Kuna sehemu ya maelezo yako unachukua propoganda za Putin ambazo siyo kweli. Ukraine haikuwauwa watu wanoongea kirusi bali hizo ni propoaganda za Putin tu. Mgogoro wa Ukraine ulianza mwaka 2013 wakati rais wa Ukraine wakati huo Viktor Yanukovych alipokataa kusaini makubaliano ya Ukraine kuingia kwenye European Union kwa kufuata maelekezo ya Putin. Wananchi wa ukraine waliandamana mfululizo mitaani na kwa karibu miezi minne nchi ikawa haitawaliki, ikabidi bwana Yanukovych akimbie nchi na kukimbilia Urusi ambako ndiko amekuwa anaishi siku zote. Yanukovych ni mtu anyetoka maeneo hayo ya mashariki yanyoongea kirusi, hivyo kama ni kweli kuwa walikuwa na uhasama na watu wanoongea kirusi, jamaa huyo asingeweza kufikiwa kuwa rais wa nchi.
View attachment 2186750
Baada ya mapinduzi hayo ya wanachi yaliyomuondoa Viktor Yanukovych ndipo Putin akavamaia na kumega eneo la Crimea, halafu akawapa asiakri watu wa mashariki wapinge serikali ya Kyiv kusidi wajitenge wawe karibu na urusi. Sasa mapigano hayo ya mashariki yaliyoanzishwa na Putin mwenyewe ndiyo amekuwa anadai kuwa watu wanoongea kirusi wanauwawa.
Putin ana tatizo na kupanua sphere of influence kwa nguvu, bado anatamani Soviet Union irudi. Kila nchi ambayo haikubalini naye amakeuwa anatafuta makundi yanayoongea kirusi na kuyapa silaha kufanya vurugu halafu anayaita independent republic na kuyangunaisha kwenye reussian federation. Amefanya hivyo Georgia, Azerbaijan na sasa Ukraine.