Dah hatimae na mie nimelamba asali, baada ya mkeka wa Kaimu Katibu kucheka
usaili nilifanya mwezi wa Kwanza mwaka huu nikasahau na kusahau maana nilijua ndio basi tena sababu katika taasisi niliyoomba ina kamfumo flani hivi ka wenyewe kwa wenyewe kupeana michongo ila sasa ona jinsi Mungu alivyo mkuu mkeka umetoka nami nimo
Ile Napeleka barua ofisi nzima wananiangalia na kuniuliza maswali ya uongo na ukweli, nikasema Mungu katenda miujiza sifa na shukrani zimrejee yeye, maana katika waliopenya ni wawili tu ndio hatukuwa kwenye ofisi hiyo
Wengine wote waliobakia ama walikuwa wanajitolea au walikuwa wana mikataba hapo kwa muda mrefu tu
Acheni Mungu aitwe Mungu akiamua jambo hakuna wa kuzuia litatimia tu kwa wakati wake.
Background: niliomba mara saba nafasi mbali mbali kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo MDA na LGA, moja sikwenda kwa sababu ya kukosa nauli, mbili nilinasa kwenye written, mbili nilifika oral na ndio moja nimeitwa, na mbili bado pending kwenye mfumo nasubiri kuitwa kwa ajili ya usaili ila ndio hivyo tena mkeka ushatiki[emoji16]
Na mpaka kufanikisha Dodoma nimeenda mara 4 na simjui hata sekretari wa utumishi ni, Mungu tu kunipigania na maombi kama yote
Tusikate tamaa friends, tuendelee kupambana.