Haiwezekani kivuko kilichoghraimu bil 7.3 kukarabatiwa kwa bil 4.4

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Pesa za umma zinaliwa huku wananchi wakiteswa na tozo.

Kivuko 1.PNG

==
Ujenzi wa kivuko cha Mv Kazi uligharimu Sh7.3 bilioni na kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 sawa na jumla ya tani 170.

Kupitia Ukurasa wa twitter wa TEMESA wamesema Kivuko cha MV. KAZI kimerejea rasmi katika eneo la Magogoni Kigamboni kwa ajili ya kutoa huduma baada ya kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.4. Kivuko hicho kiliondolewa kwenye maji baada ya kufikia muda wake wa ukarabati mkubwa.

Kilianza rasmi kukarabatiwa mwezi Juni mwaka 2022 na mkandarasi Songoro Marine Transport Boatyard katika Yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (5) 2020-2025,

Serikali inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan ilitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kuboresha huduma za vivuko hapa nchini ili kuwapunguzia wananchi kero za usafiri wanazopata katika maeneo mbalimbali kupitia Wizara mbalimbalina kupitia Wizara ya Ujenzi, Serikali imeanza kutekeleza ahadi hizo kwa kuanza kuvifanyia ukarabati vivuko hivyo.
 
Pesa za umma zinaliwa huku wananchi wakiteswa na tozo.
View attachment 2479430View attachment 2479429
Hakuna wakati ufisadi ulishawahi kuisha kwenye uongozi/ awamu yeyote ile. kilichopo kwa mpandisha uzi ni nongwa na kutaka kuonekana ana uchungu na nchi kumbe amepigwa tu na kitu kizito hapo 17/3/2021
ununuzi wa ndege chini ya chini ya chizi magufuli ulikuwa nn kama siyo ufisadi?

ujenzi wa uwanja wa ndege wa chato ilikuwa nn kama siyo ufisadi?

sukuma gaaang kaeni kwa kutulia watu washamaliza kazi
matusi ruksa
 
Embu acha kuichafua serikali yetu Kama huna ushahidi, je wewe Ni Fundi? Una utaalamu na matengenezo take? Umewahi kutengeneza kivuko Cha aina hiyo? Unafahamu kilichokuwa kinatengenezwa?

Kwa uelewa wako unaweza kutusaidia hapa jukwaani na kutuwekea ushahidi na mchanganuo inayoonyesha gharama halisi ambazo zilitakiwa kutumika? Unaweza kutwambia Ni vifaa vipi na vipi vilivaribika na gharama yake Ni shillingi ngapi?

Usiandike kwa hisia pasipo kuwa na taarifa kamili na inayoonyesha mchanganuo mzuri wa kuonyesha kuwa watanzania tumeibiwa ili tujuwe namna tukivyoibiwa kwa kutuwekea mchanganuo.
 
Kuna uwezekano kilitengenezwa kulingana na pesa iliyokuwepo ila maintenance cost yake ni kubwa. Waweza kuta engine zake zilikuwa za bei ya chini ila maintenance cost yake ni kubwa na life span yake ni fupi. Rejea simu tunazotumia.
Tukijua ni maintenance zipi zimefanyika itakuwa rahisi kufanya ulingalifu
 
Hakuna wakati ufisadi ulishawahi kuisha kwenye uongozi/ awamu yeyote ile. kilichopo kwa mpandisha uzi ni nongwa na kutaka kuonekana ana uchungu na nchi kumbe amepigwa tu na kitu kizito hapo 17/3/2021
ununuzi wa ndege chini ya chini ya chizi magufuli ulikuwa nn kama siyo ufisadi?
ujenzi wa uwanja wa ndege wa chato ilikuwa nn kama siyo ufisadi?
sukuma gaaang kaeni kwa kutulia watu washamaliza kazi
matusi ruksa
Ona mavi kama haya nayo yapo yanatetea huu utawala wa hangaya
 
Embu acha kuichafua serikali yetu Kama huna ushahidi, je wewe Ni Fundi? Una utaalamu na matengenezo take? Umewahi kutengeneza kivuko Cha aina hiyo? Unafahamu kilichokuwa kinatengenezwa? Kwa uelewa wako unaweza kutusaidia hapa jukwaani na kutuwekea ushahidi na mchanganuo inayoonyesha gharama halisi ambazo zilitakiwa kutumika? Unaweza kutwambia Ni vifaa vipi na vipi vilivaribika na gharama yake Ni shillingi ngapi?

Usiandike kwa hisia pasipo kuwa na taarifa kamili na inayoonyesha mchanganuo mzuri wa kuonyesha kuwa watanzania tumeibiwa ili tujuwe namna tukivyoibiwa kwa kutuwekea mchanganuo.
Ni aibu sana kwa mtu kama wewe kuwa hivi!

Hivi ile familia yako wanakuonaje?
 
Siku hizi wakizipiga ni kuanzia B
Nilinunua tv Samsung 2012 kwa tsh 650000,siku chache baadae nikapasua kioo,kwenda kuuliza Bei kioo ilikua 450000,nikajiuliza ninunue kioo au niongezee pesa ninunue mpya,kwenye kivuko hapo ni heri tungepekua zaidi hizo gharama Kama walivyoainisha wao,kivuko Cha juzi tu kwa nini kifanyiwe ukarabati!?..Pana jambo
 
Back
Top Bottom