Habari zenu wakuu
Kumekuwa wimbi kubwa sana la vijana wasiokuwa na kazi wala vibarua mitaani zaidi ya kufanya day-work kwa kupata pesa ya kujikimu siku mbili tatu then ikiisha wanarudi tena kijiweni kwa kuangalia tena day-work na hawajui kama hilo ni tatizo kubwa sana la maendeleo yao.
Hiyo ndio inapelekea wingi wa vibaka na wapolaji wa mtaani kuanza tabia zisizofaa kwenye jamii na wazazi/walezi wao kuwaficha wanapofanya matukio kuto onyesha ushirikiano kwa polisi jamaii mpaka kwenye serikali kuu bila ya kujua kuwa mfuga mamba umtafuna mwenyewe.
Ndio haya mambo tunayoyasikia sasa hivi mara panya road mara sijui mamwitu na mawashawasha na makundi mengine ya ovyo ovyo na kupelekea kuwapoteza vijana wao kwa kuuliwa na raia wenye hasira kali kwa vitendo vyao visivyopendeza kwenye jamii mara wizi, uporaji mpaka uuaji na ubakaji.
Kazi/vibarua zipo nyingi sana ila vijana wengi wanapenda mafanikio ya haraka hawawezi kuvumilia mpaka siku za mishahara kupelekea kumuibia boss mpaka kufukuzwa makazini wamejawa na tamaa na hawajui kubana matumizi % ya vijana wengi mtaani kwenu ukiweza kuhesabu ni wajinga wajinga sana waelevu ni wachache sana wengi wavuta masigara, mabange mpaka kuwapelekea kuwa ma-adted wa maunga mpaka kuwapelekea kuwa na muonekana mbovu kushindwa mpaka kutoweza kuanzisha familia na kuilea uzuri.
Wanasababisha maisha yao kuwa magumu wao wenyewe kwa kukosa subra, uvumilivu.
Muhimu sana kuwatafuta watu wa kuwasaidia kujitambua kama wanajiona hawatoweza kujiongoza sio mpaka waharibikiwe.
Huruma sana kwa kijana/binti ukiwa haujielewi unaonekana kabsa anguko lako “ bila hata kutumia ramli au tambiko lolote.