Zelesky aendelea kupoteza muda

Zelesky aendelea kupoteza muda

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,837
Reaction score
8,198

​

.

Chanzo cha picha,Getty Images
Marekani imeidhinisha uuzaji wa makombora 500 aina ya Patriot kwa Ukraine, ambazo ni silaha muhimu za kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameonya kuwa huenda ikachukua "miaka kadhaa" kabla ya makombora hayo kufika nchini humo.
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imesema makombora hayo ya kisasa ya kuzuia mashambulizi ya angani, aina ya PAC-3, yana thamani ya dola bilioni 2.1 na kwamba gharama yake italipwa kikamilifu na washirika wa Ukraine barani Ulaya na Canada.
Zelensky amerudia wito wake kwa Marekani kuharakisha kutoa mifumo yake ya makombora ya Patriot, ambayo ndiyo silaha pekee yenye uwezo wa kuzuia makombora hatari ya Urusi aina ya ballistic.
Hatua hii ya hivi karibuni imekuja kufuatia mvutano kati ya Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump mapema mwezi huu, baada ya Marekani kulegeza vikwazo dhidi ya Urusi kama sehemu ya makubaliano ya kupata mafuta ya dizeli kutoka Urusi.
Trump aidha alisema ni wakati mwafaka kwa Ukraine kupata kiongozi mpya ambaye anaweza kufanikisha makubaliano ya kumaliza vita na Urusi.
Urusi ilianzisha uvamizi mkubwa nchini Ukraine mwezi Februari mwaka 2022, baada ya awali kuteka eneo la Crimea na baadhi ya maeneo ya Donbas mashariki mwa Ukraine.
 
Back
Top Bottom