Tuanzie hapa 1. Nani aliyetoa tafiti hiyo 2. Wametumia vigezo gani 3.Tunajuaje uhusiano wa majasusi waliotoa tafiti hii na nchi kama Somalia au nyingine 4. Kiufupi hakuna Taifa lolote la afrika ambalo linafulaa sema We pretend to be happy....Natumaini ni kwema wakuu.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).
Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Nilitaka kuandika ila nikahisi itakuwa ndefu sana ila huu ndio ukweli.Furaha hiyo inatokea wapi? Kwa mikasa ya nchi yetu, unaishi dar na unatumia mwendokasi jua furaha haiwezi kuja, umefungua biashara yako ya kuna kodi msururu furaha huwezi kupata, ripoti ya kagi inatoka unasikia kuna trillions za pesa zimefanyiwa manjengeka kisha watu wanachekeana furaha hauwezi kuipata, unasoma wee una degree ya udaktari unaambiwa uende veta furaha unaipatia wapi, unasikia gesi imegunduliwa dhiki za taifa zinaishia hapo, anakuja kiongozi mwingine anaongea memgina furaha haiwezi kuja.
Mwendazake alikopa na miradi ya SGR, bwawa la umeme n.k ilionekana leo hii pesa imekopwa karibia trilioni 30+ na hakuna cha maana.
We mshahara wako laki 7 unalipia usafiri, kodi ya nyumba, afya, na kila kitu.
Kuna mtu ni anapokea milioni 5 kwenda juu kila kitu kwake ni free, hata gharama ya mafuta hajui, mpaka beki 3 analipiwa na ananiamulia tu kusema
"kama hamuwezi hamieni burundi
" hata mkila nyasi ndege ya raisi itanunuliwa
"kama hamuwezi kulipia, pigeni mbizi.
" umeshindwa kulipa 50k ya kujifungulia kamwambie mumeo achukue mkasi akuzalishe.
Nchi ya watu waongo mpaka wanajidanganya wao wenyewe na kukubali uongo wao haiwezi kuwa na furaha.
Achana na huo utafiti Mkuu wewe unaona watu kama wanafuraha?Tuanzie hapa 1. Nani aliyetoa tafiti hiyo 2. Wametumia vigezo gani 3.Tunajuaje uhusiano wa majasusi waliotoa tafiti hii na nchi kama Somalia au nyingine 4. Kiufupi hakuna Taifa lolote la afrika ambalo linafulaa sema We pretend to be happy....
Piga chini chama kiiziNini kifanyike kubadili hii hali?
Hakika.Ni mwaka muafaka wa kutafuta competent leader.
Nimelia sanaHata ingekuwa ni wewe blooo ungekuwa na furaha kweli?
Nchi kina Madelu wanajitungia nyuzi eti wanapigwa vita wakati wamepaisha uchumi, nchi ukiamka asubuhi unakuta mtu wa miaka 85 kachaguliwa makamo mwenyekiti wa chama kisa ni mtu wao, nchi ambayo mtu unajipinda miaka 4 kwa shida na dhiki kuu unamaliza degree ya civil engineering alafu unaambiwa haya sasa nenda veta kasomee ufundi uashi
Bloo hata ingekuwa wewe ungekuwa na furaha kweli?
Tunaanzia wapi, kenge hawa wamejiwekea mizizi.Tuitoe CCM madarakani
Ni sahihi kabisa. Zamani kidogo mwanzo wa Azimio la Musoma-1974, vijana - ambao ndo nguvu ya Taifa lolote duniani, walipitia mafunzo ya JKT (mujibu wa sheria na kujitolea) kwa mwaka 1. (mwaka mmoja) na huko walipata mafunzo ya kina na Hamasa iliyoujenga na kuchochea uzalendo wao kwa Taifa. Siku hizi JKT???? Dah! Eti ni miezi 3 (Tatu) kwa wale wa Mujibu wa sheria i.e. Ni kwa lazima. Hawa wa Mujibu wa Sheria ndo wanaotegemewa baadaye kwenda vyuoni kujifunza fani mbali mbali ili mwisho wakirudi waje kutoa Huduma kwa Wananchi na Jamii kwa ujumla. Inashangaza sana kwani Lengo la JKT ni Mafunzo yahusuyo Ulinzi wa Taifa, uzalendo, Ujasiliamali, Ujasili (kupitia mafunzo ya Kilimo, Ufugaji na Biashara) kwa nyakati tofauti tofauti kadri ya maelekezo kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Ukosefu wa UZALENDO
(Hakuna misingi imara ya kuwatrain wananchi kwa jumla wao kuipenda nchi yao kwa dhati)
Mpaka mwisho wa 2010, Hosni Mubarak na wenzie walikuwa wanaishi kama CCM wanavyoishi sasa, wakiamini wameishika nchi hakuna wa kuwatoa.Tunaanzia wapi, kenge hawa wamejiwekea mizizi.
Mtaji wa CCM ni majitu maro, majizi jizi, chenga ama wenye kujitoa akili, watu wasio wazalendo, wabinafsi wenye kujali maslahi yao kwanza,
Ambazo ndio tabia za 90% ya watanzania
Sisi werevuambao tunaona wanatzingua ni asilimia 10 ya watanzania, kazi pevu hii na katika sisi 10% tupo sisi keyboard warriors kwa asilimia 7 katika hiyo 10 yetu.
Tunachomokaje kwenye makucha ya wanasiasa waroho?
Vijana amkeni!Wanajua nchi zao zina majanga ya kiasili so wananchi wameyapokea wanaishi nayo sasa kwetu tunaona Mungu katubariki kila kitu ila kuna baadhi ya wenzetu wanatukwamisha, unakuwaje na furaha hapo
Uzalendo utatoka wapi wakati wanauza bandari, airports, Tazara, mbuga za wanyama.... kila kitu?Ni sahihi kabisa. Zamani kidogo mwanzo wa Azimio la Musoma-1974, vijana - ambao ndo nguvu ya Taifa lolote duniani, walipitia mafunzo ya JKT (mujibu wa sheria na kujitolea) kwa mwaka 1. (mwaka mmoja) na huko walipata mafunzo ya kina na Hamasa iliyoujenga na kuchochea uzalendo wao kwa Taifa. Siku hizi JKT???? Dah! Eti ni miezi 3 (Tatu) kwa wale wa Mujibu wa sheria i.e. Ni kwa lazima. Hawa wa Mujibu wa Sheria ndo wanaotegemewa baadaye kwenda vyuoni kujifunza fani mbali mbali ili mwisho wakirudi waje kutoa Huduma kwa Wananchi na Jamii kwa ujumla. Inashangaza sana kwani Lengo la JKT ni Mafunzo yahusuyo Ulinzi wa Taifa, uzalendo, Ujasiliamali, Ujasili (kupitia mafunzo ya Kilimo, Ufugaji na Biashara) kwa nyakati tofauti tofauti kadri ya maelekezo kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Je, kweli hilo 👆 👆 linaweza kutekelezeka ndani ya miezi mitatu(3)???? Waheshimiwa viongozi wetu kama yupo atakayebahatika kuisoma koment hii; Tusidanganyane hata kidogo. Sisi wote (nyie Viongozi na sisi Raia)ni watu wazima. Tuwe wakweli.
Juzi juzi kulikuwa na mafunzo ya vikosi almaarufu kama Jeshi la Mgambo, Chipukizi (sio wale wa vyama vya kisiasa hapana), Skauti na katika masomo ya Darasani esp. Shule za msingi, kuliwekwa kwa namna fulani Hamasa ya watoto kuitambua na kuipenda Nchi yetu. Siku hizi, Dah! Watoto S/M wamekazaniwa Haki za watoto, Jinsia, Afya ya Uzazi n.k. n.k.
Kwa hiyo tuwafanyeje, au tukishawajua wanaotunyima furaha imetosha?Mpaka sasa comments zinaonesha CCM ndio tatizo la kutukosesha furaha.