Mussa Mbura: Mitambo Mipya Airport ya JNIA Sasa Inachakata Taarifa ya Passport kwa Dakika Moja Tu!

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MUSSA MBURA: MITAMBO MIPYA AIRPORT INACHAKATA TAARIFA YA PASSPORT KWA DAKIKA MOJA TU

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura amesema kuwa mitambo au mifumo ya kisasa iliyowekwa katika jengo la abiria la Terminal III katika kiwanja cha Ndege cha JNIA ni kwaajili ya usimamizi na kuchakata wa taarifa za abiria, mfumo ambao abiria anajihudumia yeye mwenyewe kwa kutumia Passport yake ya Kielektroniki ambayo imesaidia kuhudumia watu wawili ndani ya dakika moja.

"Mfumo unaitwa E-Gate au E-Border unaowezesha wasafiri hasa watanzania wanaorudi nchini kuweza kuzichakata taarifa zao na kuwaunganisha na watu wa Uhamiaji (Immigration) bila kukutana na watu wa Uhamiaji" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Kabla ya mfumo wa E-Gate kufungwa JNIA abiria alikuwa na uwezo wa kuchukua takribani dakika 30 mpaka dakika 45 kukaguliwa sehemu ya Uhamiaji (Immigration Counter) kwa abiri Mtanzania aliyetoka nchi yoyote ile kuja Tanzania. Sasa hivi mfumo unaweza kuhudumia mtu mmoja chini ya dakika moja. Hii inaokoa muda kwa abiria kuwahi majukumu yao na kurahisisha kazi kwa watu wa Uhamiaji" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Tutakubaliana kwamba katika miaka mitatu Rais Samia Suluhu Hassan shughuli nyingi za kiuchumi zimekua sana na Biashara zimekua sana, uwekezaji mkubwa unaendelea, Viwanda vingi vinaendelea. Tunaboresha huduma Airport ili kuendana na kasi ya ukuaji uchumi" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Tunaendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji na kuendelea kuiwezesha TAA kifedha zaidi" - Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
4a-1-1024x683sax.jpg
WhatsApp Image 2023-07-05 at 10.18.33 PM.jpeg
 
Pole pole tutafika tu, Hatua kwa hatua ila ncho nyingine sasa hivi karibia wanahamia kwenye system mpya ambayo hata international ambao sio watanzania wanaingia na mitambo inagonga visa moja kwa moja bila kukutana na mtu.....
 
Pole pole tutafika tu, Hatua kwa hatua ila ncho nyingine sasa hivi karibia wanahamia kwenye system mpya ambayo hata international ambao sio watanzania wanaingia na mitambo inagonga visa moja kwa moja bila kukutana na mtu.....
Tukiacha Uchawa na kuanza kufikiri kwa mapama kwa maslahi ya Taifa tutafika mapema
 
Back
Top Bottom