Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Tafuta pesa itakusaidia kufurahia maisha yako na familia yenu.
 
Ni kweli mkuu anarchy inaweza kuchangia uhuru na kuwa na furaha ila kwa hasara ya kumwaga damu sana.
hiyo hali imeshazoeleka, kuna generation ya vijana wa Somalia, hawajawahi kuona serikali, ila wansimuliwa unyama waliokuwa wakifanya na serikali ya Gen. S. Barre na seikali zingine
 
Hao ni waongo Tz hatuwezi kuzidiwa na Somalia aisee

Angalia weekend watu wanavyojinafasi, Somalia hii huipati

Tanzania ukitaka kupata furaha achana na mambo ya siasa

Mimi nina furaha kwa kweli
Ni habari njema kama unafuraha mkuu.

Hizo za weekend ni raha/starehe.

"...Kumbe kuna tofauti kati ya raha na furaha, hii dunia ina mambo, do you know that"

Hawa WHR wamefanya utafiti kwa mwaka mzima sio weekend.
 
Ni habari njema kama unafuraha mkuu.

Hizo za weekend ni raha/starehe.

"...Kumbe kuna tofauti kati ya raha na furaha, hii dunia ina mambo, do you know that"

Hawa WHR wamefanya utafika kwa mwaka mzima sio weekend.
Mkuu nielezee maana ya Furaha naona unanichanganya
 
Tutaitoaje jina lenyewe tu Chama cha mapinduzi, je wakitupindua!
Wakitoka tu lazima tuhakikishe wanasambalatika haiwezekani nchi ina almost kila raslimali but, why watu wakose furaha? Kama sio utawala mbovu itakuwa nini shida?!!!😡😡😠😈
 
Mkuu nielezee maana ya Furaha naona unanichanganya
Navyoelewa mimi furaha ni kuwa na hali ya amani,kuridhika na msawaziko wa kihisia(huna huzuni,mawazo,chuki) pale unapopata mambo unayoyataka mfano, kama unataka afya njema,chakula bora,malazi, elimu bora,usafiri, mahusiano bora halafu ukavipata unakuwa na furaha.
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Chanzo cha haya yote ni Lumumba,na kwa Hilo ccm hili linawahusu wanapenda ,watu kila wakijaribu jambo wanapiiga Pini,wavuvi wanalia,wakulima wanalia,,madini wanalia.
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Mkuu badili hiyo profile weka ile ya mwanzo ndo kali, alafu tuendelee na mada
 
Navyoelewa mimi furaha ni kuwa na hali ya amani,kuridhika na msawaziko wa kihisia(huna huzuni,mawazo,chuki) pale unapopata mambo unayoyataka mfano, kama unataka afya njema,chakula bora,malazi, elimu bora,usafiri, mahusiano bora halafu ukavipata unakuwa na furaha.
Mkuu kwa muktadha huu amini kwamba Somalia hawatuzidi hata moja kati ya hayo uliyoyataja

Takwimu nyingine huwa ni za uongo tu wanabuni buni tu

Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Uhuru wa kweli kifikra unahitajika.

Japo kwa Africa uhuru hubomoa kuliko kujenga. Ona kenya wanavyouana kisa uhuru kifikra.

Ona somalia. Na nchi zote hizi zimetuzid ktk hizi ranks husika.
Nadhani uchumi unachangia sana kuwa na furaha, mifumo kandamizi imeweka gap kubwa kati ya tabaka la chini na wenye vipato vikubwa, kuna unyonyaji mkubwa na hii inachangia watu kukosa furaha, elimu ni duni,huduma za afya ni za shida, maji umeme ndio kabisaaa na wanaoumia ni maskini, uchumi ukiimarishwa furaha huenda ikarejea.

Ndio maana kina Luxembourg,Switzerland,USA na Finland wanafuraha sana kwa mujibu wa WHR.
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Ni kigezo gani au ni kipimo gani kimetumika kubainisha uwepo wa hiyo Furaha?
 
Furaha hiyo inatokea wapi? Kwa mikasa ya nchi yetu, unaishi dar na unatumia mwendokasi jua furaha haiwezi kuja, umefungua biashara yako ya kuna kodi msururu furaha huwezi kupata, ripoti ya kagi inatoka unasikia kuna trillions za pesa zimefanyiwa manjengeka kisha watu wanachekeana furaha hauwezi kuipata, unasoma wee una degree ya udaktari unaambiwa uende veta furaha unaipatia wapi, unasikia gesi imegunduliwa dhiki za taifa zinaishia hapo, anakuja kiongozi mwingine anaongea memgina furaha haiwezi kuja.
Mwendazake alikopa na miradi ya SGR, bwawa la umeme n.k ilionekana leo hii pesa imekopwa karibia trilioni 30+ na hakuna cha maana.

We mshahara wako laki 7 unalipia usafiri, kodi ya nyumba, afya, na kila kitu.
Kuna mtu ni anapokea milioni 5 kwenda juu kila kitu kwake ni free, hata gharama ya mafuta hajui, mpaka beki 3 analipiwa na ananiamulia tu kusema
"kama hamuwezi hamieni burundi
" hata mkila nyasi ndege ya raisi itanunuliwa
"kama hamuwezi kulipia, pigeni mbizi.
" umeshindwa kulipa 50k ya kujifungulia kamwambie mumeo achukue mkasi akuzalishe.
 
Nadhani uchumi unachangia sana kuwa na furaha, mifumo kandamizi imeweka gap kubwa kati ya tabaka la chini na wenye vipato vikubwa, kuna unyonyaji mkubwa na hii inachangia watu kukosa furaha, elimu ni duni,huduma za afya ni za shida, maji umeme ndio kabisaaa na wanaoumia ni maskini, uchumi ukiimarishwa furaha huenda ikarejea.

Ndio maana kina Luxembourg,Switzerland,USA na Finland wanafuraha sana kwa mujibu wa WHR.
Ukitumia kogezo Cha uchumi hutakosa validity kwenye hoja husika mkuu. ...

Tz ipo nafasi 11 za Chini kifuraha.

Ila kiuchumi tupo juu Sana kushinda hapo. Na Zaid tazama nchi tulizozizidi uchumi ikiwepo somalia zipo juu yetu kwa furaha sababu watu wake wanao uhuru wa kifikra.

Hapa bongo unaeza ukamkosoa rais na sio kumtukana (ndotoni not in reality yan ndotoni ) af huko huko ukakamatwa na usalama na usiamke milele.
 
Back
Top Bottom