $100 kama asante Mwalimu, tukapiga stori mbili tatu
Natumai bado ni mzima wa afya na nauombea afya na uzima tele.....