Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,240
2,866
Tunavutia wawekezaji lakini njia za kuwekeza na Sheria za uwekezaji haziko Ikulu.

Tunazo Wizara na ofisi zinazohusika. Kwa kuwa marais wetu wameamua kuwa ni waalikaji wa wawekezaji, nawaona Mawaziri na wahusika wengine wakikaa pembeni na kufanya kazi za sekretari, kukopi kumbukumbu za mikutano na ahadi za Rais. Hii haifai. Leo Dangote, kesho wawekezaji wa Ulaya, kesho wachina, wahindi, Wakenya, n.k. mpaka lini hali hii?

Sasa Ikulu ni ya wafanyabiashara, wakiitwa wawekezaji. Ni vigumu kwa mkulima mashuhuri kufika Ikulu. Rais hajakutana na kundi lolote la waajiliwa wake; iwe Jeshi, waalimu, idara ya afya, nk.

Imekuwa ni rahisi sana Dangote kufika Ikulu kujadili uwekezaji wa kiwanda kimoja tu. Kuna udhaifu gani unaotafutwa Ikulu? Ni kugawa shares za kiwanda kama tulivyowahi sikia?

Huu sasa umekuwa mtindo wa kudumu kwa marais wetu wa CCM.
 
Tunavutia wawekezaji lakini njia za kuwekeza na sheria za uwekezaji haziko ikulu! Tunazo wizara na ofisi zinazohusika. Kwa kuwa marais wetu wameamua kuwa ni waalikaji wa wawekezaji, nawaona mawaziri na wahusika wengine wakikaa pembeni na kufanya kazi za sekretari, kukopi kumbukumbu za mikutano na ahadi za rais. Hii haifai. Leo Dangote, kesho wawekezaji wa Ulaya, kesho wachina, wahindi, Wakenya, n.k. mpaka lini hali hii?

Sasa ikulu ni ya wafanyabiashara, wakiitwa wawekezaji. Ni vigumu kwa mkulima mashuhuri kufika ikulu. Rais hajakutana na kundi lolote la waajiliwa wake; iwe Jeshi, waalimu, idara ya afya, nk. Imekuwa ni rahisi sana Dangote kufika ikulu kujadili uwekezaji wa kiwanda kimoja tu! Kuna udhaifu gani unaotafutwa Ikulu? Ni kugawa shares za kiwanda kama tulivyowahi sikia? Huu sasa umekuwa mtindo wa kudumu kwa marais wetu wa CCM.
Watanzania tuna Nongwa na Unafiki tu.
 
Sukuma gang safari hii lazima muote majipu mdomoni
 
Nyie wasukuma mnapata shida Sana aisee , maana mmekua watu wa kupinga tu sasa , sijui mnapigia chepuo nani aingie ikulu , Kama magufuli hayupo tena na hawezi kuwepo tena.
Kama VIP hameni Nchi Kama walivyofanya wale waliokua hawamuelewi magufuli .
 
Magufuli alipokutana na Dangote Ikulu

Ogopa sana Technolojia, mtoa mada kule juu ana matatizo sana. Ana imani za kishamba kuwa ili kupata uwekezaji, unatakiwa na sera za NGUNGULI, mambo ambayo yamepitwa na wakati. Hizi enzi ni za utandawazi, utajikuta unaogelea peke yako. Dunia hii ni ya uwekezaji(narudia uwekezaji na siyo uchuuzi)!
Falsafa za kichuuzi na kujitenga zimeonesha kushindwa, kifo cha mende!
 
Back
Top Bottom