HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kanzidata japo ina kanuni na miongozo yake ila mwajiri ndio mwenye uamuzi wa kukubaki au kukataa.

Hizi zinazotangazwa ilihali tunaona huenda kuna watu wapo kanzidata ujue mwajiri hajataka apewe kutoka Kanzi data.
Kanzidata ni kamdudu kanakofurahisha hahahaha. Mwajiri kama amekubali kupokea watu waliofanyiwa interview na utumishi kwanini akatae kanzidata. something is not clear at all. Kunyweni mtori nyama zipo chini. NEXT WEEK KUNA WATU WATAFURAHI HUMU,japo now wamekata tamaa kabisa.
 
Na kwa mfano mtu umereprt tarehe 21 mwezi X, unatakiwa kulipwa mshahara wa huo Mwezi husika au inabidi subiri mpka mwezi unaofuata?
Kinachoangaliwa sio kureport angalia barua yako ya kazi toka kwa mwajiri wako inasoma tar ngapi ndo uanze kudai mshahara kureport sio kuajiliwa
 
Wakuu kwa mtu mwenye mshahara kwa mf. 1M calculations za makato zinakuwaje? Including loarn board?
 
katibu.png

Bila shaka huwa anapitia hapa pia kuona wateja wake (watafutaji wa ajira) wanapitia kwenye changamoto zipi!!
😂😂 mmeshindikana
 
Nyie mko taasisi gani hizo per diem 100,000 taasisi nyingi naona ni 150,000, 170,000 na kuendelea kwa degree holder

Sent using Jamii Forums mobile app
per diem hutolewa kwa mujibu wa ngazi ya mshahara ya mtu. Kiwango cha chini ni 100,000/= na kiwango cha juu ni 250,000/=. Tumenukuu kiwango cha chini kwa maana ya kuwa hakuna atakayeweza kupewa chini ya hapo. Si waombaji wote wa ajira ni digrii holder na mtu anayeulizia kiwango hajasema ngazi yake ya elimu, kwa hiyo ukinukuu kiwango cha chini ni sahihi maana hawezi kupewa chini ya hapo. Hii ni baada ya Rais Samia kupandisha viwango kama inavyooneshwa hapa chini:

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.
 
Tunashkur mkuu maana wengi wetu haya mambo ni weupe.!
Hivi pesa ya kujikimu huwa inatoa halmashaur kutoka kwenye mapato yao au inatoka hazina kama ilivyo mishahara?
mbingunikwetu
Pesa yote kimsingi hutoka hazina. hata kama ikikusanywq na halmashauri mwisho wa siku hiyo pesa inaingia kwenye mfuko mkuu wa serikali lakini hesabu inaonesha kila halmashauri imekusanya kiasi gani. Matumizi ya halmashauri ni kwa mujibu wa bajeti yao na hutoka hazina (zikiwamo hizo hizo walizokusanya wao).
 
Back
Top Bottom