Nimesoma majibu yote uliyojibiwa kuhusu jambo lako, mimi nakushauri hivi pia.
Tafuta hela ya kutosha inayoweza kukukalisha kule kwa angalau siku 5.
Ukiripoti waulize watatumia muda gani kukuita rasmi ukaanze kazi, wakikuambia haijulikani ila watakupigia simu, nakushauri urudi nyumbani uje usubiri hiyo simu. Nauli ya Kasulu - Kibaha haiwezi kuwa kubwa na gharama utakayotumia kukaa kule kwa siku angalau 3.
Au kwa kusamaraizi, karipoti halafu rudi nyumbani, nauli ya kwenda na kurudi haiwezi kuwa kubwa ukilinganisha na gharama utakayotumia kukaa kule kwa angalau siku 3.
Reference: Case study.
Kuna mlamba Asali wa JKCI alitoka mkoani akapeleka barua, akaambiwa asubiri kupigiwa simu akakaa Dar kusubiri, zikapita wiki 2 bado hajapigiwa, hadi akakaukiwa mfukoni akaanza kulalamika(alileta uzi humu), tukaanza kumwambia alikosea, alitakiwa kurudi nyumbani kwanza.
Na wewe usije ukafanya hilo kosa.