Nidhamu na umoja ndani ya CCM Ndio msingi na nguzo ya ushindi katika kila uchaguzi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,289
9,720
Ndugu zangu Watanzania,

Uwepo wa CCM madarakani kwa miaka mingi ni matunda ya nidhamu na umoja uliotamalaki ndani ya CCM na miongoni mwa wanachama wake. Nidhamu ya kuheshimu maamuzi halali ya vikao vya chama,nidhamu ya kujizuia kuzungumza chochote katika jambo linalohitaji maamuzi na kauli ya chama.

Nidhamu ya kujuwa kama hujaridhishwa na jambo unatakiwa upeleke kwenye vikao vya chama,nidhamu ya kukosoana kwa staha na kwa hoja za ukweli ndani ya vikao rasmi vya chama,nidhamu ya kujuwa majukwaani au mitaani siyo mahali pa kushambuliana wao kwa wao, na nidhamu ya kutambua mipaka ya kila mtu katika kuzungumzia au kutolea ufafanuzi wa jambo fulani.

Chunguza taasisi zote zilizofanikiwa Duniani au nchi zote zilizopiga hatua za kimaendeleo utakuta msingi wa mafanikio yao ni nidhamu tu katika yale wayafanyayo au kupanga na kuyaadhimia kutekeleza.Embu jiulize jeshini kama kungekosekana nidhamu hata kwa siku moja tu nini kingetokea? Nini kingetokea ikiwa wanajeshi wangepinga amri ya kiongozi wa juu?

Lakini kutokana na nidhamu iliyojengeka ndani ya majeshi ndio maana askari akipewa amri ya kufanya jambo fulani ni lazima atekeleze kwanza na siyo kuanza kuhoji uhalali wa amri hiyo.ndio maana unaona majeshini nidhamu ni nguzo namba moja itakayokufanya askari kuendelea kusalia kikosini.

Ndio maana ukija ndani ya CCM Hata kwenye vikao vyake tu vya ndani hata pasipo kuambiwa unatambua kabisa huyu ni kiongozi wa hapa na huyu ni mwanachama.ndani ya CCM Kila mwanachama anaheshimu maamuzi ya chama,maagizo ya chama na kila mtu anayetekeleza vyema.huwezi ukakuta ndani ya CCM mtu anajijenga binafsi au kujiona mkubwa kuliko chama.kila mtu anajuwa chama ni kikubwa kuliko mtu na maslahi yake.

Tofauti na vyama vya upinzani kama CHADEMA unakuta kila mtu anaongea tu kana kwamba yeye ni mwenyekiti au makamu au katibu,unakuta ndani ya CHADEMA mtu yupo zake huko sumbawanga amejiamkia zake asubuhi na pombe zake kichwani anaita vyombo vya habari na kuanza kuzungumza kwa kujivika koti la chama.

unakuta ndani ya CHADEMA kwa kuwa mtu ana bando basi anaingia mtandaoni anachapisha habari yake na kuiweka katika sura ya chama kana kwamba chama kilifanya kikao na kumpa yeye akisemee maazimio yake au msimamo wake juu ya jambo fulani.

Mambo kama haya ya kukurupuka yanakiathiri chama kwa kuwa wanachama wanakuwa na misimamo tofauti tofauti hata kabla ya vikao rasmi vya chama,ambapo hata wakienda kwenye vikao rasmi kila mtu anakuwa ameingia kwenye vikao au anataka misimamo au mtizamo wake ndio uwe wa chama ili asije onekana amekula matapishi yake juu ya kile alichokwisha kiandika mtandaoni.

Ndio maana kutokana na kukosekana kwa nidhamu ndani ya vyama vya upinzani kunakuwa na madaraja ya wanachama ,ambapo wengine wanajiona ni bora sana kuliko wengine na wana akili sana na wanapaswa kusikilizwa kwa kila kitu na haitakiwi hata kidogo kuwakosoa kwa mitizamo yao.

Hawa wanaojiona bora kwa kukosa kwao nidhamu unakuta wanaandika mambo mengi kwa kukurupuka na kuyavisha nembo au mwamvuli wa chama.yaani upinzani hakuna cha mkubwa wala mdogo,hakuna cha kujuwa mipaka wala ukomo wa mdomo wako wala wapi unapaswa kuishia kuzungumza juu ya jambo fulani,wala nani ni kiongozi au msemaji wa chama.

Ndio maana CCM Inaendelea kuwa chama tegemeo sana na Tumaini la mamilioni ya watanzania,ndio maana Inaendelea kuwa chama kiongozi na mfano wa kuigwa barani Afrika na iliyosimama imara .Hii yote ni kutokana na nidhamu iliyopo ndani yake. hata familia iliyokosa nidhamu haiwezi kusimama imara na ikaheshimika kwa majirani zake. Na pia haiwezi ikapata maendeleo ya aina yoyote ile ,maana haina umoja wenye kuongozwa na kinidhamu.

Vyama vya upinzani kama CHADEMA vina safari ndefu sana kuifikia CCM ilipo leo hii na vitakapo fika ilipo CCM Leo hii basi CCM itakuwa imehamia hatua nyingine ya juu zaidi.kwa hiyo ni wazi kuwa CCM itaendelea kuongoza Taifa letu Daima na huwezi ukalitenganisha Taifa au Tanzania na CCM.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Jana waziri Simbachawene amelalamika nchi imejaa rushwa kila kona, alafu wewe unasifia?
Ni wajibu wake kuchukua hatua maana yeye ni waziri.sasa yeye akilalamika anataka wananchi wa kawaida tufanye nini sisi wakati yeye ndiye anavyombo vyote vinavyolipwa mishahara inayotokana na kodi zetu wananchi kwa ajili ya kushughulikia mambo kama hayo ya rushwa na ufisadi.
 
CCM ina nidhamu?..

Sidhani kama mnafanyaga survey mtaani kupima kukubarika au kutokukubarika kwa CCM.
Watanzania wengi wameichoka CCM na kuzipuuza siasa maana ndio option pekee iliyobaki maana upinzania ni kama haupo.

CCM walichofanyikiwa mpaka sasa ni kuwafanya watanzania mateka kwa kuzuia kwa nguvu zote kila aina ya upinzani unaoweza kuwaamsha Watanzania na hatimaye watanzania wawe na option B.
 
Ukija mitaani CCM Ina aminika , kukubalika na kupendwa sana.ndio maana Inaendelea kuchaguliwa katika kila uchaguzi unaofanyika hapa Nchini
 
I'll we Faza wewe.
Unaweza kuiga tabia za Chama chako ukazileta nyumbani kwako kuendesha familia tuone itakuaje ?
 
CCM ipi? Wabunge wanalia bungeni kwba mafisadi hayachukuliwi hatua. Na pia Waziri wa Utawala Bora analia serikali imejaa rushwa. Nidhamu gani unaongelea?. Halafu CCM imeshinda lini kiuhalali ? Zaidi ya goli la mkono.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uwepo wa CCM madarakani kwa miaka mingi ni matunda ya nidhamu na umoja uliotamalaki ndani ya CCM na miongoni mwa wanachama wake. Nidhamu ya kuheshimu maamuzi halali ya vikao vya chama,nidhamu ya kujizuia kuzungumza chochote katika jambo linalohitaji maamuzi na kauli ya chama.

Nidhamu ya kujuwa kama hujaridhishwa na jambo unatakiwa upeleke kwenye vikao vya chama,nidhamu ya kukosoana kwa staha na kwa hoja za ukweli ndani ya vikao rasmi vya chama,nidhamu ya kujuwa majukwaani au mitaani siyo mahali pa kushambuliana wao kwa wao, na nidhamu ya kutambua mipaka ya kila mtu katika kuzungumzia au kutolea ufafanuzi wa jambo fulani.

Chunguza taasisi zote zilizofanikiwa Duniani au nchi zote zilizopiga hatua za kimaendeleo utakuta msingi wa mafanikio yao ni nidhamu tu katika yale wayafanyayo au kupanga na kuyaadhimia kutekeleza.Embu jiulize jeshini kama kungekosekana nidhamu hata kwa siku moja tu nini kingetokea? Nini kingetokea ikiwa wanajeshi wangepinga amri ya kiongozi wa juu?

Lakini kutokana na nidhamu iliyojengeka ndani ya majeshi ndio maana askari akipewa amri ya kufanya jambo fulani ni lazima atekeleze kwanza na siyo kuanza kuhoji uhalali wa amri hiyo.ndio maana unaona majeshini nidhamu ni nguzo namba moja itakayokufanya askari kuendelea kusalia kikosini.

Ndio maana ukija ndani ya CCM Hata kwenye vikao vyake tu vya ndani hata pasipo kuambiwa unatambua kabisa huyu ni kiongozi wa hapa na huyu ni mwanachama.ndani ya CCM Kila mwanachama anaheshimu maamuzi ya chama,maagizo ya chama na kila mtu anayetekeleza vyema.huwezi ukakuta ndani ya CCM mtu anajijenga binafsi au kujiona mkubwa kuliko chama.kila mtu anajuwa chama ni kikubwa kuliko mtu na maslahi yake.

Tofauti na vyama vya upinzani kama CHADEMA unakuta kila mtu anaongea tu kana kwamba yeye ni mwenyekiti au makamu au katibu,unakuta ndani ya CHADEMA mtu yupo zake huko sumbawanga amejiamkia zake asubuhi na pombe zake kichwani anaita vyombo vya habari na kuanza kuzungumza kwa kujivika koti la chama.

unakuta ndani ya CHADEMA kwa kuwa mtu ana bando basi anaingia mtandaoni anachapisha habari yake na kuiweka katika sura ya chama kana kwamba chama kilifanya kikao na kumpa yeye akisemee maazimio yake au msimamo wake juu ya jambo fulani.

Mambo kama haya ya kukurupuka yanakiathiri chama kwa kuwa wanachama wanakuwa na misimamo tofauti tofauti hata kabla ya vikao rasmi vya chama,ambapo hata wakienda kwenye vikao rasmi kila mtu anakuwa ameingia kwenye vikao au anataka misimamo au mtizamo wake ndio uwe wa chama ili asije onekana amekula matapishi yake juu ya kile alichokwisha kiandika mtandaoni.

Ndio maana kutokana na kukosekana kwa nidhamu ndani ya vyama vya upinzani kunakuwa na madaraja ya wanachama ,ambapo wengine wanajiona ni bora sana kuliko wengine na wana akili sana na wanapaswa kusikilizwa kwa kila kitu na haitakiwi hata kidogo kuwakosoa kwa mitizamo yao.

Hawa wanaojiona bora kwa kukosa kwao nidhamu unakuta wanaandika mambo mengi kwa kukurupuka na kuyavisha nembo au mwamvuli wa chama.yaani upinzani hakuna cha mkubwa wala mdogo,hakuna cha kujuwa mipaka wala ukomo wa mdomo wako wala wapi unapaswa kuishia kuzungumza juu ya jambo fulani,wala nani ni kiongozi au msemaji wa chama.

Ndio maana CCM Inaendelea kuwa chama tegemeo sana na Tumaini la mamilioni ya watanzania,ndio maana Inaendelea kuwa chama kiongozi na mfano wa kuigwa barani Afrika na iliyosimama imara .Hii yote ni kutokana na nidhamu iliyopo ndani yake. hata familia iliyokosa nidhamu haiwezi kusimama imara na ikaheshimika kwa majirani zake. Na pia haiwezi ikapata maendeleo ya aina yoyote ile ,maana haina umoja wenye kuongozwa na kinidhamu.

Vyama vya upinzani kama CHADEMA vina safari ndefu sana kuifikia CCM ilipo leo hii na vitakapo fika ilipo CCM Leo hii basi CCM itakuwa imehamia hatua nyingine ya juu zaidi.kwa hiyo ni wazi kuwa CCM itaendelea kuongoza Taifa letu Daima na huwezi ukalitenganisha Taifa au Tanzania na CCM.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Hakika hilo halina ubishi!
 
CCM ipi? Wabunge wanalia bungeni kwba mafisadi hayachukuliwi hatua. Na pia Waziri wa Utawala Bora analia serikali imejaa rushwa. Nidhamu gani unaongelea?. Halafu CCM imeshinda lini kiuhalali ? Zaidi ya goli la mkono.
Uwe na subira maana serikali ya Rais samia haina subira wala uvumilivu kwa wala rushwa na mafisadi.ndio maana unaona kuna wakurugenzi wamesimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
 
Back
Top Bottom