Kwanini TBC wanatulazimisha kusikiliza kila dakika Habari ya Libya na Iraq?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Kuna nini?

Kwanini TBC1 wana tangazo moja tu la Historia ya Libya na Iraq, kuna nini huku kwetu, wanatengeneza mazingira au ni kampeni, mwenye uelewa atujulishe maana, kwangu binafsi sina Histora yoyote ya ACT wala CHADEMA kuwateka wanachama wa CCM na kuwaua sina kabisa, huenda wengine wana historia ya wengine kuwaua wengine.

Kujuzane hatuelewi kabisa.
 
Sijaelewa Kabisa, ina maana TBC1 sio ya serikali ya vyama vyote bali ni ya chama kipi maana sijaelewa ubaguzi huu. kama ni kweli basi kuna mabadiliko tunahitaji watanzania. flavour ya pande zote muhimu sana kuipata
 
Wanadhani Tanzania kutatokea machafuko ambayo mara nyingi husababishwa na uchu wa madaraka na kuongoza kwa kuto fuata sheria
Kwani nani anahisiwa atasababisha machafuko, walio anzisha mauwaji ya wanasiasa ni nani huenda kuna jibu kwa hili sio watu kuwa waoga tu, au wanajihisi kuna kulipa kisasi
 
Kwa hotuba Kama za kina lissu unafikiri wataonyesha nini..?
Au unapenda kusikia ile michambo na Tambo zakisiasa..😂
 
Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, kama halipo kwanini wanatulazimisha tuendelee kulisikiliza? sisi tuna amani hatupo huko wala hatuna haja ya kuambiwa si tumeyaona kwann walazimishe yaingie masikioni mwetu. Ryoba (MKURUGENZI WA TBC)naye sijui nini kimemkuta
 
TBC inahitaji marekebisho makubwa sana, TV ya umma inayotumika na ccm pekee.Ccm wanachokifanya sio uzalendo kwa taifa letu
 
Na wewe jamaa, unatoka wapi kutazama huo utopolo, kama kifurushi kimeisha si uweke channel no 100 utazame matangazo ya katuni na sinema tu...!!
 
Kuna nini? Kwanini TBC1 wana tangazo moja tu la Historia ya Libya na Iraq, kuna nini huku kwetu, wanatengeneza mazingira au ni kampeni, mwenye uelewa atujulishe maana, kwangu binafsi sina Histora yoyote ya ACT wala CHADEMA kuwateka wanachama wa CCM na kuwaua sina kabisa, huenda wengine wana historia ya wengine kuwaua wengine.

Kujuzane hatuelewi kabisa.
nimeona wanaonesha ile hotuba ya MAGU akizungumzia issue za GADAFI sijui ujinga wao utaisha lini
 
Kuna nini? Kwanini TBC1 wana tangazo moja tu la Historia ya Libya na Iraq, kuna nini huku kwetu, wanatengeneza mazingira au ni kampeni, mwenye uelewa atujulishe maana, kwangu binafsi sina Histora yoyote ya ACT wala CHADEMA kuwateka wanachama wa CCM na kuwaua sina kabisa, huenda wengine wana historia ya wengine kuwaua wengine.

Kujuzane hatuelewi kabisa.
Pale TBC pana mpumbavu mmoja anaitwa Shaban Kisu ndiye kilaza wa ku engineer huo ujinga!
 
Nipo huku lindi kwenye nanane pita pita zangu kwenye nimesikia redio moja jina kampuni na maharufu huku kusini hasa hapa lindi mjini nimesikia nyimbo ikiimba mungu ibariki Tanzania mungu ibariki magufuli. Eeeh unajua nimeshituka maana pole pole na msajili wa vyama vya siasa wanatuhumu chadema kwanini umeongeza ubet kwenye nyimbo yetu pendwa ya taifa
 
Back
Top Bottom