NJAA zitawauwa vijana, acheni kujipa mioyo na kutegemea ajira za kubeti..endeleen na ishu zingine huko mtaani.
Kuna wengine kila wakitizama selections za wanaoitwa makazini wasipoona majina yao wanakasirika na kutukana, mtatukana sana, haiwezekan wote mkaajiriwa hilo muondoe akilini.
Na kuna wale wengine wao hukesha mitandaoni wakingojea hizo PDF ni kama wamejihakikishia kuwepo humo ktk hizo PDF nipende kuwaambia na ninyi mnapoteza muda wenu.
Na kuna wale wazee wa kulaum na kulalamika kila jambo, utasikia System mbovu, sjui kitu gani na gani, na ninyi pia mnapoteza muda wenu.
Nchi ina watu wengi majobless so msitegemee kila mtu kuajiriwa, ukipata chance shukuru, ukikosa kausha na fanya ishu zingine.
Tatizo lenu wasomi uchwara hamtaki kazi ngumu mitaan mnajiona special sana wacha niwape hii KWELI CHUNGU, mtajibeba acheni kujipa matumain ya kupata ajira, achen kujipa matumain ya kusubiri hizo ajira za kubeti.
Mtu unapoteza muda wako kwenda interview ya watu wanaoomba zaid ya 1000 na wanaohitajika kazini si zaid ya 100 sasa unaenda kutafta nini huko kama sio kuitaka heart break?.
Vijana niwaambien ktk nyakat za sasa ili utoboe ni either uwe na[emoji116]
Connection
Connection
Connection
Uchawi+ndumba
Rushwa+kujituma+Luckness.
Tofaut na hapo utasota sana la muhimu wajameni pigeni kazi, mmepoteza muda wenu kusoma si ili mje kuwa walalamishi na wategemezi bali kujiongeza na kujitambua nini mnatakiwa mufanye ili musurvive.
Huu ndio ukwel mchungu ambao vijana wengi humu hamuupendi.