Kwanini unaenda bar na maeneo ya starehe?

Kwanini unaenda bar na maeneo ya starehe?

Mimi huwa naenda kwa ajili ya kusikiliza mziki wenye 'vibe' pamoja na kuosha macho kwa kuona warembo walivyopendeza. Hii inaniondolea msongo wa mawazo wa kimaisha na kuendelea kutamani kuishi zaidi na zaidi.

Pia nakuwa sina muda wa kutembelea watu mbali mbali majumbani mwao, kwa sababu binadamu wa sasa wengi ni wanafiki, na kujikuta nikitembelea maeneo yaliyo changamka bila kumkwaza mtu pamoja na kutokuathiri mipangilio yangu n.k

Je wewe, kwa nini unaenda bar na maeneo ya starehe?​
Kukaa bar ni njia mojawapo ya watu wenye upweke kukabiliana na changamoto zao plus stress.
 
Kukaa bar ni njia mojawapo ya watu wenye upweke kukabiliana na changamoto zao plus stress.
Hao unaokaa nao ndani ndio wanao ongeza stress, mara watakuambia elfu 20 ulioacha asubuhi imeisha leta nyingine, mara sukari imeisha n.k
 
Halafu kuna baa kama hizi, unaenda kustarehe lakini mguu mmoja ndani mmoja nje, saa yoyote kinawaka

Halafu kuna baa kama hizi, unaenda kustarehe lakini mguu mmoja ndani mmoja nje, saa yoyote kinawaka

Nenda bar/club ambazo zina ulinzi, pia kama wewe ni mtu wa fujo wa kung'ang'ania watoto wazuri wa wengine, kule hakukufai.​
 
Maendeleo ni kununua kilo 50 za sukari kwa pamoja.
Sio kila week unanunua kilo moja moja
Toka leo ukaoshe macho
leo3.jpg
 
Back
Top Bottom