Kwanini Viwanja vya ndege vya Kenya ni bora kuliko Tanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Yaani baada ya kuangalia Video inayosambaa, nikashangaa Tanzania hawana Viwanja pamoja kuwa na ndege za kisasa.

Tatizo ni nini? Kwani jengo la Abiria Shilingi ngapi?

Wakenya wanawacheka Tanzania kwa dharau

Samia kazi anayo.. Hivi Magufuli kumbe hakujenga kiwanja hata kimoja

Naona aibu.
 
Hili nalo mkalitazame...

Au nasema uongo ndugu zangu?

Siiisiemu hoyeeee....
 
Yaani baada ya kuangalia Video inayosambaa, nikashangaa Tanzania hawana Viwanja pamoja kuwa na ndege za kisasa.

Tatizo ni nini? Kwani jengo la Abiria Shilingi ngapi?

Wakenya wanawacheka Tanzania kwa dharau

Samia kazi anayo.. Hivi Magufuli kumbe hakujenga kiwanja hata kimoja

Naona aibu.
View attachment 2639190
Kenya ni kimoja, Tz cha Dar hakipo, Mbeya hakipo, vyote ni vipya. Vilivyowekwa ni vya zamani vya majiji mbalimbali, nafikiri umeona hata majina, mbona Kenya hamna jina?
 
Kwa nini pamoja na kuwa na vyote hivyo bado njaa inawatandika hadi wanataka kuingia mashambani kwetu kwa lazima?
 
Gharama zinazotumika kujenga nyumba za popo ie Msalato airport zingetumika vizuri zingepatikana Airport nyingi ndogo.

Dodoma hakuna wasafiri tofauti na wafanyakazi wa serikali,wabunge
 
Hata uchumi wametuzidi
Siri ni Kuwa waKenya. wengi wapo nchi za nje. Safari za kurudi na kuondoka ni nyingi ukilinganisha na ss Tz.
Airport zao zinapata faida kwa kuwa busy.
Hapa Tz tunanyimana passport na lugha yetu ya Kiswahili tunachokienzi mashuleni hatuwexi kutengeza deal kimataifa. Tambua mmachinga wa Kenya anaongea English vizuri kuliko huyu wa Tz. Hivyo ataweza ku deal na wazungu kama sio kuondoka basi kuwakaribisha.
sasa kwa mmachinga wa Tz ataishia kuuza karanga mtaani.
 
Duh, siku nineingia na ndege Airport ya Kigoma ilikuwa balaa. Haujui kama ni nyumba ya mtu binafsi au ndio Airport yenyewe. Jamhuri yetu bado inasafari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom