Kwanini sisi wakulima tunateseka ivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini sisi wakulima tunateseka ivi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chokambayaa, Dec 5, 2010.

 1. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mimi mwananchi wa kawaida kabisa ninayeishi kijijini
  Tatizo kubwa tulionalo ni umasikini tunaoishi nao
  Tunategemea kilimo sana (kilimo ndio uti wa mgongo) I use to hear…
  Lakini ki ukweli tunataka kuacha kulima kwa sababu tumedharauliwa na kusahauliwa kabisa
  Tumeshindwa kuacha kulima kwa sababu hatuna mbadala….
  Mbole (simenti, bati, mafuta ya taa, powertilar) ni bei juu sana kuna issue ya vocha za mbolea (ruzuku ya serikali)
  Mkulima masikini anapaswa kuwa na almost shs laki moja na ushee ili
  Uweze kutumia package ya mbolea ya ruzuku kupandia, kukuzia na mbegu nk..Hivi bibi, babu na mjombako kule Kijijini anapata wapi hizo fedha?


  Haya tunapovuna mazao yetu tunapangiwa bei (pamba, kahawa) na pa kuuzia ….. kuuza nje marufuku….
  Hivi mnataka tufanyeje? Tumlilie nani?
  Kwanini wakulima tunateseka hivi…..hizo mnazoziita Sera, itikadi na ….wala hazitusaidii zipo ktk makaratasi yenu tuu.
  TUMECHOKAAAAA!!!!!!!!!!!!!
   
 2. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi ujao pigia kura chama sahihi na kilicho na sera madhubuti.....
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wakulima - kwa bahati mbaya sana - hawana mtetezi! Serikali haina habari nao kwani kila siku ni kuwadanganya-danganya tu. Siku wakipata watetezi wa kweli serikalini ndiyo tutajionea mabadiliko ya kweli katika jamii yetu kwa sababu wengi wa wananchi wetu ni wakulima.
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa bahati mbaya sana, wakulima na wamachinga ndiyo wanaoongoza kwa kulialia maisha magumu, na haohao ndiyo siku zote wanaoongoza kwa kuipigia kura CCM. Sasa sisi tuwasaidieje? Nendeni mkamuulize mliyempa kura zenu. Kwani si mlimpa kura ili awasaidie? Na mtateseka sana tu, hadi hapo mtakapojifunza kuchagua chama makini.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mtetezi wa wakulima atakuwa nani ilihali waliopo kwenye system hawajui hata jembe linashikwaje? Fanya analysis ya wabunge wote, halafu useme kama kuna mmojawapo ambaye kilimo ndiyo hasa chanzo chake cha mapato. Kwa kiasi kikubwa utakuta wengi wanalima kama sehemu ya burudani. Wana mashamba ambayo ni mahali kwa kupumzika siku za weekend. Sasa wabunge kama hao ambao ni wafanyabiashara wakubwa na mafisadi watajua lini kama kilimo kinahitaji utetezi? Huwezi hata siku moja kutegemea mtetezi wa wakulima kutoka katikati ya wafanyabiashara wakubwa na mafisadi ambao hawakuwahi kulima. Hicho ni kilio tu kwa wakulima. Wanalo hilo!!!!
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  [​IMG]:A S 114:
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wabunge karibu wote wa nchi nzima wanaishi kinondoni matatizo ya wakulima watajua wapi?
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  vipi?

  ulipata mgao wako wa fulana ya kijani na kofia ya njano?
   
 9. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakika naadhani wana JF hamjabahatika kwenda remote areahivi karibuni

  Yaani hakika mbolea ndio issue yaani akitokea mtu mfano CDM, CUF, NCCR
  akaweza kutoa ufumbuzi wa bei ya mbolea na upatikanaje wake huku Kijijini
  kura zote za 2015 za wakulima anakula...

  Hali ni mbaya sana ni ugomvi kila siku na viongozi wao (maafisa kilimo)
  Kura walipigia upinzani (wengi wao) ila zilichakachuliwa sasa wamlilie nani
   
 10. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Mmejiandaa vipi na kudhibiti uchakachuaji?
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha kuchakachua wala nini! Kwa nini hazikuchakachuliwa Arusha mjini, Iringa mjini, Mbeya mjini, Msoma mjini, Nyamagana etc? Nyie mliuza kura zenu kwa tshirt na kofia bwana!!! Hakuna haja ya kulalamika wakati mnaenjoy tshirt na kofia za bure.
   
 12. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hapo kweli mkuu lakini mbona wengi wao ni watoto wa wakulima
  wameishi vijijini na wamesomea huko
  au ndo mwenye njaa.......
   
 13. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2010
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Inasikkitisha ukulima wengi bongo wanakuwa hawawezi kuishi vizuri, nchi zilizoendelea zingine wakulima wanapesa sana na wengi wanakuwa matajiri
   
 14. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mijini wanaufahamu wa maisha kulikoni huku tulipo
  Kuishi mjini tuu tayari ni form four

  Huku mmetuacha wenyewe hakuna wa kututetea hata kampeni zenu nyingi
  mlifanyia mijini huku hata matawi hamjafungua mnategemea nini
   
 15. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapa liko obvious that our leaders/administrators are men,actually men, who didn't grow up in their local equivalent of Ifakara or Njombe. If they had, one suspects their view of the government of the day would be somewhat more jaundiced and confrontational! As you may know that our colonial masters dubbed today as donors used to set prices for our dear fathers/ peasants, and today they regard our leaders (mawaziri and presidents) when they meet in wooden panelled offices to discuss the fate of wakulima wa tanzania na africa kwa ujumla as their social equals! kwa hili wakulima wataendelea kuwa maskini! :A S-alert1:
   
 16. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,438
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Mtu wa kwanza kumbadilisha ni wewe mwenyewe, achana na kufanya kazi kivyako vyako ungana na wenzio kuunda kikundi ambacho mtatumia kama chombo cha kusemea na kutafuta masoko na kutafuta taarifa.

  Kama umekuwa ukifanya hivyo muda wote na hubadiliki, you must change sasa mchakato wa maendeleo hauna short cut ni kama kifo lazima u-experience. Achana na siasa na kutafuta mchawi songambele wengine watakufuata ukianza safari.

  Avatar yako imenikumbusha marehemu Musiba (RIP) na kitabu chake cha usiku wa balaa enzi hizo.
   
 17. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  There is no single linear equation to development.
   
 18. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Yah nimesoma sana vitabu vyake MUNGU amrehemu

  Ndugu yangu songambele vikundi tumeunda sana, vyama vya kuweka na kukopa tumeanzisha sana
  lakini hakuna jipya mabilioni ya kikwete yanaishia mijini sisi hatupati fursa eti
  tutashindwa kurejesha...

  Huku michango ya serikali kila kukicha
  Kuchangia ujenzi wa sekondari, zahanati, ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji, shule ya msingi, bweni...akhaaa
  na usipochangia utakiona cha mtema kuni Mtendaji anawewe.....

  Tumlilie nani....
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  tatizo niserikali yetu kukubali sisi kuwa chanzo cha utajiri wa nchi za magharibi na makampuni makubwa kama nestle, starbuck nk kwa vimsaaada kidogo tunaopata na nafasi wanazo pata hao vioongozi wetu.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  si nasikia kuna mh anaitwa mtoto wa mkulima? Ila mtoto wao karithi kilimo cha siasa. Sio hicho chenu cha pamba na mahindi. Nawe ndugu nakushauri uanze kulima siasa
   
Loading...