😅Somalia wanafuraha iliyopitiliza kwa sababu hawana serikali ya kuwabanabana na kuwaibia, kila mtu anakula kwa mtutu wake wa bunduki![]()
😅😅Furaha itatoka wapi wakati wewe hata kiwanja kisiju huna ..........mwenzanko mtoto wa kigogo ananunua morroco square apartment na tena wala hana muda wa kuishi wala kuipangisha ipo tu ............
Wanasema hata kama wazungu wakija Afrika na waafrika wakaenda uzunguni baada ya miaka kumi tu, afrika itajengeka kama uzunguni na uzunguni patakuwa kama Afrika!Kwenye computer ikiingia virus unatakiwa upige chini windows utoe uchafu wote uanze upya...hata huku ilitakiwa iwe hivyo hivyo....ilitakiwa raia wote wapigwe chini waje binadamu kutoka pande nyingine za dunia waanzishe maisha mapya
Miaka 10 ni mingi sana, mtu mweusi hana akili ya kukabiliana na baridi kali ya ulayaWanasema hata kama wazungu wakija Afrika na waafrika wakaenda uzunguni baada ya miaka kumi tu, afrika itajengeka kama uzunguni na uzunguni patakuwa kama Afrika!
huku kwetu hayo yamebakia kuwa hadithi hadithi uongo na utamu kolea, ni ndoto tena ya mchana! Tumeishia kuyaona kwenye TV.Wenzetu kama Finland wamewekeza kwenye usawa, afya bure, elimu bure tena yenye viwango. Watoto wa raisi na viongozi wengine wanasoma shule za kawaida na wananchi wengine. Waziri anatumia usafiri wa umma au baiskeli sababu unapatikana kirahisi. Huwezi kusikia mwanamke kafa sababu ya kujifungua. Ukienda kujifungua unakutana na sanduku lenye kila kitu cha mtoto. Wana fao la wasiokuwa na ajira. Waziri au raisi anapanfa foleni kama mwananchi mwingine kupata huduma. Kuna likizo ya kulea watoto wachanga. Usafi wa hali ya juu. Umeme na maji havijawahi kukatika. Maji ya bomba huna haja ya kuchemsha.
Wazee wanapata huduma safi kabisa. Utaacha kuwa na furaha.
Kuna watu walikuwa wanachangia mjadala kwenye blog moja. Lilian Mwasha alikuwa anahojiwa kuhusu usafiri wa daladala. Sasa wameweka kipande tu cha video akisema hawezi panda daladala hata iweje. Ee bwana wee, watu wametokwa mapovu, sijui kwani yeye ana miadi na Mungu, asijitie kiburi na mengine mengi. Yaani unaona watu wana wivu wa kijinga kabisa.Achana na huo utafiti Mkuu wewe unaona watu kama wanafuraha?
Hapa Jf tu ukiwa unasoma komenti asilimia kubwa zinaonesha hamna furaha,tazama tu kwenye huu Uzi pia uone vinyongo vya watu na kutokuwa na furaha wanausapoti uzi vizuri kabisa bila kinyongo kuwa hatuna furaha na sababu wanatoa.
Nchi kama Finland muda mwingi ni baridi hawawezi kuzalisha chakula lakini wamewekeza kwenye mambo mengine ya kuwaingizia kipato.Sio kweli. Kwa mfano Hadi March 2025 (mwaka huu) Maeneo mengi ya Nchi mvua hazijanyesha vizuri. Kwa hiyo Mwakani tunatarajia kuwepo na upungufu mkubwa wa chakula hapa nchini. Tukiwa na njaa tutakosa furaha. Je, hao jamaa CCM wanahusikaje na ukame uliojitokeza? Hao CCM wanauwezo gani kuondosha Ukame? Mbona na wao wanalia-lia kama sisi tusiokuwa na Chama? Mimi nadhani mambo mengine siyo ya Kisiasa na kwa hiyo ufumbuzi wake hautoweza kupatikana kwenye siasa.
Unaonaje kama:-
1. Unapata chakula safi na cha kutosha
2. Unapata huduma nzuri na toshelevu za kijamii e.g Elimu, Afya, Maji, Usafiri, Mawasiliano, Ulinzi na Usalama, Kiimani hubughudhiwi, n.k.
4. Unakuwa na Amani ya moyoni na miongoni mwa Jamii unamoishi
5. Unakuwa uko huru kufanya mambo yako kwa namna unayotaka lakini bila kuvunja sheria zilizopo.
Kama hayo 1-5 yapo na unayapata; utakuwa na sababu gani za msingi kwenda kuikumbatia Siasa???
Lazima wawe na wivu maana ni kama tamthilia fulani hivi hawajawahi kuishi maisha hayo, hata mtu humu akisema hali ugali anakula diet ya maana, mashambulizi yatakua mengi mara unajiona mara hivi mara vile!Kuna watu walikuwa wanachangia mjadala kwenye blog moja. Lilian Mwasha alikuwa anahojiwa kuhusu usafiri wa daladala. Sasa wameweka kipande tu cha video akisema hawezi panda daladala hata iweje. Ee bwana wee, watu wametokwa mapovu, sijui kwani yeye ana miadi na Mungu, asijitie kiburi na mengine mengi. Yaani unaona watu wana wivu wa kijinga kabisa.
Chuki zimewajaa sababu hawana furaha.
Natumaini ni kwema wakuu.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).
Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Samia ndio amekunyima kazi? Ndio alikuzaa? 🤣🤣Mama Samia na familia yake , Kikwete na familia yake na vigogo wa CCM wana furaha sana. Machawa watakuja hapa na kukubishia kwasababu wenyewe binafsi wana furaha sana na pesa za uchawa za Mama huku Watanzania wengi wakiwa hawana furaha wala matumaini.
Sasa utafurahi vipi wakati kijana huna kazi, kura zinaibiwa, hakuna hata wasemaji kura ni fake za polisi na usalama , wapinzani wanaokupigania basi ndiyo wanatekwa na kupigwa risasi. mikataba basi iwe ya wazi hapana ni ya siri na wanawekewa pesa huko nchi za waarabu. Vijana wenye pesa ni watoto wa Samia , kikwete , Pinda na viongozi wengine. Vijana wetu wamekuwa machawa hata hapa tunao! furaha itatoka wapi!
ChoiceVariable
Pascal Mayalla
Mashamba yameisha?Kamundu hali inatisha kesi za kujiua zinazidi kuwa nyingi!
Ajira zinazidi kuwa adimu.
Tsh inazidi kufa thamani dhidi ya dola $.
Deni lataifa ndio hilo linaenda $100T.
Umeme waliahidi watauza mpaka nje ila sasa wananunua kukidhi uhaba kanda ya kaskazini!
Hao wote sio Watanzania wanaofanya Bali ni Waarabu au siyo? 🤣🤣Hamwezi kuwa na furaha kama huduma za msingi kila mahali ni mbovu na hadi utoe rushwa ndo shauri lako lifanyiwe kazi.
Hamwezi kuwa na furaha kama watoa huduma ni watu wasiojali. Kwa mfano mzee ambaye ni mwanachama wa PSSSF amekuwa akichangia sasa kastaafu lakini kuja kupata mafao yake hadi azungushwe na bado akutane na kikokotoo.
Unatakiwa kujisemea mwenyewe usijumuishe.Natumaini ni kwema wakuu.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).
Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Jisemee wewe usijumuishe wengine kukosa furaha.![]()
Happiest Countries in the World 2026
Finland (7.74), Denmark (7.52), and Iceland (7.52) are the world's happiest countries in 2026. Explore global happiness rankings and the factors behind high life satisfaction.worldpopulationreview.com
ChoiceVariable machawa mtashangaa sana tunasingiziwa eee!! Huu ni uongo eti
Unalima wapi kwanza, unalima kwa pembejeo zipi? hata ukifanikiwa unauza wapi? hata ukiuza mda wa kuuza bei unapangiwa! wanadai kilimo ni uti wa mgongo ila mkulima serikali haimjali mkulima anachukuliwa kama mtu aliefeli maisha.Mashamba yameisha?