HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kwa hiyo ukiichukua barua psrs ndani ya wiki unapasika kuipeleka halmashaur husika ndani ya muda gani?
Na baada ya kupeleka barua halmashaur unaambiwa urudi utapigiwa simu, ni baada ya muda gani ndo wanawapigia simu??
Ukishachukuwa barua toka psrs unatakiwa kuripoti kituo chako cha ajira ndani ya siku 14 baada ya kuwa umepokea barua hiyo. Ukisharipoti kwenye kituo chako cha kazi na kujaza fomu ya personal particulars, utatakiwa kusubiri hadi utakapoitwa kwa simu!! Hawakuambii utapigiwa simu lini ila uzoefu unaonesha kuwa walio wengi hupigiwa simu baada ya siku 14, japo wengine inaenda hadi mwezi mmoja au zaidi. Ndio maana inakubidi kujipanga vizuri!!
 
Mchawi hicho cheti Cha JKT, au JKU.
Ni kweli kabisa!! Hilo sharti kusema kweli si la haki kwa mazingira ya sasa, ambapo serikali haina uwezo wa kuwapatia fursa vijana wote kupitia mafunzo ya JKT. Kila kitu huanza kwa malalamiko na kutoa hoja zenye nguvu. Mwisho wa siku serikali itakuja kuliona hilo. Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo ilikuwa kila mwajiri katika utumishi wa umma akitangaza nafasi za ajira moja ya sifa ilikuwa ni kuwa na uzoefu wa miaka angalau 2. Watu wakalalamika wakasema, huo uzoefu tutaupatia wapi kama hatuajiriwi? Mwisho wa siku hilo sharti likafutwa kwa nafasi zilizo nyingi serikalini na taasisi zake. Kwa hiyo na hili sharti la JKT likilalamikiwa na wengi lazima litatafutwa!! Ila iwe kwa yule aliyepewa fursa ya kujiunga na JKT halafu akakataa, huyo asipewe nafasi kwenye majeshi.
 
Mkuu, asante sana. Nimekuelewa vema.

Umenikumbusha jambo.
Kuna jamaa tulisoma wote Chuo kimoja, Mwaka mmoja wa masomo lakini Kozi tofauti (Yeye Kozi X, mimi Kozi Y). Huyu jamaa alikuja akapangiwa kituo cha kazi halmashauri flani kama Afisa Y (zingatia alisoma Kozi X na angeitwa kama Afisa X, lakini akaitwa kazini kama Afisa Y). Nafasi ile haikuwahi tangazwa, ingetangazwa tungeiona na ku-apply sababu tupo wengi tulo-graduate na bado ni jobless. Huyu jamaa mara kwa mara tukiwasiliana hua ninamuuliza hivi ulipataje hiyo nafasi na wakati ulisoma Kozi tofauti na hiyo nafasi, hakuwahi nijibu kabisa zaidi ya kucheka na kuleta story za mzaha. Ila nilipokaa na kutafakari nikagundua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara (kipindi jamaa ameenda kazini) inayosimamia taasisi za Kada yangu na yake alikuwa ni mtu wa jimboni kwao (kwa sasa ni Mbunge) na huenda alikuwa ni connection yake. Hizi mambo zinachanganya sana.
Hayo mambo usiyatafakari kiasi cha kukuchanganya!! Kubebana nchi hii hakuishi japo kwa kweli psrs wamejitahidi na wamebanwa sana na taratibu!
 
katibu.png

Bila shaka huwa anapitia hapa pia kuona wateja wake (watafutaji wa ajira) wanapitia kwenye changamoto zipi!!
 
Wakuu naomba kuuliza hivi hizi kazi za tutorial assistant na assistant lecturer huwa ukifaulu unatunzwa kwenye kanzidata ya waliofaulu usahili wakakosa nafasi au hazina database.
Mbona naona psrs kila mara wanarudia kuzitangaza na watu wamefanya usahili mara nying mfano udsm, udom mocu ardhi mzumbe iaa nit tia muhas kcmc irdp naona zinatangazwa many times.
Naomba ufafanuzi
 
Wakuu naomba kuuliza hivi hizi kazi za tutorial assistant na assistant lecturer huwa ukifaulu unatunzwa kwenye kanzidata ya waliofaulu usahili wakakosa nafasi au hazina database.
Mbona naona psrs kila mara wanarudia kuzitangaza na watu wamefanya usahili mara nying mfano udsm, udom mocu ardhi mzumbe iaa nit tia muhas kcmc irdp naona zinatangazwa many times.
Naomba ufafanuzi
Hawa hupenda kufanya usaili fresh wenyewe, na usaili hufanyikia vyuoni. Ukifikiri kwamba uko kwenye database utasubiri sana kama ndoto yako ni kuwa academician!! Jitose tu ukafanye tena kama ulishafanya!
 
Imagine Kitenge ndo baba yako, unakosaje kazi BOT pale[emoji3]
Ila kuna wengine ni waadilifu usipime! Kama ana sifa atatakiwa akapambane!! Na huko kwenye paper hutumika namba na si jina!! Watoto wa Nyerere walitakiwa kupambana sambamba na watoto wa watanzania wengine! Je tuna waadilifu kiasi hicho waliobakia hapa Tz?
 
Hawa hupenda kufanya usaili fresh wenyewe, na usaili hufanyikia vyuoni. Ukifikiri kwamba uko kwenye database utasubiri sana kama ndoto yako ni kuwa academician!! Jitose tu ukafanye tena kama ulishafanya!
Mbona nimeona kwenye kanuni zao zinaelezea database ya wakufunzi?
Mm hata hiyo GPA sina unaweza kuwa na ndoto Ila GPA ikakusaliti

Kuna jamaa anasema alifanya usahili hizi Kaz za tutorial chuo flan hakupata nafasi badae akaja kupangwa kwenye taasisi nzuri zaidi ya Kaz ya academician aliyoomba asa nikajiuliza Kuna ukweli au alitupiga kamba
 
Back
Top Bottom