Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

sa kama ni hvo kwann hao wanga wasijiupdate version yao wanaotumia ili wakikuta umelala vyvyte wafanye yao tu
 
Hapana ukiwa kwenye mlalo mzuri I mean mshazari ni ngumu sana mwanga kufanya yake... Ni mpaka aidha uwe chali ama kifudifudi... Sana sana atasonya na kuondoka zake
Bwana kusonya inahusiano gani na wachawi au majini?? Nakumbuka zamani tulikuwa tunakatazwa kufanya hivyo
 
Hilo sio jibu lake..... Nimekuuliza kipimo ulichotumia kupata analysis yako... Jibu hilo kwanza mengine yatafuata
Milango mitano ya fahamu hupata ganzi baada ya mtu kulala kabisa. Mtu akilala fofofo mwili huachia homoni inayofanya milango hiyo ya fahamu kufa ganzi yaani haifanyi kazi kwa asilimia 100.

Ukiona mtu amelala alafu baada ya wewe kumuangalia usoni akaamka ujue hakulala kwa Asilimia Mia Bali alifumba macho. Pia mwili wake haukuachia homoni ya kuupa mwili ganzi kwa Asilimia 100.

Huo ni Uzushi kabisa.
 
Milango mitano ya fahamu hupata ganzi baada ya mtu kulala kabisa. Mtu akilala fofofo mwili huachia homoni inayofanya milango hiyo ya fahamu kufa ganzi yaani haifanyi kazi kwa asilimia 100.

Ukiona mtu amelala alafu baada ya wewe kumuangalia usoni akaamka ujue hakulala kwa Asilimia Mia Bali alifumba macho. Pia mwili wake haukuachia homoni ya kuupa mwili ganzi kwa Asilimia 100.

Huo ni Uzushi kabisa.
Naona umeshindwa kabisa kujibu swali ama la hukuelewa
 
Maandiko matakatifu yanasema kwamba tuna malaika ambao ndio walinz linapotokea jambo la hatari hakuna andiko linalozungumzia jicho la tatu na hiyo ipo tofauti nijuavyo mimi mtu akiwa anakuangalia kwa kukukazia macho ukiwa mahala fulani kuna hali flani inakushitua angalia kulia au kushoto ndio unapoona mtu au kitu kimekutolea macho na sio ukiwa umelala
 
Ni sayansi gani hii? Ni uchawi!? Ni mazingaombwe ama ni jambo la kufikirika tu lisilo na ukweli wowote?

Niliahidi kuleta mada hii, baada ya Dr. Shika kuchagiza kwenye simulizi yake ya kutoroka watesi wake kwamba hakumwangalia yule mtesi mlinzi aliyebaki naye machoni la sivyo jamaa angeamka!

Tujadili kipengele kwa kipengele.

A. Kwenye mada zilizopita za jicho la tatu, majinamizi na jicho la rohoni tuliona jinsi jicho la tatu lilivyo na nguvu pale macho yaonekanayo yakiwa yamefumba, yamelala.. Kumbuka jicho la tatu liko kwenye paji la uso.. Tunapozungumzia mawasiliano ya kiroho kiunganishi ni jicho hilo la tatu kwamba kuna muunganiko usioonekana kati ya jicho la tatu na jicho la tatu lingine...
Kama nilivyosema kwenye mada ya majinamizi na ndoto mbaya hatushauriwi kulala chali kwakuwa juu yetu zinapita roho nyingi na za kila aina, ambazo connection yake ni jicho hilo la tatu

B. Wachawi na wanga hutumia sana jicho la tatu kufanya mawasiliano ya kiroho na ndio maana wanapotaka kuingia ndani ya nyumba kwanza kuingia kinyume nyume kwa rivasi na wakiwa uchi... Hapa ni kuepusha uwezekano wowote wa wewe kuna na direct connection ya jicho la tatu na yeye... Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake... Lakini kwakuwa tayari ile connection ishakuwa established basi subconscious mind inakuwa alert na ndio mwanzo wa kukabana..
Jiulize kwanini wanaoingiliwa na popobawa hawana kipingamizi chochote, hujikuta tayari washachafuliwa..

C. Muingiliano mwingine wa jicho la tatu ni ndege kunguru mwewe, huyu ni ndege mwerevu na mwepesi sana huwezi kumpiga akiwa mbali, hivyo wajuzi huenda kinyume nyume mpaka kumkaribia kabisa ndio hugeuka na kumpelekea moto... Ukiweza kurudi rivasi kwa kunyooka, unaweza kumkaribia kunguru mpaka umbali wa mita tano.. Unaweza kufanya majaribio

D. Mwili wetu huu una mashine tatu moja ni conscious mind na nyingine ni subconscious mind na ya tatu ni unconscious mind
-conscious mind- ni hii hali tuliyo nayo ya kuweza kufanya kila kitu kwa utashi na bila utashi, kuandika kuongea kuvaa nguo nk nk, ni katika hali hii subconscious mind (jicho la tatu) nayo hufanya kazi.. Hii hufanya kazi ya ulinzi kuzunguka mwili wote na ndio maana huwa tunahisi kuna mtu anatunyemelea, kuna mtu yuko nyuma yetu ama kuna hatari inatukaribia.. Lakini vilevile hufanya kazi ya machale... Jicho la tatu huona zaidi ya kuona (seeing beyond) huwa tunapewa tahadhari na nafsi zetu, huwa tunasita kufanya jambo . hii ni kazi ya subconscious mind... Halafu kuna hali ile ya kuzirai ama kupoteza fahamu... Hii ndio unconscious mind... Macho yote mawili yamezima, jicho la tatu nalo linakuwa kwenye dormance state.. Lipo lakini utendaji hupungua uwezo mpaka kufikia chini ya asilimia 50 ili kulinda uhai kidogo uliobakia. Ni sawa na kukipunguzia mizigo chombo baharini kinachokaribia kuzama ili kisizame

Sasa tuhitimishe kwa suala la Dr Shika, aliachwa na mlinzi lakini akalala kutokana na uchovu pombe na madawa.. Lakini kwakuwa tayari ana ufahamu (inbuilt intuition) wa kumlinda Dr, hivyo hata alale vipi lile jukumu kiroho hubaki kwenye subconscious mind/jicho la tatu na ikitokea ukamwangalia usoni una establishe connection kati yako na yeye na kumfanya ashtuke na kuamka
ef5089328ced34d6ad19285ea79b58d6.gif


Mojawapo ya mafunzo ya walinzi ni hili.. Na subconscious mbili zinapokutana moja ndio hu trigger nguvu ya kuamsha nyingine.. Hivyo haishauriwi kabisa kukutanisha macho Kwenye situation kama hizi

Naomba radhi kwa kuchanganya lugha
Mkuu jaribu Sikh moma kwenda kuiba Mlinzi akiwa amelala halafu usimwangalie usoni ili utupe mrejesho tujue kilichoendelea ni kweli ukimwangalia aliye lala ataamka au ni stories tu
 
Zamani kipindi nasoma ilikua nachelewa sana kufua nguo za shule, nakama ikitokea nimeaziacha zilale nje kwenye kamba ilizikauke hio siku nalala chali kulinda ili niwahi kushtuka kma mvua itanyesha nahaijawai kutokea nkakosea timing zikanyeshewa
 
Mkuu jaribu Sikh moma kwenda kuiba Mlinzi akiwa amelala halafu usimwangalie usoni ili utupe mrejesho tujue kilichoendelea ni kweli ukimwangalia aliye lala ataamka au ni stories tu
Mimi sio mwizi Kwahiyo sitaweza kufanya hivyo
 
Hakuna ukweli wowote. Fix tu.
Jambo kama hili simple sana kuprove. Sijawahi kuangalia mtu usoni akiwa kalala akaamka, wengine hadi nawagusa kabisa bado wamelala.
Kama kawaida conspiracy theorists watajaa hapa na kushangilia kitu kipya bila kushughulisha bongo zao hata kidogo. Story hii haina basis yoyote ile, tungo tu
watu kama nyinyi ndio mnasemaga hakuna uchawi halafu ghafula mtt wako analipuka mapepo hapo ndipo mnanyooshwa......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom